"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, August 22, 2008

Ni akina Hitler wa Ndoa

Wakati mwingine huwa tunajikuta tumebeba mabox ambayo tunadhani ni yetu lakini mbele ya safari tukifika nyumbani tunashangaa kukuta si yetu ni mali za watu wengine.
Maisha ya mahusiano nayo wakati mwingine ni kama kubebeshana mabox, mwenzako akijua wewe ni mbebaji mzuri basi utachakaa kwa kubeba mabox yake ya hasira zake, ukari wake, au manyanyaso ya kila aina, hadi siku utakapostuka.
Hujakutana na watu ambao katika mahusiano yao mmoja huwajibika kumpendezesha mwenzake kumfanya awe na furaha au ajisikie vizuri huku yeye mwenyewe akiishi kwa hofu na mashaka, hata hivyo huyo anayefanyiwa yote hayo bado hana shukurani na ni kama kumpigia mbuzi gitaa.
Kuna kitu kinaitwa “Narcissism” hili ni neno la kigiriki lenye maana ya mtu kuipenda zaidi nafsi yake kuliko kawaida (extreme self-loving).
Hili Neno linaendana na story ya kijana wa Kigiriki ambaye alivutiwa na taswira yake mwenyewe kwenye bwana kiasi cha kushindwa kuondoka hadi alifia hapo.
Hili tatizo huanzia wakati mtu bado mtoto mdogo hasa baada ya Kukosa upendo na huruma, ukweli ni kwamba yeye mwenye hajipendi na matokeo yake hawezi kujua kupanda mtu yeyyote.
Utafiti unaonesha ni asilimia 75 ya wanaume ni narcissists.
Na Adolph Hitler alikuwa kinara wa hizi tabia ingawa huyu alikuwa hatari hata hivyo tunao akina Hitler wengi sana kwenye mahusiano yetu ya kila siku kama vile ndoa, uchumba nk.
Hawa akina Hitler wanachofanya ni kukubebesha kibox cha wewe Kujiona una hatia, hofu, woga, mashaka, kutojiamini ili wakupelekesha wanavyotaka wao.
Hawa wanaweza kukudhalilisha kimwili, kimapenzi, kihisia na pia
wanaweza kuzira kuongea (silence) na wanachofanya ni kuku-control wewe idara zote za maisha yako unakuwa kama mfungwa fulani kwa kuwa umeingia kwenye anga zao.

Hata unapoishi nao unakuwa unaishi maisha ya mateso na kunyimwa uhuru.
Hii aina ya mahusiano ni hatari tupu na Huhitaji msaada wa ushauri kwa wataalamu wa maswala ya ndoa na mahusiano.
Wengine ni watu wenye status kubwa katika jamii zetu anaweza kuwa manager, lecturer, tajiri, mbunge au waziri na hawa watu huonekana watu wa heshima kubwa sana mbele ya jamii kwani ni wapole, wema, watii, ni marafiki, wastaarabu, wamevaa ngozi ya kondoo huku ndani ni mbwa mwitu na katika maisha yao ya ndani ni hatari (lethal)
Kufanya kosa moja tu ukilifanya wao huona unastahili kupewa adhabu ambazo wao wanaona zinafaa.
Hawa wanaume aua wanawake hufurahia sana kutesa wake zao au waume zao, hawana huruma na hawafai kabisa katika jamii.
Tupendane katika ndoa zetu

No comments: