"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, July 9, 2008

Tabia zinazokera katika ndoa

Wengine hata siku moja hatandiki kitanda na wengine wamewaachia mahouse girl wawatandikie vitanda vyao.
Kuna tabia nyingi sana kwenye ndoa ambazo husumbua sana hata kufikia mahali kwa wengine kuhatarisha uhusiano wao kwa sababu mtu huendelea kurudia kile kile hata akiambiwa na mwenzake.
Mfano wa tabia ambazo husumbua sana kwa baadhi ya wanandoa ni kama vile:-Kuchelewa yaani kutojali muda.
Kuendesha vibaya gari na kuwa na ufahamu mdogo sana kujua maeneo.
Kutosaidia kazi za nyumbani hata kama mwenzake akiwa amechoka.
Kushika remote na kutaka wote kuangalia channel moja ya TV ambayo yeye anataka.

Kutojali usafi wake mwenyewe au kuwa mchafu, kunuka mdomo na soksi.
Kulalamika mbele za watu au kulaumu mwenzake mbele za watu.
Kutumia muda mwingi kuwa tayari kwa kila kitu.
Kushindwa kuchagua nguo au kuwa mbishi pale mwenzake anapendekeza nguo za kuvaa.
Kuwa ovyo katika masuala ya vyakula, hataki kula au kuchagua mno.
Kutorudisha vitu mahali pake baada ya kutumia.
Kuacha taa zinawaka.

Je, ni tabia gani mumeo/mkeo au mchumba wako anazo na zinakukera?

2 comments:

Fikirikwanza said...

Hallo salut
Naona Mzee kihalali leo kajitahidi kitanda kikubwa ,kakofia kake kakaweka fresh,na kataulo kake kananing'inia fresh kabisa ila tuu amesahau kukusanya vijishuka vyake hivyo na kuvitia kwenye kamfuko aka_arrange kwenye one ya vibongondzera . Ila wamiliki wa hii room pengine wanainjoy life kama kawaida kwani nani huingia kwenye hiyo room yao na kama akiingia atakuwa anatafuta nini?
School ya leo ni bomba ili swala si kumwambia mtu juu ya tabia yake bali,tatizo ni namna gani ambavyo unaweza kumwambia huyo partener wako. Kila mtu anafanya makosa lakini vipo vijamaa vyenyewe vinajifanya vilizaliwa havifanya makosa na hata vikikuelewesha ni kuudhi tuu.
Ni adhali usubiri hadi wakati sahihi wa kumwelekeza huyo ?? juu ya hiyo tabia yake kutumia sufuria kama sahani kuliko kumwambia halafu asikusikilize maisha yenu yote ya ndoa. nani asiye penda kuona mabo yapo smart? .Mimi mwenyewe i love it na nini amini nadni ya ndoa kuna shule nzuri na inayo hitaji bidii kuliko ile tuliyo ifanya tulipo jifunza a,e,i,o u.
Thank you wasalimie Ima na Mama manu.

Lazarus Mbilinyi said...

Sidhani kama mzee Kihalali ana muda wa kuwa na kitanda kama hicho kwani kwanza kutokana na kilivyo atakuwa anachelewa kwenda Msasi kuendelea kulima miwa yake, isitoshe hata kuwa anapata usingizi mzuri kwani yeye amezoa kile kitanda chake cha ngozi na mkeka wake na lile blanket jeupe ambalo sasa hivi ni jekundu si unajua hawezi kufua eti jua haliwaki na anakosa muda. Sasa hivi yupo busy na vinyungu kule Msasi ndo maana kitanda kinaonekana halaliwi!