"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, August 12, 2008

Harufu Mbaya Mdomoni (Halitosis)

Kuwa na harufu mbaya mdomoni ni kitendo kinachoweza kuathiri maisha ya mtu kimahusiano si kwa mpenzi tu bali marafiki na jamii kwa ujumla.
Pia kuwa na harufu mbaya mdomoni hupunguza mtu kuwa lovable kwani hata unapoongea wengi watakwepa kuongea direct na wewe kwa sababu ya harufu mbaya inayotoka mdomoni.

Kile unakula kina affect hewa unayotoa iwe mdomoni au sehemu nyingine. Na baadhi ya vyakula vina matokeo mabaya sana kwa hurufu unayotoa mdomoni.

Harufu mbaya mdomoni si ugonjwa wa kuambukiza haina haja kuogopa ukikutana na mtu mwenye harufu mbaya mdomoni kwamba atakuambukiza.


Pia tatizo kubwa ni kwamba watu wenye harufu mbaya mdomoni hawajijui kwamba wana harufu mbaya.
Asilimia 85 – 90% ya tatizo la harufu mbaya mdomoni asili yake ni kinywa chenyewe. Pia kiwango cha harufu hutofautiana kutokana na muda (mchana, usiku na asubuhi).

Harufu nyingi mbaya mdomoni hutokana na vyakula vyenye asilia ya protein.
Kuna zaidi ya aina 600 ya bacteria wanaoishi kwenye kinywa cha Binadamu (sehemu ya juu ya ulimi, fizi na kuzunguka meno).

NINI HUSABABISHA KUWA NA HARUFU MBAYA MDOMONI

Kutokuwa makini na usafi wa kinywa kama vile kupiga mswaki vizuri kunakoacha mabaki ya chakula ambayo huoza na kusababisha harufu mbaya mdomoni.

(Wengi hupiga mswaki haraka haraka na kuacha mabaki ya chakula)

Maambukizi ya magonjwa kama vile fizi kutoka damu, mfumo wa upumuaji na kisukari.

Kinywa kuwa kikavu kutokana na medications

Kuvuta sigara, kunywa kahawa

JINSI YA KUTAMBUA KWAMBA UNA HARUFU MBAYA MDOMONI

Wanasayansi wamekiri kwamba ni ngumu sana mtu kujijua mwenyewe kama ana harufu mbaya kwa sababu ya mazoea (habituation).

Ni rahisi sana kutambua harufu kutoka kwenye kinywa cha mtu mwingine.

Unaweza kutambua kama una harufu mbaya mdomoni kwa kumuuliza mtu unayemuamini.

Pia unaweza kujua harufu mbaya kwa kulamba nyuma ya kiganja na kunusa, wengine hupumua mbele ya kioo na kunusa.

Pia unaweza kutumia kijiti cha kuchokonolea meno na kukinusa.

Kisayansi unaweza kutumia vifaa kama Halimeter, Gas Chromatography na BANA Test.

JINSI YA KUJILINDA NA HARUFU MBAYA MDOMONI (TIBA)

Kula vyakula vyenye afya na pia kula vyakula ambavyo wakati unakula vinaweza kusafisha kinywa vizuri.

Kusafisha meno mara mbili kwa siku asubuhi na baada ya mlo wa usiku, unashauriwa kutumia tongue cleaner kusafisha ulimi.

Tumia chewing gum ambazo husaidia kuongeza kiasi cha mate kwenye kimywa kilichokauka. Baadhi ya gums zina viungo vinavyoondoa harufu mbaya mdomoni na zingine husafisha kinywa na bacteria wanaosababisha harufu mbaya.

Tumia dawa ya kusukutua mdomoni (mouthwash) kabla ya kulala usiku.

Kuwa makini na afya ya kichwa chako kama vile kupiga mswaki vizuri, kuondoa mabaki ya vyakula kwenye meno na kumuona daktari kila unapoona una Matatizo ya meno au kinywa.

Kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku angalau glass mbili za maji.

Mwone daktari wako ukiona una tatizo la harufu mbaya mdomoni.


4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Chukulia kama upo kijijini ambako hawajui hata daktari wa meno ni nini na wengine hawana hata mswaki je hii hali itakuwaje.

Lazarus Mbilinyi said...

Kijijini?
Kwanza chakula wanakula ni cha asili, pia wanajali afya ya meno kuliko mijini kwani wanatumia miswaki ya miti ya asili ambayo ni dawa kuliko hiyo miswaki ya kununua ambayo nyuzi zake ni ngumu hadi kuumiza fizi kitu ambacho ni hatari.
So kuwa kijijini kuna tofauti sana na mijini na meno ya watu wa vijijini ni imara na ni ngumu sana kupata mtu mwenye harufu mdomoni kama mijini, wengi wanaonuka midomo ni watu wa mijini. Bisha?
ninyi mnatumia gum kwa ajili ya kuondoa harufu sisi tunatumia kitunguu hahaha!kidding

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kweli kubadilishana mawazo ni kuzuri sana.Unajua nilisahau kwani nilipokuwa mdogo nilikuwa natumia miswaki hiyo ya asili kama vile mibuni. Halafu kuna mti mwingine ukisugua meno yanakuwa maupe na midomo kama umepaka lipstick eehh bwana we raha sana.(kama nakumbuka vizuri uliitwa mdawa)

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,
Ndo utamu wa kublog tunakumbushana na kupeana elimu hata pale tungesahau.

Sasa ukipata vacation chukua hao wajomba zangu hadi kijijini wafundishe jinsi ya kupiga miswaki kwa kutumia mti wa asili.

Nashukuru sana kwa mchango wako.

Upendo daima!