"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, July 17, 2008

Ndoa; kama kujenga Nyumba

Kujenga ndoa kuna fanana sana na kujenga jengo lolote kama nyumba tunazoishi.
Kwanza unaanza kwa kuwa na michoro mizuri (plan) na hatimaye unajenga jengo lenyewe.
Ndoa ni mahusiano ya juu sana kwa binadamu ni maamuzi ya ku-share moyo, akili, mwili; vyote kwa pamoja.

Katika kujenga jengo lolote suala la vifaa (material) haliwezi kukwepeka kwani ndivyo husaidia jengo kusimama na ndoa ni hivyo hivyo kuna tools ambazo lazima utumie katika kujenga ndoa imara.

Kabla ya kununua hizo tools za kutumia kujenga ndoa kumbuka kwamba wewe na mwenzi wako wote mpo timu moja na lengo si kushindana kwani hatuhitaji mshindi bali tunahitaji kufanya kazi kama timu.
Ndoa si nani anashinda bali ni wanandoa wote kuelekeza nguvu kusukuma au kuvuta kama kuelekea upande mmoja.
Katika ndoa si lazima ushinde kila mgogoro unapojitokeza na wewe kuwa sahihi kuliko mwenzio bali ni kusaidiana na kumtanguliza mwenzako.

Kifaa cha kwanza ni kuwasiliana.
Ni muhimu kuwa na mwasiliana ya pamoja kila siku. Tunapozungumzia mawasiliano tunaenda katika nyanja zote zinazomuhusu mtu pamoja na kuhusisha milango yote mitano ya fahamu yaanu kuguswa, kunuswa, kusikia, kuonana na kuonja hahaha!
Hapa ni mawasiliano ya kihisia, kiakili, kimwili na kiroho

Kihisia (Emotionally): jitahidi kutiana moja kati yenu na pia fahamu kwamba katika kuwasiliana ni asilimia 7 tu ni maneno asilimia 93 ni jinsi ya tone ya sauti yako na body language. Jinsi unavyoonekana wakati mwenzako anaongea na sauti yako unavyojibu huwasilisha hisia zako kwa mwenzi wako hivyo uwe makini kuhakikisha humuumizi. Watu wanapanda gari wote kwenda kazini na hawaongei hadi wanafika na hata wakiongea majibu ni mkato tu, kihisia hapo kuna jambo.

Kiakili: je, kuna gazeti umesoma na kuna kitu kimekufurahisha nawe wataka mwenzi wako ajue?
Mweleze basi. Je, una story yoyote unataka kumsimulia mkeo au mumeo msimulie basi.

Kimwili: mpe miguso mingi tu ambayo si ile ya chumbani wakati unataka ile kitu. Mkumbatie, mbusu, mshike mkono, unampompa mguso (touch) maana yake unamjali na touch ni hitaji la msingi la binadamu. Kama mnaweza oga pamoja it is so fun and so nice.

Kiroho: kuna wanandoa wengi husahau kushirikiana katika mambo ya kiroho hata kama wapo imani moja. Unahitaji kumuombea mwenzi wako, na pia unahitaji kuomba pamoja kama wanandoa hii husaidia kuinua mahusiano yenu. Imba pamoja nyimbo za kumsifu Mungu. Soma Neno kwa pamoja na kila mmmoja kushiriki kutafakari.

Kifaa cha pili ni kubariki
Mbariki mwenzi wako kila iitwapo leo.
Anza leo kutoa maneno ya baraka kwa mume wako au mke wako hata kama hukuzaliwa familia ambayo imekuridhisha kumbariki mwenzako.
Mpe sifa anazostahili kwa mambo mazuri anafanya, inawezekana anafanya kazi kwa juhudi, anapika vizuri, anakutunza vizuri, anakupenda, anakurishisha kitandani, mwambia “asante, nakupenda, pole sana, ubarikiwe, unapendeza nk.
Hata kama wewe ni mgumu mno kutoa neno la baraka basi anza leo kwa neno lolote dogo unaloona mwenzi wako amekufanyia.

Kifaa cha tatu ni kushirikiana
Shirikiana mambo mengi katika maisha kwa kadri mnavyoweza.
Kuwa pamoja katika muda, mawazo, kucheza, kutazama TV program pamoja, kikombe cha kahawa au chai pamoja, kusafisha nyumba pamoja, kuendesha baiskeli pamoja., kula chakula sehemu pamoja, kufanya vitu mmoja anapenda pamoja nk.
Mnapotumia muda pamoja husaidia kuwaunganisha zaidi na kuwa kitu kimoja.

Kifaa cha nne ni kuitia bila kulaumu kwanza
Usibishe, itikia kwa kukubali kwanza. Jinsi unavyoitikia kuna elezea zaidi kuliko vitendo wakati mwingine.
Je, kama mume wako au mke wako amechelewa kurudi nyumbani, na hajapiga simu, huwa una respond vipi. Kitu cha msingi si kurukia na kuanza kulaumu bali kwanza kumsikiliza na kujua sababu ni ipi kuliko kulalamika na kuanzisha moto au zogo la nguvu.

"Ndoa haijengwi wa vitu tunavyonunua dukani tu, bali hujengwa kwa upendo kwanza"

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Upendo, Kupenda ni nini? na mapenzi ni nini? Nina maana kama mtu anakuambia NAKUPENDA je wewe utadefine vipi? Na Jingine kama mke au mume anakuwa na wivu sana kwa mwenzake hii ina maanisha nini?

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,
Ni Neno Upendo ni moja ya maneno muhimu sana katika maisha ya binadamu pia kujua upendo ni nini limekuwa swali gumu sana duniani kwa sababu kwa upendo dunia imefanyika mahali bora kuishi na wakati mwingine kwa upendo kumetokea vitimtim kwelikweli hasa linapokuja suala la mapenzi.
Naamini si muda mrefu tutaangalia neno upendo, kupenda na mapenzi kwa ujumla ili tupate uzoefu zaidi.

Upendo daima!