"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, July 31, 2008

Koteka

Huko Papua New Guinea (angalia ramani hapo chini) kuna kabila la Kombai ambalo bado wapo katika traditions zao na wanaume huvaa kivazi hicho (picha ya juu) kufunika nyeti zao.

Picha ya chini mwanaume wa hilo kabila akiwa amevaa hilo kufuli tayari kuendelea na shughuli za kila siku kwa ajili ya kutafuta mlo wa familia.
(shughuli kubwa ni uwindaji)

Picha ya juu wanaume wa hilo kabila wakiwa kwenye pozi bila wasiwasi.


Picha ya chini akina mama nao wakiwa katika pozi wakionekana natural kabisa


Ramani inayoonesha Papua New Guinea mahali ilipo
Source: http://en.wikipedia.org/wiki/Koteka

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hapo ipo kazi, Ila nina swali je wanalaleje. Halafu wananifurahisha ni lazima wanabana sana matumizi ya nguo.

Lazarus Mbilinyi said...

Kweli dadangu hapa kazi kubwa!
Unaambiwa hawa ndugu zetu hadi leo bado wanadumisha mila zao na miaka ya karibuni walikuwa hawajui kama duniani kuna watu zaidi ya wao kwani waliamini wapo wenyewe tu duniani.

Usiku wakitaka kulala wanavua hizo kufuli zao na kuzitundika kama mimi na wewe tunavyofanya na wakiamka asubuhi wanavaa kama tunavyovaa sisi. Ila ndo hivyo ni kweli wanabana bajeti ya nguo na pia nahisi mali zinalindwa kwelikweli naona FBI hawaoni ndani.

Mimi wasiwasi wangu ni jinsi ya kukimbia tu maana nahisi hapo itakuwa shida kidogo!

Yasinta Ngonyani said...

Mmhh sikuwaza sana kuhusu kukimbia kwani binafi ni mkimbiaji maarufu yaani kufanya mazoezi. ni kweli watakimbiaje.kwani wao ni wawindaji

Anonymous said...

Your blog keeps getting better and better! Your older articles are not as good as newer ones you have a lot more creativity and originality now keep it up!

Anonymous said...

I just added your website on my blogroll. I may come back later on to check out updates. Excellent information!