"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, August 21, 2008

Ondoa TV Chumbani

Ingawa Tv hutupasha habari na kutuburudisha bila kuwa makini Tv humaliza muda wetu na kutulemaza akili zetu na kuathiri ndoa zetu.

Utafiti unaonesha kwamba kukiwa na Tv chumbani huathiri kiwango cha sex huathirika.
Na ukiwa huna Tv chumbani kiwango cha kufanya sex huwa mara mbili zaidi.
Bado kuna mawazo tofauti kuhusiana na suala la kuwa na Tv chumbani wapo wanaosema kuna faida zaidi kuliko hasara na wapo wanaosema kuna hasara zaidi kuliko faida.

Zaidi ya kuathiri muda na uwezo wa sex kwa wanandoa TV ikiwa chumbani husababisha yafuatayo:
TV Huwafanya kuwa wakimya au bubu (dumb)
Kukiwa na TV kila mmoja huelekeza kusikiliza TV badala ya mwenzako na matokeo yako mkiwa chumbani mnakuwa bubu.
TV husababisha kuwa wanene na vitambi
Ukiizoea Tv unakuwa addicted na matokeo yake kila wanandoa wakirudi kazi jioni hujifungia chumbani kwa ajili ya kutazama Tv badala ya kufanya kazi au shughuli ambazo zinafanya mwili kuwa active. Pia wengi wanapotazama TV huwa wanatafuna vitu au kunywa kitu hali ambayo hujaza tumbo na kusababisha kunenepeana.
TV huathiri muda wa kulala
Kama kuna show nzuri na ipo muda tofauti na ule umezoea kulala matokeo yake ni kuchelewa kulala na kuathiri usingizi.

TV husababisha wengi kuwa wavutaji zaidi wa sigara.
Hasa kama mwanaume au mwanamke anaruhusiwa kuvuta sigara ndani ya nyumba au hata nje.
Tv husabisha kukosa muda wa Maombi na kusoma Neno.
Muda wa maombi na neno huchukuliwa na shows za kwenye TV.
TV Hupunguza uwezo wa kuwa wabunifu (creativity)
Akili huwa tegemezi kwa sababu ya kutazama TV

Je, watu wengine wanasemaje?
Wao wanakiri kwamba kitu muhimu chumbani kwa wanandoa ni sex na kulala
Muda mwingi mnaotumia kuangalia hizo shows unaweza kuwafanya kuwa mmechoka na bored na matokeo yake mnaweza kushindwa kujipanga vizuri kwa sex.
Wao wanasema kwamba huwezi kuweka vifaa na vitu vya kazi kwenye mazingira ya chumbani huko ni kuchanganya mambo kwani chumbani ni mahali pa love zone.
Ni muhimu sana kuepuka kutazama Tv, au kulia chakula chumbani pamoja na kudiscuss issue ambazo ni emotional kwani huweza kuathiri sana usingizi na sex.
Muda wa kulala si kulala tu bali ni ku-renew na kuimarisha mahusiano ya wanandoa, ni wakati wa kujifunza na kushare nini kimetokea siku nzima kwa wanandoa na si kukaa na kusikiliza, kutazama na kuongeleshwa na Tv.
Chumbani ni mahali ambapo wanandoa wanakuwa na quality time pamoja kupanga mipango, kufanya maamuzi, kuweka deals au kukabiliana na disagreements zozote, ku-solve Matatizo, kupeana habari muhimu.
Muda mwingi wa maisha yetu tunalala hivyo basi ni muhimu wanandoa kuufaidi vizuri muda wao ambao ni muhimu kuliko kuisikiliza TV na kuiangalia.

Source: Italian sexologist Serenella Salomoni.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

swali je ni vizuri kuwa na redio chumbani?

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,
Radio haina shida sana hata hivyo ukiona radio unawapotezea muda wa faragha yenu zima kabisa.
Pia kuwa na Tv chumbani si vibaya sana ila inakuwa vibaya pale inapowaongoza ninyi badala ya ninyi kuitawala yenyewe. Yaani mnakuwa addicted na kuangalia program za TV hadi mnaharibu muda wa kuwa pamoja na kufurahia sex chumbani kwenu kama wanandoa, au tuseme TV inachukua nafasi ya muda wenu na mambo yenu mnakuwa kama vile ninyi ndo sasa mmeolewa na TV.

Upendo daima