"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, August 2, 2008

Maisha nayo!

"Life is Not a Short Race, It is a Marathon of Marathons"Kwa wale wenye kumbukumbu za historia ya riadha Tanzania picha ya juu ni mwanariadha John Steven Akhwari ambaye mwaka 1968 huko Mexico city, Mexico alivunja rekodi ya kuwa mtu wa mwisho kuchelewa kumaliza mbio saa moja baada ya mbio kwisha.

Yeye alimaliza mbio saa moja baada ya mtu wa kwanza kumaliza mbio na wakati anamaliza walikuwa katika taratibu za mwisho kufunga ukimbiaji wa hizo mbio na baadhi ya mashabiki walikuwa wameshaondoka uwanjani.
Akiwa anataabika na kuhakikisha anamaliza mbio huku amejifunga bandeji miguu huku amechoka.
Watu walishangaa na kutaharuki kuona bado kuna mkimbiaji alikuwa bado anakimbia na hakukata tamaa hadi mwisho, kumbe alikuwa ni John kutoka Tanzania alikuwa bado anachakarika kuhakikisha anamaliza hizo mbio za marathon saa moja baada ya mbio kwisha.
uwanja ulilipuka kwa vifijo na nderemo na wakamuwekea utepe ili amalize mbio zake akiwa wa kwanza kutoka mwishoni saa moja baada ya mbio kwisha.

Ndipo mwandishi wa habari Mr. Greenspan alimuhoji kulikoni kuendelea kupigana hadi damu ya mwisho wakati uwezekano wa kushinda ni sifuri ?
John alijibu
"My country did not send me to start the marathon but sent me to finish the marathon"
"Nchi yangu haikunituma kuanza mbio za marathon bali kuhakikisha namaliza"


Huu ni mfano wa maisha tuliyonayo hakuna kukata tamaa, hata kama unakumbana na shida na matatizo, muhimu ni kufunga bandeji na kuendelea na mbio.

John Steven Akhwari akiwa anakimbiza Beijing Olympic Games Touch.
Kwenye relay tarehe 13 April 2008 mjini Dar es Salaam, TanzaniaHapa akiwa Nchini China kwa ajili ya maandalizi ya Olympic 2008.


No comments: