"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, August 7, 2008

Office Romance (ii)


Imeandaliwa na Mercy Wanjiru Mutahi (China)

Kwa kweli kwa ofisi za serikali ni too much kwa suala hili la mahusiano sehemu za kazi hadi sasa Wizara ya Afya wameamua kuanzisha mpango wa kufundisha maambukizi ya ukimwi katika sehemu za kazi, lakini hii ni kwa ofisi zilizo chini yake tu.
Unajua tatizo la mahusiano makazini ni ile kuwa age moja na utani uliopitiliza. Utakuta watu wanataniana [sweetie, honey, darling} na sometimes wana act kama kweli na kushikana sehemu sensitive na hii inapelekea kuzama kabisa.

Suala lingine ni kuwa kuna watu wao ngono kwao ni kitu cha kawaida tu. Mbali na utani wa maofisini kingine kinachochangia ni kuwa ofisi nyingi wanaajiriwa wafanyakazi wengi kwenye cadre moja so utakuwa kazi zinakuwa chache sana kwa wafanyakazi na kupelekea kukosa shughuli za kufanya na kubaki kutaniana na kuongelea mambo ya mapenzi wengine hata tongue kiss kabisa.
Kwa mabosi, mabosi wetu wengi tatizo kubwa huwa hawawachagui wafanyakazi wale wanaopaswa kuchaguliwa kwa kufuata pass rate zake za interview na ingewezekana kabisa interview zingekuwa zinafanywa na watu ambao hawako katika ofic husika na wala hawana interest zozote.

Utakuta interview imepita na watu wamechaguliwa, bosi anasema kuwa mimi ndio nimefanya efforts hadi wewe uchaguliwe, then sasa utanipa nini. Yeye mwanaume na wewe ni mwanamke, ukimwambia kuwa mheshimiwa niko tayari mshaharawangu wa kwanza ule wewe atakuambia kuwa hana shida ya hela.
Kwa hiyo unakuta ajira nyingi zimetawaliwa na rushwa ya ngono siku hizi.
Wengine wameshaajiriwa ila tu bosi anakupenda hapo inakuwa shida maana atafanya vitimbi kama umemkatalia matakwa yake kiasi kazi utaiona chungu.

Ni kama pepo linawakumba watu, utafuatiliwa inapelekea kupunjwa mshahara, na mambo mengi yanayokuhusu wewe kutotimiziwa au kukwamishwa kwa sababu tu hujawa tayari kutoa ngono ila ukiwa mwepesi kwa hilo utapata favour zote ila madhara ni kuwa na magonjwa juu.


No comments: