"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, August 14, 2008

Kunuka Miguu

Tatizo la kunuka miguu husababishwa na pale jasho linaposhindwa ku- evaporate na bacteria kuanza kupata mlo humo kwenye jasho la miguuni ambalo huwa katika mfumo wa organic acids na hii hutoa harufu kali sana (pungent smell).
Mara nyingi huwapata wale ambao wana miili yenye kutoa jasho jingi.

Watu wa aina hii wanapovaa viatu vinavyofunika sehemu kubwa ya miguu huku wamevaa soksi, halafu wakakaa navyo kwa muda mrefu, basi wakivua ni balaa.
Tatizo hili ni sugu sana kwetu sisi wanaume, utakuta mwanaume amekutembelea ile kutoa viatu akifika nyumbani kwako au chumbani kwako tayari hapakaliki.

JINSI YA KUONDOKA NA TATIZO LA KUNUKA MIGUU
Safisha nyayo za miguu, katikati ya vidole kwa maji kwa kutumia antibacterial soap kila mara.
Tumia soksi safi na tofauti kila siku.
Pia usivae viatu pair moja kila siku.
Uwe makini na aina za viatu na aina ya miguu uliyonayo. Hakikisha unavaa viatu safi.
Vaa ndala (thongs) unapoenda kuoga siyo unaenda kuoga umevaa viatu na ukishaoga unavaa viatu na kuingiza miguu imelowa kwenye viatu.
Pia, kuna deodorant ambazo zinasaidia zaidi kama vile Admire Deodorant Spray ambayo ndani yake ina Butane, Propane na Alcohol ambazo husaidia kukausha jasho na kuondoa harufu mbaya ya miguu na kuwa mtanashati wa uhakika na usiwe usumbufu kwa marafiki na watu wengine.
Pia unaweza kutumia corn starch powder kwenye miguu yako.

Ukiona tatizo ni kubwa Nenda kupata ushauri kwa daktari ujue kwa nini miguu inanuka.


2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mhh kunuka miguu Nachukia sana ninapokaa na mtu anayenuka miguu (Fangasi) Ni kweli ni muhimu sana kuhakikisha baina ya vidole.Binafsi huwe natumia muda mwingi kukausha baina ya vidole mpaka wengine wanachukia nachukua muda mrefu. Raha kwa sisi wanawake unajua sipendi kuvaa soksi navaa wakati wa baridi tu na hata hivyo navaa nikiwa nje tu hakuna hata siku moja nimevaa/navaa soksi nikiwa ndani. Labda niumwe.

Lazarus Mbilinyi said...

Hongera sana dadangu,
Suala la usafi si wanawake tu pia ni kwa wote wanaume na wanawake lazima wote tuwe safi, inachukiza sana kukuta mwanaume au mwanamke ananuka kinywa, mwili na hata miguu hata wanaume akitoa soksi na utakuta wengine ni vijana kabisa hajaoa sasa hapo nani atavutiwa na wewe hali mbaya kiasi hiki, usafi ni tabia si kitu cha gharama.
Pia urembo ni pamoja na kuwa safi mwili wako.
Inapendeza sana kukuta mwanamke au mwanaume anakuwa safi hata kama atatumia muda ila kuwa msafi ni muhimu.
Mtu ananuka kama shimo la takataka, hapo hamjafika chumbani tuache tu ila mimi pia nachukia sana na mambo haya ya uchafu na kunuka.