"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, August 9, 2008

Msinifuate Mimi

Mohamed Bello Abubakar (84) mzee anayeishi mji mdogo wa Bida huko Nigeria ametoa tahadhari kwa wanaume wengine hasa wale wa kiislamu kutokuoa wanawake wengi kama yeye kwa sababu anasema bila nguvu ya Allah huwezi kufika popote.
Mohamed Bello Abubakar ameoa wanawake 86 na sasa ana watoto 176 ukiacha wawili waliofariki.
Ingawa waislamu wengi wanakubali kuoa wanawake mwisho 4 yeye anasema Allah amemuwezesha kuoa wanawake hao 86 na wanawake ndo huenda kwake ili waolewe.


Baadhi ya wake zake wana umri mdogo kuliko watoto wake mwenyewe aliozaa na wanawake wengine.

Pia kitu cha kushangaza ni kwamba pamoja na kuwa na familia kubwa bado yeye pamoja na familia hawana kazi maalumu za kufanya na hivyo yeye akiishiwa chakula hutuma timu ya watoto wake mitaani kuomba ngawira na kila mmoja huambiwa lazima apate dola 1.75 kiasi ambacho wakirudi home wanapata jumla ya dola za kimarekani 290.

Pia Bwana Mohamed Bello Abubakar ambaye amewahi kuwa mwalimu wa dini ya kiislamu anakiri kwamba yeye anauwezo wa kuongea na Mtume Mohamed moja kwa moja pia hufanya kazi ya uganga wa kienyeji na pia anakiri kwamba huweza kuona ugonjwa wa mtu moja kwa moja akimuona kwa macho tu, hata hivyo watoto wake wawili walishakufa kwa ugonjwa.

Pia ameleta gumzo kubwa nchini Nigeria kwani wengi wanasema ni kiongozi wa imani potofu tofauti na uislamu wa kweli.

Ganiat Bello Abubakar (moja ya wake zake) anakiri kwamba "Ukiolewa na mwanaume mwenye miaka 84 kama Bello Abubakar unajua kabisa anajua jinsi ya kutunza wanawake".

Kwa habari zaidi bonyeza hapa

http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/7547148.stm

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

ama kweli hapo ni mwisho. kwani wengine mke mmoja tu kasheshe. sasa hapa tusemeje ni penzi kweli au ni kutaka sifa tu na hao wanawake kweli wanampenda au. je anawajua watoto wake na kuwapenda wote hao. kwa sababu ukiwa na mmoja tu kichwa kinataka kupasuka. Je inakuwaaje katika swala la ndoa anaweza kuwahudumia wote 86?

allen said...

Haya mambo yamepitwa na wakati na naamini hii familia ina maisha magumu mno na huyu mzee hata waislamu wenzake wanamsema kwamba anaenda kinyume kabisa na ana amani potofu (cult)
Wanasema watoto wake ni omba omba na hana kazi maalumu. Pia naamini umaskini kitu kibaya sana maana hawa wanawake maskini huona fahari kuolewa na mwanaume kama huyu anapata hela za uganga wa kienyeje na wanajiona hapo wamefika.
Sidhani kama anaweza kuhudumia wake zake wote 86 vizuri nahisi kuna wengine huwa wanapiga kona kwa wanaume wengine, si unajua miaka 84 hata speed ndogo.
Utamu wa ndoa ni mke mmoja na mume mmoja na kuzaa watoto unaoweza kuwalea.

Lazarus Mbilinyi said...

Kwa nini anasema msinifuata mimi?
Naamini kwa sababu anapata shida mno na huo msululu wa familia.

Ni kweli haya mambo yamepitwa na wakati kwa sasa kwani masuala ya uchumi na kijamii yamebadilika sana na pia mambo ya magonjwa.