"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, August 8, 2008

Kuridhika

"The best and most beautiful things in this world cannot be seen or even heard, but must be felt with the heart."

Kama wewe umeoa au kuolewa labda nikuulize hili swali.

Je, huwa inatokea unapoamka asubuhi kujisikia hatia na kutokurishwa sawa na unavyotegemea, hata kama usiku mlikuwa na tendo la ndoa la kufurahisha?
Yaani unajikuta bado kuna kitu kikubwa sana unakikosa kutoka kwa mwenzako zaidi ya tendo la ndoa kwenye mahusiano yenu?

Ukweli ni kwamba Binadamu katika maisha ya mahusiano hukamilishwa katika maeneo muhimu matano ambayo yote kwa pamoja yakikamilishwa basi kunakuwa na faragha (intimacy) ya kweli.
Mambo hayo ni pamoja na kuridhishwa:
Kimwili (physical),
Kihisia (feelings and emotions),
Kiroho,
Kiakili (mental) na
Kijamii.

Mara nyingi sana wengi hutimiziana hitaji la faragha kimwili (sex) tu kitu ambacho ni rahisi, hata hivyo baada ya kutimiziana kimwili wanajikuta ndani kabisa bado kuna hitaji halijatimizwa na hawajaridhika au kuridhishwa vilivyo na mwenzake.
Na wapo wajinga zaidi ambao baada ya kuona haridhiki ndiyo hukata kona kwenda kutafuta mwanamke au mwanaume mwingine akidhani huku atapata sex itakayomfanya aridhike zaidi hata hivyo matokeo yake anaona ni kitu kilekile.

Kitu cha msingi si sex bali ni intimacy, kuunganishwa kiroho, kimwili, kiakili, kijamii na kihisia.

Faragha (intimacy) ni kule kwa wawili kuwa karibu, pamoja, ku-share maisha pamoja katika yote, ni kule kujisikia karibu kabisa katika kutegemeana, kuhusiana, kuaminiana, Kusaidiana wakati wa shida na raha, kusameheana, kupendana, kuchukuliana, kuhurumiana na kutumikiana, kuwa pamoja kwa kila eneo la maisha hadi kuhusisha milango matano ya fahamu.

Kucheka pamoja, kucheza pamoja, kutembea pamoja, kushikana, kubusiana, kukumbatiana, kulala pamoja, kuoga pamoja, kusoma vitabu pamoja nk, si sex tu.
Je, kwako faragha ni kimwili tu au hata kiroho, kiakili, kihisia au kijamii?
2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kaka MBilinyi ama kweli ni mafundisho mazuri ambayo labda wengi waliolewa/oa wanasahau ningependa kama wote wangekuwa na uwezo wa kusoma blog yako.Kwani ina mafundisho mazuri

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,
Asante sana kwa comments zako, binafsi najifunza na lengo ni kutaka maisha yangu na yule nampenda yawe ya kuridhishana idara zote katika maisha yetu si unajua ndoa za siku hizi usipofanya efforts unaweza kuona inakumbwa na Tsunami.
Ubarikiwe