"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, August 6, 2008

Ndoa, Uwongo na Ukweli

Hivi ili ndoa idumu vitu gani ni vya msingi?

Uwongo: Msingi wa maisha ya kudumu ya ndoa ni mapenzi mazuri
Ukweli: Msingi wa maisha ya kudumu ya ndoa ni kujitoa kwa Mungu kwa kila mwanandoa.
Mapenzi mazuri ni matokeo ya kumjua Mungu
(Warumi 7:2 –3)

Uwongo: Ikitokea mmoja ya wanandoa hana furaha hiyo ni dalili kwamba talaka ipo njiani inakuja.
Ukweli: Utafiti unaonesha kwamba wanandoa wengi hujisikia kutokuwa na furaha wakati fulani katika ndoa zao, lakini kiasi cha miaka 5 baadae hujisikia furaha zaidi kuliko mwanzo na ndoa huwa tamu zaidi.

Uwongo: wanawake waliosoma wengi hushindwa kuolewa ukilinganisha na wanawake ambao hawajasoma sana.
Ukweli: Utafiti wa karibuni unaonesha kwamba wanawake waliosoma sasa wana uwezekano mkubwa wa kuolewa ukilinganisha na wale ambao hawajasoma.

Uwongo: Ndoa huwapa faida zaidi wanaume kuliko wanawake.
Ukweli: Wanandoa wote hupata faida sawa katika maeneo yote kama vile tendo la ndoa, ushirika na kuwa pamoja (companionship) Kusaidiana kazi.

Uwongo: Ndoa itakufanya ujisikia kuridhika na maisha.
Ukweli: Utajisikia kuridhika na maisha pale tu utakapokuwa huna ubinafsi na pia ikiwa utamtumikia mwanandoa mwenzako kwa kujitolea.

Uwongo: Katika ndoa kila mmoja anahitaji kujipenda mwenyewe na nafsi yake kwanza ili kumpenda mwenzako.
Ukweli: Unatakiwa kumjali na kumtanguliza mwenzako kwanza ili kuonesha unampenda.
(Yoh: 13:34, Math 16:24)

1 comment:

Fikirikwanza said...

Kweli mwenda kwao hatundzi, hizi kofia mkiwa wangama mnawaachia kina mkangafu na kina shaulembela si kasi lakini hapa si onaona ilivyo kutoa mzee. Nenda madilu wakakushonne ya mianzi nafikiri itakuwa super kuliko hiyo uliyo ivaa.
safi sana nimeipenda hiyo foto ila where is mwindzuhuru?
Ok bye