"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, August 18, 2008

Kuwa "Single"

Bado Mungu ana mpango na maisha yako hata kama umri unaenda na hujaolewa bado.


Katika mahusiano tunapoongelea mtu kuwa SINGLE tunaongelea mtu ambaye hajawahi kuwa na ndoa kabisa au amaewahi kuwa na ndoa then kukawa na talaka au kifo cha mmoja.

Mtu akiwa single bado anaweza kuwa yupo katika kutafuta mwenzi, mke, mume au partner wa kuishi naye baadae kama mke au mume.

Si kweli kwamba watu ambao ni single wote wanahitaji kuoa au kuolewa, wapo ambao hawahitaji tena kuoa au kuolewa na wanaishi kwa kuridhika na hiyo hali.

Data zinaonesha kuwa miaka ya karibuni idadi ya singles inaongezeka sana.

Katika jamii nyingi suala la mtu kuwa single bado halijapewa nafasi kubwa sana ya kuonekana jambo la kawaida na watu ambao ni single wanakuwa na wakati mgumu sana kwani hawapewi nafasi kubwa ya kuonekana ni watu muhimu katika jamii.

Hata ukienda kwa duka la vitabu bado kuna vitabu vichache sana vinazungumzia masuala ya mtu kuwa single, kanisani pia ni mara chache sana yanatolewa mahubiri ambayo yanawajenga watu ambao ni single.
Jamii yetu pia hasa hapa Tanzania, bado mtu ukiwa single na hasa kama hajawahi kuoa au kuolewa hupata maswali mengi kama vile kwa nini hajaolewa au hajaoa.

Kama wewe ni Single, Kumbuka Mungu ana mpango na maisha yako.

Inachukua hatua ya imani kubwa kuamini kwamba Mungu ana mpango kamili na maisha yetu na hasa pale tunapoona muda unaenda na hatuolewi au kuoa na zaidi unapofika mahali unaona hakuna kinachoendelea.

Unawezekana unajiuliza maswali kwamba;

Je, hivi nitakuwa single maisha yangu yote?
Au hivi Mungu amenisahau?
Au hivi nitakuja kuenjoy mapenzi (sex) katika maisha yangu na umri huu?

Je, kama ni single uishi vipi kwa furaha na ushindi?
Je, kama ni single ni mambo gani ya kuzingatia ili uweze kuolewa au kuoa?
Je, kuna faida zipi au hasara zipi za kuwa single?

(Yer 29:11)
Maana nayajua mawazo ninayo wawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

Nakukaribisha ili tuweze kujadili suala hili kwa undani zaidi.

No comments: