"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, August 27, 2008

Mwenye Ndevu au Asiye na Ndevu!

Eti kwa aina hii ya ndevu wengine huvutiwa zaidi! Wanaume wamekuwa wakijiuliza je, ni vizuri kunyoa ndevu kipara kabisa au kuziacha zikue na kuwa mzee madevu?.
Je, nitaonekana navutia nikiwa nimenyoa ndevu au sijanyoa ndevu?

Utafiti huko Uingereza unaonesha kwamba wanawake wengi (si wote) huvutiwa sana na wanaume wenye videvu vyenye ndevu kidogo (Stubble) kuliko wale wasio na ndevu kabisa (clean shaved) au wenye vichaka vya ndevu (full beards) kwa ajili ya sex, mapenzi na ndoa.
Njia rahisi ya kuvutia wanawake ni mwanaume kuwa na kidevu chenye ndevundevu na si kuwa kipara au nyingi kama akina Osama.

Kuwa na ndevu (kwa mwonekano wa aina hiyo) hudhihirisha uwezo kinguvu, uimara, ukomavu kijamii na mvuto (best romantic partners)
Kuwa na ndevu ni kiungo cha nguvu kijamii na kimapenzi kwani ni alama ya kuonesha ukomavu kibaolojia.
Wale wasio na ndevu kabisa huonekana hawajakomaa na wale wenye vichaka vya ndevu huwa na sura inayotisha mno au kuonekana wababe na hawavutii sana.

Je, huu utafiti una ukweli wowote? labda wanawake wanaweza kutoa maoni!

Source: British newspaper the Sunday Telegraph,
India times newspaper.
http://timesofindia.indiatimes.com/HealthSci/Women_prefer_men_with_stubble/articleshow/3178159.cms

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hii ni upendeleo wa mtu kuna wanawake wengine wanapenda wanaume wenye ndevu na kuna wanawake wengine wanapenda kinyume. Sawa na kuna wanawake wengine wanapenda wanaume wanene na wengine kinyume, wengine wanapenda wanaume warefu na wengine wafupi. Chukulia mfano wa kuwa na nywele kwapani wengine wanaona ni safi sana na wengine kinyume. Ila kwa nini iwe hivyo kwani kama mtoto, mvulana mdogo ulikuwa huna ndevu na sasa ndio wakati wa kuwa nandevu ila hata mimi sipendi kama wanaume wanakuwa na ndevu kama msitu na pia sio kipara isipikuwa katikati. nadhani nimeeleweka

Lazarus Mbilinyi said...

Umeeleweka!
Ni kweli kila mwanamke ana namna yake ya kitu maalumu kinachomvutia kutokakwa mwanaume. Ingawa upo sahihi pia kwamba kuna asilimia kubwa wengi wanapenda mwanaume mwenye umbo au sura fulani.
Kuna wengine hawapendi kabisa mwanaume akiwa mfupi wakati huohuo wengine akiona mwanaume mfupi anachanganyikiwa kabisa.
Kila mtu na ladha yake.

Anonymous said...

Mimi napenda mwanaume wenye ndevu si ndefu sana wala asiye na ndevu kabisa pia awe na kamustachi kidogo, ila kwanza ni Upendo.