"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, August 28, 2008

Hakuna kitu "Painless Love"

Ukweli Mapenzi ni Matamu na ni Machungu! Je, umewahi kumpenda mtu kuliko maisha yako mwenyewe na ukampa kila anachohitaji lakini ukaishia kujuta kwa sababu amekusaliti na kukuumiza?
Sisi sote kwa kuwa tuna hisia tumeshapitia (au tunapitia) katika kuguswa na machungu ya aina hii.
Maisha ni kama fumbo huwezi kujua nani utakutana naye na itakuwaje, kuna watu tunakutana nao na kuachana nao baada ya siku moja, au wiki moja au mwezi mmoja au mwaka mmoja au miaka kadhaa, lakini wapo ambao tukikutana nao hugusa mioyo yetu na kujiona maisha bila wao hayana maana ndipo tunapotoa mioyo yetu na roho zetu kwao hata hivyo huishia majanga makubwa na ukichaa wa ajabu na kuumizwa kusikotamkika.

Kuna swali kubwa ambalo huulizwa na watu wengi kwamba inakuwaje watu wawili mwanaume na mwanamke ambao walikuwa wanapendana pia wakapata watoto, wakajenga maisha pamoja na kuishi pamoja lakini wakaishia katika zogo kubwa la aibu na kutukanana, kuumizana na kuaibishana hadi makamani kwa uadui mkubwa?
Hakuna mtu anayeingia kwenye Ndoa akitegemea ndoa kuishia njiani.
Pia hakuna mtu anayeweza kuutoa moyo wake na roho yake ili aishie mikononi mwa mtu atakayemuuumiza na kumtesa kihisia, kiakili au kimwili.
Hata hivyo hasira tunaziona, machungu tunayaona, kudanganyana tunakokuona na wakati mwingine kuuana tunakuona hutokea kwa sababu ya upendo.

Upendo ni kitu kinachofanya maisha kuwa na maana duniani.
Mapenzi ni kiini cha maana ya maisha ya dunia, upendo huweza kuhamisha milima, upendo huweza kudondosha kuta nene na ndefu kwa kuziyeyusha kama barafu.

Hata hivyo ukweli ni kwamba Love is never painless.
Hili halipingiki kwani kila unavyopenda zaidi yule mtu akikuacha basi kuumia kupo.
Wapo watu wamepitia katika kuumizwa na wapenzi wao wa mwanzo na wakipata mpenzi mpya hutoa masharti kwamba tupendane ila don’t hurt my heart.

Hicho ni kitu kisichowezekana kwani huwezi kupata upendo mkubwa ambao siku ukiachwa huwezi kuumia.
Unavyozidi kupendwa na kupenda mambo yakigeuka kuumia kupo hakukwepeki maana;
The higher you love the higher the pains

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mimi naamini kuna penzi la kwli na pia kuna pezi lile ambalo ni basi tu nampenda. Kama ulivyosema inaweza kipita muda mrefu lakini ukikutana na yule mtu penzi lenu mlilokuwa nalo linachanua tena, hata kama mlikuwa mnasoma shule ya msingi, secondary nk. Naamini pia kupenda ni nature. Kwani huwezi kulilazimisha penzi. Huwa mara nyingi nafikiri kwa yale makabila ambayo wazazi huwachagulia mabinti zao mume ambaye ataishi naye miaka yote hata kama hampendi. Bado sijaelewi vipi mtu unaweza kuishi na mtu usiyempenda na kuzaa naye watoto. Ila kwa kweli ile ya kukutana na mpenzi wako ambaye mmeachana muda mrefu halafu hamuwezi tena kufanya lolote huwa inauma sana. Amini usiamini. Trust me!!!

Anonymous said...

Kaka Upo sahihi kabisa ila kwa upande wangu nimeshuhudia ndoa nyingi zikivunjika baada wa mwanaume kuwa kafilisika au hana kitu hapo ndo migogoro huanza hasa kwa wale wanaoingia kwenye ndoa au Penzi kwa sababu mume au mke ana pesa. Msafiri

Yasinta Ngonyani said...

kama unaingiwa na penzi kwa mwanamume/mwanamke mwenye pesa halafu pesa zinapokwisha na wewe unaondoka. Basi hilo lilikuwa si penzi la kweliau sio penzi kabisa

Lazarus Mbilinyi said...

Ni kweli wapo watu huingia kumpenda mtu kwa sababu ya kile alichonacho sasa siku kikiisha na mapenzi yanaisha. Huo si upendo wa kweli bali kupotezeana muda.
Upendo wa kweli haujengwi katika vitu.