"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, August 13, 2008

Kikwapa

Hawa nao sijui vipi? eti wanafanya utafiti kujua wanawake huvutiwa na harufu ipi na wanaume? inayofanana na wao au isiyofanana na wao?

Kawaida mwili wa Binadamu una harufu nzuri sana ukiwa msafi na ukitunzwa vizuri na naturally Mungu alituumba kila mmoja ana harufu yake nzuri kiasi kwamba hata mpenzi akimnusa anapata msisimko na raha ya ajabu.

Ukiwa safi na harufu sana huweza kukupa ujasiri mbele za watu na jamii kwa ujumla.

Tabia yako ya kutokuwa msafi inakufanya watu wakukwepe kuwa na wewe sidhani kama kuna mtu anapenda kuwa karibu na kitu kinachonuka na kuwa na harufu mbaya.

Hata uvae nguo za gharama namna gani kama una hitilafu hasa ya harufu mbaya iwe mdomoni, kikwapa, mwili mzima au miguu bado utaonekana unakasoro kubwa sana.

Wapo watu hulalamika mara watu hawanipendi au sipati mchumba au mume au mke hanibusu na kunikumbatia au tunapokuwa faragha sipati kitu halisi, tatizo inawezekana una harufu mbaya na hupo makini kwenye masuala la kujiweka safi mwili wako.

NINI HUSABABISHA HARUFU MBAYA YA MWILI?

Jasho kama lilivyo halina harufu na harufu mbaya hutokana na bacteria waliopo kwenye ngozi ambao huishi humo kupata mlo.

Kumbuka mwili wa Binadamu una bacteria kila eneo na ngozi ndicho kiungo nkikubwa kuliko vyote hii ina maana ngozi ina bacteria wengi sana na hawa wasiposafishwa vizuri husababisha harufu mbaya sana.

Kuna aina mbili za sweat glands ambazo huhusika na kitendo cha kutoa jasho yaani cooling system ya mwili.

Ya kwanza ni Eccrines hizi zinazotoa jasho la maji na chumvichumvi zipo karibu mwilini mzima na pili ni Apocrines zenyewe zinapatikana sehemu chache kama kwapani na sehemu zingine zenye nywele nyingi hizi hutoa fat na protein ambayo huvunjwavunjwa na bacteria waliopo na hapa ndipo kwenye kasheshe ya harufu mbaya ya mwili.
Pia kumbuka jasho unalotoa linauhusiano mkubwa sana na kile unakula kupitia kinywa chako.

(hujaona walevi wa pombe wanavyonuka pombe pamoja na mikojo yao)

Kwa ufupi harufu mbaya ya mwili husababishwa na

Genetics,
Baadhi ya medications,
Mabadiliko ya homoni mwilini na
Uchafu, mtu kutokuwa msafi mwili na nguo

NINI KIFANYIKE KUONDOA HARUFU MBAYA YA MWILI

Jambo la msingi ili kuondoa harufu mbaya ya ngozi ni kuwa msafi kila siku.

Safisha mwili mzima hasa kwapa kwa sabuni wakati mwingine zile zinazoua bacteria.

Tumia perfume (deodorant or antiperspirant).

Pia kumbuka kutumia perfume bila kuoga ni kazi bure unajimaliza mwenyewe

(unatengeneza mkorogo wa harufu)

Fua nguo unazovaa hata baada ya kuvaa mara moja siyo mtu unavaa shati wiki zima kwa nini watu wasikukimbie au chupi wiki nzima haijafuliwa, unajijali kweli?

Achana na vyakula na vinywaji vinavyosababisha harufu mbaya, kama vile garlic na beer au pombe za kienyeji kama ulanzi, ugimbi, kimbumu, mbege nk

Oga mara kwa mara, wapo anaoga kwa wiki mara mbili na joto la Dar es Salaam zitatuua wenzako na usafiri wa daladala huu tutapona kweli hizi pua zetu?

Nyoa nywele zilizopo kwapani, kwani bacteria hujificha kirahisi (kichaka cha bacteria kujificha) husababisha harufu mbaya sana.

NB: Wazee vijijini walikuwa wanafundisha kwamba kama una kikwapa au harufu mbaya ya mwili unaweza kuondoa harufu kwa kuoga kutumia maji ya ugali yaani sufuria lililopikiwa ugali, unalilowekwa kwa muda usiopungua saa 12 kisha yale maji yake unayaoga.


Hata hivyo Utafiti unaonesha ukiweka Corn starch (aina ya wanga wa mahindi) kwenye kwapa basi kwapa habaki kavu na kuzuia harufu mbaya

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Aise tena jana jioni nilikuwa naangalia TV wanawake ambao wanatoa jasho kila wakati. Mpaka mmoja alisema ametumia kila mbinu ili asitoe josho imeshindikana kwa hiyo sasa tumaini lake la mwisho ni kupasuliwa kwapa. Lo kaka MBilinyi umenifurahisha sana eti watu waache kunywa ulanzi, ugimbi na mbege na nk. Lakini sasa nina swali mmoja kama mtu umeoga na ni saa hiyo hiyo umebadili nguo na kuvaa nguo safi kabisa na mara hiyohiyo unaanza kunuka je hii inasababisha na nini?

Lazarus Mbilinyi said...

Hapo inaonesha geneticaly wewe una kikwapa au aina ya chakula unakula inabisi ubadilishe.
Tumiea corn starch (kama upo majuu) au oga maji ya ugali kama upo kijijini.
Tumia hizo perfume kabla hujafika mbali.
Au mwone dakatari kwa ushauri zaidi