"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, August 15, 2008

Je, Huwa unalala vipi

Baadhi ya wanandoa hulala na watoto wao kitanda kimoja, wana sababu zao, ingawa mara nyingi watoto nao huwa na kitanda chao na wanandoa nao huwa na kitanda chao na chumba chao.
Je, unaamini kwamba jinsi wanandoa wanavyolala huonesha afya ya ndoa yao?
Chukulia wanandoa wanalala bila watoto katika picha zifuatazo.
Swali la kujiuliza je, wewe huwa unalala vipi na mume wako au mpenzi wako na je, jinsi mnavyolala huelezea mood ya jinsi unavyojisikia huo usiku?
( 1) The Spoon Style
Huu mara nyingi ni mlalo wa miaka 5 ya kwanza ya ndoa, ukiona mwanamke anapenda sana kuangaliana uso kwa uso maana yake ni mtoaji (giver)
Wanandoa wengi hulala kwa kukumbatiana wote pamoja au mmoja kumkumbatia mwenzake.
Ndoa ipo kwenye miaka ya kwanza ya mapenzi motomoto.(2) The Honeymoon Sytle
Hii ni style ambayo mara nyingi hutumika na wanandoa ambao kwanza kabisa wapo honeymoon. Uso kwa uso, intimacy ya hali ya juu yaani kama haamini kwamba sasa wameoana.
Hapa ni fukuto la penzi la kwanza kabisa, ni uzoefu mpya kabisa.
Furaha hutawala muda wote wa kuwa kitandani.
Pia Kulala kwa namna hii huja kujirudia kwa ndoa zilizodumu muda mrefu na kupita katika mambo mengi na kujikuta kwamba "kweli tumetoka mbali na tumepita katika mengi".

(3) Like shingles style
Hii ni style ya kulala inayoonesha kwamba wanandoa wanategemeana, mwanaume anawajibika kumlinda mwanamke na kwamba mwanamke anajisikia salama kuwa na mume wa aina hii. Wanandoa wanaonesha commitment kubwa, na attention kwa mwenzake.
Ndoa ipo katika hali salama na tulivu kila mmoja anaridhika na mwenzake.
(4) Sweetheart cradle style
Hii ni style inayoonesha kupeana upendo na hasa mmoja anapopita katika jaribu, tatizo au shida kama vile mwanamke ambaye ana cancer, mwanaume aliyefukuzwa kazi au kuumwa.
Ni mlalo unaoashiria kwamba mmoja anamtia moyo mwenzake na kwamba tupo pamoja katika lolote linalopita katika maisha.
Ni mlalo wa faraja na kufarijiana na kuonesha upendo.
(5) The Loose tethered Style.
Baada ya miaka 5 ya ndoa, wanandoa wengi hujisikia secured sana kiasi kwamba huwa huru kulala anavyotaka kitandani (siyo lazima kukumbatiana, kugusana au kushikana).
Hapo unaweza kumsogelea au yeye kukusogelea wewe kwa kadri anavyopenda au unavyopenda upo huru.
Pia Ndoa huwa imejikita sana katika majukumu kuliko zile "fall in loves" hivyo baada ya kurudi kitandani kila mtu ni kujimwaga kivyake.

(6) The Leg Hug Style.
Baadhi ya wanandoa huwa hawajisikii kugusana au kukumbatiana au kushikana moja kwa moja wakati wamelala.
Wao huweza kugusana vidole vya miguuni au mguu mzima kwa mwenzake au kuulaza juu.
Wakati mwingine wengi hufanya hivi hasa ikitokea kuna misunderstanding, ni kama unatega je, ata-respond vipi nikiweka mguu au nikimgusa?

(7) The Pursuit style.
Kimsingi style ya kulala hivi inaonesha kuna kamgogoro na mwanaume hana mpango kabisa so mwanamke anajakaribu kumrudi mume kwa kumsogelea na kumkumbatia, lengo ni kumpima kama anaweza kugeuka na kuonesha kamgogoro kameisha.
Pia inaweza kuwa anayegeukia pembeni anakuwa amekutega wewe kuona utaitikia vipi?
je, utamsogelea? au na wewe utaamua kula jiwe na kulala mzungu wa nne kabisa?

(8) Zen Style
Jinsi muda unavyoenda kwenye ndoa baadhi ya wanandoa huanza kulala kivyao kitandani.
Kitanda kinaanza kuwa baridi na akilala kila mtu anageukia kwake.
Kila mtu anachunga privacy yake na kuna wengine hudiriki kwenda kununua vitanda vikubwa zaidi King size au Queen size.
Wakilala wanagusana ila kitu mtu kivyake na privacy yake.
Kila mmoja ameshamzoea mwenzake.


(9) The Cliff hanger style
Hii ni style ambayo kila mmoja hulala pembeni kivyake.
Mara nyingi kunakuwa na tatizo kubwa inaweza kuwa hasira, kukazwa, kukasirishwa, au uchovu.
Ni vizuri kuchunguza kama kuna tatizo lolote.
Hapa ni ishara kwamba kuna mambo mengi hayapo sawa kwa hawa wawili.
Bila kuwa makini kutatua kila tatizo linalojitokeza basi mgogoro mkubwa unaweza kuzuka.(10) The Crab style.
Huu ulalaji kwanza ni dalili kwamba mmoja anamuogopa mwenzake.
Hapa mwanaume anaonesha ni kama vile ameacha kitanda na kulala chini.
Kama kuna mshauri wa ndoa basi hapa anahitaji kwani hii ni dalili kwamba ndoa ipo ICU.
Hii ni dalili kwamba mmoja hana mpango na hiyo ndoa kwani ni sawa na wasafiri wawili wanaosafiri kila mtu na mwelekeo wake.
Kama kuna chumba kingine basi hapa ndo mwanandoa mwingine huenda kulala huko yaani amekata tamaa kwabisa na hana interest na mwenzake.

No comments: