"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, August 10, 2008

Angalia uwezekano si Kikwazo

Wanawake wengi (siyo) wote hulalamikiwa sana na wanaume kwamba baada ya kuolewa hujisahau kwenye masuala ya kujiweka safi na kujipamba tofauti na enzi wakati wapo single.
Hata hivyo wapo ambao wanatia moyo sana hadi wanaume hujisikia fahari.
Ni muhimu kusoma saikolojia za mume wako zipoje ili aridhike na mwonekano wako.
(Picha kwa hisani ya A. H )

Angalia uwezekano pale wengine wanaona ni kikwazo!

Kila mahusiano, kuna uwezekano wa kuona ushahidi unaonesha kwamba hayo mahusiano hayawezi kufika mbali.
Hata mahusiano yanayoonekana ni imara zaidi bado hupita kwenye matatizo na vikwazo ambavyo hutoa ushahidi kwamba kuna uwezekano hayo mahusiano yanaweza yasifike mbali.

Swali halisi ni hili,
Je, unatia mkazo kwenye ushahidi upi?
je, ni uimara (strength) au udhaifu (weakness)?

Ku-focus kwenye udhaifu uliopo hupelekea kuharibu zaidi mahusiano wakati kuelekeza nguvu nyingi kwenye uimara wa yale mahusiano hupelekea mahusiano kuwa imara zaidi.

Hii ina maana kwamba wakati wowote katika ndoa yako au uchumba wako unapokutana na shida au migogoro au matatizo jambo la msingi ni kuwa na mtazamo chanya na kuangalia mambo mazuri yanayojenga mahusiano kuliko kuangalia udhaifu wa mwenzako na kuchukulia ndiyo kitu cha msingi au jambo la maana zaidi.

Fahamu hakuna binadamu ambaye ni mkamilifu na sahihi wakati wowote, labda uende sayari zingine lakini sayari ya dunia (earth) haina mtu mkamilifu ambaye anaweza akaishi na wewe na ukaridhika asilimia 100.No comments: