"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, August 20, 2008

Imani Potofu na Kuwa "Single"

Wakati mwingine kwa akina dada kuwa 'Single" hujitakia wenyewe, mtu unachagua mume hadi inakuwa "too much" mara unasema hajasoma, mara, hana kazi, mfupi mno, mwembamba mno, mara kabila lake silipendi, mara mweusi mno, mara anatoka ukoo maskini, mpaka unajikuta wenzako wote wameolewa na wana watoto wewe bado unachagua tu.


Uwongo: Kuwa single ni kuwa mpweke na mbinafsi na mtu wa Matatizo.
Ukweli: Mungu yupo na wewe, unaweza kuwa kwenye ndoa na pia ukawa kwenye upweke uliokithiri. Kumbuka Mungu yupo pamoja na wewe na wewe ni mtoto wa Mungu
(Warumi 8: 10 – 13, 15 – 16)

Uwongo: Mungu hana mpango na maisha yangu kwa sababu nipo Single:
Ukweli: Mungu ana mpango na maisha yako. Pia anataka kukubariki kwa vitu vizuri pale tu ukisimama katika kumtegemea yeye na kuwa mvumilivu.
(Yeremia 29:11 – 14, Zaburi 103:2 – 5, Zaburi 5:12)

Uwongo: Ukiwa single ni ngumu sana kushinda vishawishi na majaribu hasa linapokuja suala la sex:
Ukweli: Kwa Mungu hakuna lisilowezekana. Kwa msaada wa Mungu unaweza kushinda kila aina ya vishawishi na majaribu.
(Warumi 8:11, 1wakorintho 10:13)

Uwongo: Ukiwa single upo huru ku-enjoy sex na kila mtu.
Ukweli: Sababu kubwa inayokuwezesha kufanya sex ni nguvu uliyonayo ya kutaka kufanya dhambi ndani yako.
Mungu alikuumba kwa namna ya kuweza kuenjoy sex pale ukiwa katika ndoa zaidi ya hapo bado ya sex hujisikia guilt.

Sex hufanywa kwa watu wawili waliounganishwa kimwili, kiroho na kihisia na kwa kuwa kiroho hamjaunganishwa sex kinakuwa kitendo cha hatia kwani sex ni zawadi kwa wawili waliokubaliana kuishi katika ndoa.

Uwongo: Ukiwa single, Unakuwa huna maana kwa sababu sexually hupo active.
Ukweli: Mungu anakuthamani sana, Sex nje ya ndoa ni dhambi, hata kama watu wengi wanakucheka na kukudharau bado Mungu anakuona mtu wa maana na atakubariki kwa baraka zake. Pia kuishi mbali na sex kunakupa kibali zaidi kuwa jasiri kuomba haki zako kwa Mungu.
(Zaburi 139:1113 – 18)

Uwongo: Nipo single kwa sababu Mungu ananiathibu kwa dhambi zangu:
Ukweli: Kwa kuwa Kristo alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, Mungu hawezi kuchukia kwa kuwa tumetenda dhambi, mara nyingi tunavuna vile tunakuwa tumepanda na Mungu hahusiki.
Inaweza kuwa Mungu bado anashungulika na maisha yetu na bado wakati hujafika kuolewa na kuoa na ukifika Mungu atafanya. Ni muhimu kuwa wavumilivu kusubiri wakati wa Bwana ufike kwetu kuolewa na kuoa.

Uwongo: Siku za sikukuu kama Christmas huwa za upweke na kuwa mkorofi.
Ukweli: Fuatilia ndoa ngapi hupalaghanyika siku za sikukuu kama Christmas hapo unajua ukiwa single si ticket ya kuwa na upweke pia kuwa mkorofi.

Uwongo: Kuwa single ni kinyume na Biblia na si mpango wa Mungu.
Ukweli: Si watu wote wameandikiwa ndoa, Mbona Biblia ipo wazi kabisan na imeeleza wazi kabisa watu ambao waliishi wakiwa single maisha yao yote.
Mfano, Yesu, Mtume Paulo, Yeremia, Eliya, Elisha na Daniel, Sila, Luka, Timotheo, Appollo, Lydia na Phoebe wote walikwa single.

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

pchani hapo wamependeza kweli na pia inaonekana wanapendana sana. Hongera zao

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,

Unawajua wenyewe? ukipatia nakupa zawadi ya viazi (gunia)

Haya kazi kwako!

Yasinta Ngonyani said...

Mmmh viazi gunia moja swa hivyo ni vyangu jibu ni kaka Lazarus na wifi (bahati mbaya jina silijui) je nimepata au

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,
Yaani umepatia 100% huyo wifi yako anaitwa Gloria.
Picha ilipigwa mwezi Desemba 2001

Badala ya kukupa gunia la viazi kama zawadi sasa utapewa shamba zima si unajua Njombe ardhi si tatizo bali tatizo ni mindset jinsi ya kutumia hiyo aridhi ili kujipatia utajiri.

kwa hiyo siku ukipita kwenda Nyasa tuwasiliane ili nikakukabithi shamba lako la viazi maana najua nikikupa viazi vitaisha ila nikikupa shamba naamini hata uncles wangu watakuja kulilima wewe ukiwa mzee.
Asante sana jirani.

Yasinta Ngonyani said...

itabidi unipe na trekta la sivyo itakuwa kasheshe. Haya basi msalimie wifi (Gloria)

Lazarus Mbilinyi said...

Tractor usijali hilo umepata.
Nani kama dada!

Upendo daima