"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, July 4, 2008

Unataka Mke Asipende Tendo la Ndoa!

Ukifanya haya Yafuatayo mke wako atajitahidi sana kukwepa tendo la ndoa hasa kama unahisi hupo interested sana na sex na hutaki kusumbuliwa.

Isipokuwa kama unataka kuwa na uhusiano mzuri na kufurahia tendo la ndoa na mke wako basi achana kabisa na tabia Zifuatazo.Hakikisha unakuwa na utaratibu usiobadilika yaani muda ule ule, sehemu ileile, kitanda kile kile na style ileile miaka nenda miaka rudi wakati wa tendo la ndoa.

kama una harufu mbaya basi Jitahidi kila unapotegemea kuwa na tendo la ndoa hiyo harufu mbaya inakuwa maradufu.

Mguse mwili wake pale tu Ukitaka tendo la ndoa.

Usimbusu wala kumkumbatia, au kushikana naye hadi pale ukiona inataka sex tu, kwa njia hiyo akiona unambusu au unamkumbatia au unamshika atajua unataka sex, unakuwa unamrahisishia sana maana anajua alama zako kwake kupata sex.


hakikisha unamlazimisha kufanya tendo la ndoa, awe anataka au hataki wewe ndo kichwa cha nyumba lazima akusikilize na tendo la ndoa ni haki yako, Umetoa hata mahari halafu anakata?

Kama unaona anakupa dalili kwamba hana interest na tendo la ndoa usikubali, wewe ni kichwa cha nyumba anahitaji kukutii.


Usipoteze muda mwingi kwa ajili ya maandalizi (foreplay) nenda moja kwa moja kwenye shughuli yenyewe.

Kwa nini utumie muda wako kufanya vitu ambavyo ninakupotezea muda, hata hivyo kwa nini mpoteze muda mwingine kwa kubusiana, kushikana shikana, kuchezeana wakati mnahitaji kulala na kesho kwenda kazini? Siyo busara kupoteza muda wakati mna majukumu mengi muhimu.

kama hana jipya wakati wa kufanya mapenzi mwambie ajirekebishe na mwambie wakati ule mpo kwenye tendo la ndoa, na kama hana ujuzi mwambie pia kwani kwa nini yeye asiwe na ujuzi wakati wanawake wengine wana ujuzi yeye ana Matatizo gani. Si vizuri kubaki kimya wakati unaona hana jipya au hana skills zozote kitandani.


Kama mwonekano wake anatatizo mseme sana. Kama ameanza kunenepeana mpe vidonge vyake na mwambie ukweli jinsi anavyokufanya upoteze hamu ya kufanya naye mapenzi. Hiyo inampa motivation yeye kujirekebisha au kupunguza unene wake.

Kama hufurahi kitu chochote kuhusu yeye mwambie on the spot na uwe serious kama mwanajeshi vile.


Kama umepigiwa simu wakati upo kwa tendo la ndoa basi unaweza kuacha kwanza then pokea simu kwani huwezi kujua simu ina umuhimu gani. Unaweza kufanya sex muda wowote kwa nini uzime simu au uache kupokea? Inawezekana ni miaka sasa umekuwa unapata sex kwa nini mke akasirike kwa wewe kupokea simu?

Wakati wa Tendo la ndoa wale usimuumize kitu chochote, wewe assume kila kitu kilo fine, labda yeye kuuliza.

Usipoteze muda kuwa na maongezi ya faragha na yeye, ukiona yupo tayari kwa tendo la ndoa hakikisha unafanya haraka iwezekanavyo ili upate muda wa kulala kama ni usiku. Pia kwa nini uwe na maongezi wakati hata kesho mnaweza kuongea. Usipoteze muda wakati tendo la ndoa ni haki yako.

Hakikisha tangu asubuhi unakuwa na majibu ya mkato kwa maswali anayokuuliza, jibu kavu kavu. Ukiona anakulazimisha kukuongelesha Jitahidi kuzira kabisa. Pia achana na mambo ya kusifiana ukiwa na mke wako wenyewe au hata mbele za watu.

Jitahidi kuwa kutozoeleka na mke wako, yaani awe anakuogopa kama simba hata ukirudi nyumbani ajione kweli sasa mume kaja mnyime kabisa uhuru kwani ukikosea akajua wewe ni dhaifu atakutawala kitu ambacho ni aibu sana kwa mwanaume.

Usitegemee kuwa na ndoa imara kama utafanya haya, ni muhimu sana kuyakwepa kwa uwezo wako wote.

Pia utamu na furaha ya ndoa ni kuishi kwa upendo, furaha na amani na kuridhishwa kimapenzi.

Achana kabisa na hizi tabia!

2 comments:

Anonymous said...

Mbona mnataka hizi pilipili ziwe sayansi kama ile ya uhandisi?.

Anonymous said...

mh inatisha,mbona ukauzu