"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, August 10, 2008

Bon - Fire

Leo nilikumbuka kuchoma viazi hata hivyo nilifanikiwa kupata Marshallows na kuzichoma huku tunapiga story.
Ilikuwa jioni njema yenye kibaridi kama cha Makambaku na Njombe Tanzania.

Utamu wa kiazi ni kuiva vizuri bila kuungua (kiive bila kuungulia), hilo nipo makini hata kungekuwa na mashindano ya kuchoma viazi naamini ningepata medali ya dhahabu.
Unawapigisha story; wakijakushtuka viazi vimeisha.
Ujanja kupata si kuwahi

6 comments:

Fikirikwanza said...

nyie nimewagundua kumbe mnayataka maisha ya kina shaulembela mkiwa ameriaca mkisha fika bongo mnajifanya nyie ni wa mjini. Si mnaona maisha yalivyo bomba ya kwenye vihegele vya kina mwangutwa kule ikelo.
nimezipenda hizi picha nafikiri mtaota maisha yenu yote.

Sharuvembo Hill said...

Maisha mahali popote unaweza kuyaweka kama unavyojisikia kwani raha ni kuyachukulia maisha kama yalivyo.

Yasinta Ngonyani said...

Nimeona wivu sana lakini nimeshangaa nimeona wengine wamevaa kaputula na T-shirt tu kweli baridi kama makambaku na Njombe sikubaliana nawe. Na hivyo viazi ni viazi mviringo(matosani) au viazi vitamu?

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,
Angalia vizuri wote tulivaa masweta, pia kwa kuwa moto ulikuwa mkali ndo maana tulivaa kaptura.
Vilikuwa viazi mviringo (matosani)

karibu sana

Yasinta Ngonyani said...

Oh samahani sikuangalia vizuri. Je? hivyo viazi mviringo vilikuwa vitamu kweli maana sijawahi kuchoma wala kula. Ila viazi vitamu(matata) kweli

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Pole sana,

Viazi mviringo (matosani) vikichomwa vitamu sana acha kabisa. Basi siku Ukija lazima nikuandalie au tutakutana Nyasa, na mimi nitakufungashia kutoka Njombe.

Sikia tu ila vitamu acha kabisa.