"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, July 29, 2008

Tendo la ndoa katika umri mkubwa (II)

(Picha kwa hisani ya Corbis.com)
Kuna imani potofu nyingi kuhusiana na tendo la ndoa katika umri mkubwa zifuatazo ni baadhi tu ya hizo imani;
Kushindwa kushiriki tendo la ndoa ni matokeo ya umri kuwa mkubwa.
Tendo la ndoa ni hatari kwa wazee wenye umri mkubwa.
Uwezo au hamu ya tendo la ndoa (libido) hupungua kwa kadri mtu anavyozeeka.

Yote hapo juu si sahihi kabisa.
Hizo imani potofu zipo kwa muda mrefu na zimekuwa zikisababisha watu wenye umri mkubwa (wazee) kushindwa kufurahia tendo la ndoa au uumbaji wa Mungu.

Je, mabadiliko ya mwili kwa wanaume wazee huathiri vipi tendo la ndoa?
Kawaida wanaume wazee huhitaji muda mrefu ili kuweza kusisimka.
Kile kilichokuwa kinahitaji sekunde chache hadi dakika chache katika umri wa miaka 19 huhitaji zaidi ya dakika 15 katika umri mkubwa kwa mwanaume.

Wanaume wengi wenye umri mkubwa hupona ugonjwa wa Kukosa uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa kujifunza matokeo na athari za umri kwenda sana (Uzee) Katika umri ulioenda wanawake wazee wahahitaji kufahamu kwamba wanaume wazee huhitaji muda mwingi na wakutosha kuuandaa jogoo awike.

Mabadiliko mengine ambayo hutokea kwa mwanaume mzee sana ni kupotea kwa uwezo wa kufika kileleni tofauti na wakati akiwa kijana.
Hii ni kutokana na Kukosa hisia (sensation) za tendo la ndoa.
Pia kiwango cha sperms anazotoa hupungua hivyo mwanamke mzee asiwe na mtazamo wa kudhani kuwa uwingi wa sperms ndio uzuri wa tendo la ndoa.

No comments: