"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, August 29, 2008

Barack & Michelle Obama

Barack na Michelle
wakati wa 36th NAACP image Award Los Angeles, California in March 19, 2005
Kwa sasa Jina la Barack na Michelle Obama limekuwa ni jina maarufu sana pande zote za dunia.
Barack Obama amefanya kile ambacho wengi hawakutegemea na bado habari zake ni gumzo kwa kila mmoja, ukubali au usikubali ukweli ni kwamba yeye ana uwezo wa tofauti.
Kwa sasa amepitishwa kuwa mgombea rasmi wa urais wa nchi ya Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic.
Ni vizuri kupitia habari zake kwa upande wa ndoa yake ili tuweze kupata lolote la kujifunza.
Barack na Michelle Obama walizaliwa lini?
Barack kwa kifupi Barry Hussein Obama alizaliwa August 4, 1961 Honolulu, Hawaii.
Jina lake linatokana na neno la Kiswahili “Baraka” kwa maana kwamba “Aliyebarikiwa” alikulia Hawaii na Indonesia.
Michelle Lavaughn Robinson alizaliwa Chicago, Illinois January 17, 1964
Picha chini ni Barack na Michelle wakiwa na wazazi wao (Marian Robinson mama wa Michelle na Ann Danham mama wa Barack) siku ya harusi mwaka 1992 Je, Barack na Michelle walikutana wapi?
Barack na Michelle walikutana mwaka 1989 wakati Michelle alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya wanasheria kutoka Havard na Michelle anasema kilichomvutia kwa Barack ni ule uwezo alionao kujihusisha na wengine na jinsi watu walivyokuwa wanamheshimu na pia Barack alivutiwa sana na Michelle

Michelle anasema alimkatalia outing kwa mwezi mzima hata hivyo ilifika siku akamkubalia kwenda pamoja dinner na kwenye movie na hilo kwake lilikuwa kama vile kufanya jambo la kwanza katika wakati sahihi.

Je walioana Lini?
Ndoa yao ilifungwa katika kanisa la Trinity United Church of Christ Chicago, Illinois tarehe 18 Oktoba 1992 na mchungaji Jeremiah A. Wright Jr.
(Source: Dreams From My Father, page 401)

Picha chini ni Siku ya harusi mwaka 1992

Je wana watoto wangapi?
Barack na Michelle wamebarikiwa mabinti wawili
Malia Ann Obama aliyezaliwa mwaka 1999
Natasha Obama ambaye alizaliwa 2001

Je, mji wao (wanaishi wapi)?
Barack na Michelle wanaishi kusini mwa jiji la Chicago kwenye nyumba yao waliyoinunua mwaka 2005 (US$ 1.6 million) ambayo wanakiri ina kiwanja kikubwa kwa ajili ya watoto wao kucheza.
Pia Barack hujitahidi sana kuwepo nyumbani kila weekend kuanzia Ijumaa hadi jumapili kwa ajili ya familia.
Pia hawakuona sababu ya kuhamia Washington DC kwani kuwa Chicago kunawafanya kujisikia stable.
(Source: Chicago Tribune, 12/24/2005)

Picha chini ni Barack na Michelle Obama wakiwa na watoto wao Malia na Natasha
Je, wao ni dini gani?
Barack na Michelle walikuwa wakristo washirika wa kanisa la Trinity United Church of Christ kwa Muda miaka 20 na tarehe 30/05/2008 walijitoa kuwa washirika wa hilo kanisa.
Wakati wa Christmas, Barack na Michelle hutembelea Hawaii kwa bibi yao na dada yake Obama ambao bado wanaishi huko.

Je wanafanya kazi gani za kuajiriwa?
Mwaka 2004 Barack alichaguliwa kuwa US Seneta wa Illinois (Community organizer, civil rights lawyer), Pia amekuwa mwakilishi wa bodi mbalimbali huko Chicago, Illinois.
Michele amekuwa akifanya kazi ya umakamu wa rais wa Community and External Affairs at the University of Chicago Hospitals. Mwaka 2007 alitangaza kuacha hiyo kazi.
(Source: MSNBC.com)

Je kuna vitabu wameandika?
Barack Obama ameandika vitabu viwili:
Dreams From My Father: A Story of Race and Inheritance
The Audacity of Hope: Reclaiming the American Dream


Picha chini ni Nyumba ya Seneta Barack Obama na mkewe Michelle huko Chicago, Illinois
Nukuu ya Barack Obama kuhusu uzoefu wa kuwa na familia nyumbani;
"It is important that when I'm home to make sure that I'm present and I still forget stuff. As Michelle likes to say, 'You are a good man, but you are still a man.' I leave my socks around. I'll hang my pants on the door.
I leave newspapers laying around.
But she lets me know when I'm not acting right.
After 14 years, she's trained me reasonably well.
("Source: Lynn Norment, Ebony, "The Hottest Couple in America", February 2007, pages 52-54.)

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ina pendeza kuona mabadiliko maana kuna watu wanaamini watu wausi hatuwezi kitu. Kweli ndoto imetimia na leo mtu mweusi anakuwa rais. Unajua leo ni miaka 45 imepita tangu Martine Luther....."I have a dream" Kila la kheri Obama mungu awe nawe.

Anonymous said...

Heri ya wale walio na upendo katika ndoa zao maana mungu yu pamoja nao; wasimuache mungu aende zake, Wakae nae, Watembee nae, Wale nae chakula, Walale nawe,Waamke nae,Waombe naye,na sifa zote wampatie maana ni haki yake kupewa sifa.
MSAFIRI

Pendo said...

Thanx mbilinyi, umetuambia Barack Obama alikuwa mkiristo akiabudu dhehebu la Trinity, kwani kwa sasa ni mwislamu au bado ni mkristo ila amehama dhehebu tu??

Lazarus Mbilinyi said...

Kwa sasa bado ni mkristo na sijajua anasali kanisa lipi baada ya kutokea mgongano na hili kanisa lake la kwanza, Obama hajawahi kuwa muislamu na anabaki mkristo naamini nitafuatailia ni wapi sasa anapata chakula chake cha kiroho yeye na familia yake.

Ubarikiwe na Bwana