"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, July 12, 2008

Jinsi ya kuthibiti hasira

Hawa kweli walikuwa wanazipiga au utani? mbona kuna jamaa kule ukutani anachapa uji (kikombe na kijiko) wakati wenzake wanazipiga na wala hawaamlii? WAKATI mwingine, hasira na kuchanganyikiwa kwetu kunasababishwa na matatizo yasiyozuilika katika maisha yetu ya kila siku.
Si kila hasira haina mpangilio, na mara nyingi inatokana na mambo ya kiafya, ni hali ya asili inayojitokeza katika mambo tunayokutana nayo.
Njia sahihi ya kukabiliana na tatizo linalokukabili, ambalo linakusababishia hasira, si tu kulenga katika kutafuta muafaka, lakini zaidi ni jinsi gani ya kulichukua na kukabiliana nalo.
Kutatua matatizo yanayokusababishia hasira kutaleta matokeo mazuri, lakini pia si kujiadhibu mwenyewe kama jibu halitakuja kama ulivyotarajia.
Watu wenye hasira mara nyingi hurukia jambo na kulifanyia maamuzi, lakini baadhi ya maamuzi hayo yanaweza yasiwe sahihi.
Kitu cha kwanza cha kufanya kama upo kwenye majadiliano makali ni kupunguza hasira na kufikiri juu ya majibu yako unayoyatoa.Katika majadiliano hayo, kamwe usiseme kitu cha kwanza kinachokujia kichwani pako, bali tuliza hasira na fikiri kwa uangalifu juu ya kile unachotaka kukisema. Wakati huo huo, sikiliza kwa makini mtu mwingine anachokisema na jipatie muda kabla ya kujibu.

Kwa habari zaidi soma makala nzima kama ilivyoandikwa na dada Lucy Ngowi kwenye blog yake

http://lngowi.blogspot.com/2008/06/jinsi-ya-kudhibiti-hasira.html


No comments: