"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, July 30, 2008

Office Romance

Mapenzi mahali pa kazi au maofisini ni kitu cha kawaida sana kusikia siku hizi, hii ni kwa sababu kushuka kwa nidhamu makazini na kwamba tunatumia muda mwingi sana kuwa ofisini kuliko nyumbani hivyo wafanyakazi huwa na muda wa pamoja kuliko hata familia.

Urafiki wa mapenzi ofisini kama hujaoa au kuolewa unaweza kukusaidia kuoa au kuolewa au unaweza kukusababishia madhara makubwa kiasi cha kufukuzwa kazi au kufungwa jela na kupata magonjwa kama UKIMWI, kuharibu taaluma yako na sifa zako, pia kuvunja ndoa za wengine kitu ambacho ni hatari zaidi.

Pia suala la mapenzi kazini huweza kusababisha kuzorota kwa utendaji na ufanisi binafsi wa mtu kazini.
Mapenzi na kazi ni vitu viwili tofauti sana ndiyo maana waajiri wengi hawaruhusu watu kujihusisha ma masuala ya mapenzi kati ya wafanyakazi.

Pia kuna utafiti unaonesha kwamba (Vault.com) nusu ya watu wanaofanya kazi maofisini huvutiwa kimapenzi na mtu mwingine wa jinsia tofauti katika ofisi moja na wengine hupelekea hata kuoana kabisa.

"Si vema kuchanganya biashara, kazi na mapenzi ofisini"

Wapo watu wamejitoa muhanga kuwaridhisha mabosi wao kwa mapenzi ili kujihakikishia kupata kazi nzuri au kuongezewa mshahara, au marupurupu au kupewa visafari kikazi au kupelekwa kusoma nje ya nchi, hata hivyo matokeo yake ni kudhalilika na wakati mwingine kujipatia bonus ya magonjwa kama HIV/AIDS.
Pia wapo mabosi au waajiri ambao bila kutembea (sex) na mtu anayemwajiri bado hajakamilisha taratibu zake za kuajiri, hii ni tabia mbaya sana na si ya kistaarabu.

Je, hali ipoje katika ofisi yako kuhusiana na suala la mapenzi kazini au ofisini?
Je, katika ofisi zetu za serikali hali ipoje?
Na huko kwenye sector binafsi hali ipoje?

Naamini kila mmoja wetu ana jibu kwa haya maswali1 comment:

Anonymous said...

Kwa kweli kwa ofisi za serikali ni too much kwa suala hili la mahusiano sehemu za kazi hadi sasa Wizara ya Afya wameamua kuanzisha mpango wa kufundisha maambukizi ya ukimwi katika sehemu za kazi, lakini hii ni kwa ofisi zilizo chini yake tu. Unajua tatizo la mahusiano makazini ni ile kuwa age moja na utani uliopitiliza. Utakuta watu wanataniana [sweetie, honey, darling} na sometimes wana act kama kweli na kushikana sehemu sensitive na hii inapelekea kuzama kabisa.

Suala lingine ni kuwa kuna watu wao ngono kwao ni kitu cha kawaida tu. Mbali na utani wa maofisini kingine kinachochangia ni kuwa ofisi nyingi wanaajiriwa wafanyakazi wengi kwenye cadre moja so utakuwa kazi zinakuwa chache sana kwa wafanyakazi na kupelekea kukosa shughuli za kufanya na kubaki kutaniana na kuongelea mambo ya mapenzi wengine hata tongue kiss kabisa.

Kwa mabosi, mabosi wetu wengi tatizo kubwa huwa hawawachagui wafanyakazi wale wanaopaswa kuchaguliwa kwa kufuata pass rate zake za interview na ingewezekana kabisa interview zingekuwa zinafanywa na watu ambao hawako katika ofic husika na wala hawana interest zozote. Utakuta interview imepita na watu wamechaguliwa, bosi anasema kuwa mimi ndio nimefanya efforts hadi wewe uchaguliwe, then sasa utanipa nini. Yeye mwanaume na wewe ni mwanamke, ukimwambia kuwa mheshimiwa niko tayari mshaharawangu wa kwanza ule wewe atakuambia kuwa hana shida ya hela. Kwa hiyo unakuta ajira nyingi zimetawaliwa na rushwa ya ngono siku hizi.

Wengine wameshaajiriwa ila tu bosi anakupenda hapo inakuwa shida maana atafanya vitimbi kama umemkatalia matakwa yake kiasi kazi utaiona chungu. Ni kama pepo linawakumba watu, utafuatiliwa inapelekea kupunjwa mshahara, na mambo mengi yanayokuhusu wewe kutotimiziwa au kukwamishwa kwa sababu tu hujawa tayari kutoa ngono ila ukiwa mwepesi kwa hilo utapata favour zote ila madhara ni kuwa na magonjwa juu.