"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, August 5, 2008

Kusamehe na Kusahau

Watoto husamehe na kusahau haraka, tunahitaji kuwa kama watoto kwenye ndoa zetu ili tuishi kwa kusameheana na kusahau.

Kusaheme ni kuwa huru na kuwa huru ni kitendo cha akili kuwa bila mawazo, Hasira, kukwazwa, kukasirika, kugadhibika, kukasirishwa.
Kusamehe ni jambo la msingi sana hasa katika mahusiano (sex) ili uweze kuridhika na mapenzi halisi yanayotakiwa katika mahusiano.
Jinsi wewe unavyijisikia mara nyingi huathiri jinsi wengine wanavyojisikia kuhusu wewe.
Kama utakuwa na moyo wa kusamehe na kusahau basi utakuwa na mvuto ambao ni mfano wa sumaku inavyovuta chuma.

Kwa upande mwingine kama huna moyo wa kusamehe, basi watu wote wanaokuzunguka watafanya kila njia kukuepuka, wakati mwingine hata mpenzi wako mwenyewe, mke au mume.

Faida za kusamehe ni kama ifuatavyo;
Kunapunguza BP

Kunapunguza stress

Kunapunguza uadui
Kunapunguza mapigo ya moyo
Hupunguza mawazo
Huongeza marafiki
Huimarisha mahusiano
Kuimarisha kiroho chako na maisha
Kunaimarisha maisha kisaikolojia
Kuongeza hamu ya tendo la ndoa (libido)

If we practice eye for an eye and a tooth for a tooth, soon the whole world will be blind and toothless.

Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa Mbinguni atawasamehe nanyi
Mathayo 6:14


No comments: