"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, August 25, 2008

Patashika kwenye Harusi

Nchini Kenya katika jiji la Nairobi katika kanisa linalojulikana na kwa jina la "Deliverance Church" hivi karibuni kulizuka patashika ya nguo kuchanika wakati wa ibada ya ndoa baada ya mwanamke mwenye mtoto wa Bwana harusi kufika kanisani kuzuia ndoa isifungwe kwa kuwa yeye mwanamke ndiye mke halisi wa Bwana harusi.
Pichani chini Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Esther Wangali akiwasili nje ya uwanja wa kanisa na mtoto wake kwenda kuzuia ndoa isifungwe hata hivyo alipoanza vurugu tayari ndoa ilikuwa imeshafungwa wakaishia kuvuruga sherehe tu.

Picha chini.
Kila mmoja akifanya analoweza kuhakikisha anatoka salama kwenye hiyo patashika kwani ex - lover wa Bwana harusi alikuja na kikosi cha kukodi kuhakikisha kila kitu kinaenda ndivyo sivyo.

Picha chini
Bi. Esther Wangari akihojiwa na watu wakati anawafika kanisani


Kwa wengine kilikowa kilio na majonzi
Picha ya chini
Ilibidi Polisi waitwe ili kuja kuzuia madhara zaidi kwani vurugu zilisababisha kamera za wanahabari kuharibiwa na kikosi kilichokodiwa kuja kuvuruga harusiBi. Esther anadai kwamba yeye alikuwa ni mke halali wa Bwana harusi na kwamba Bwana harusi huyo amekuwa akila jiwe kuhudumia mtoto kama vile mahitaji ya shule na chakula.
Pia Esther aliwaambia watu kwamba alishamtonya mchungaji wa Bwana harusi hapo "Delivarence Church" kwamba mshirika wake (bwana harusi) ana kesi na yeye kwani anamtambua kwamba ni mume wakehalali, hata hivyo pastor aliendelea na taratibu za ndoa bila kumsikiliza.
Source: By Alphonce Shiundu - Sunday Nation


2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

aise hiyo kweli kasheshe hii imewahi kutokea mara nyingi unajua nimekumbuka kuna kaka mmoja alimpa mimba msichana mmoja na wakati huu huu alikuwa na mchumba na wakaahidiana kufunga ndoa. Sasa cha ajabu akampa mimba huyo pia kabla ya kufunga ndoa.Sasa sikiliza kilichozuka hao wanawake wakazaa muda mmoja labda zilipisha siku tu. Yule aliyefunga naye ndoa hakujua kama kuna mtu mwingine pembeni. Siku moja yule mwanamke wa nje akaja nyumbani kwa yule kaka na kufoka kama mbogo na akamweka mtoto nje ya nyumba na kuondoka. Kwa vile yule mke wa ndoa alikuwa na roho ya kibinadamu alimpokea yule mtoto na kumlea kwa hiyo badala ya kuwa na mtoto mmoja akawa na mapacha. Naona hii habari inalingana na hii ya kuvuruga harusi. Lakini kwani yeye bi Esther na bwana harusi walikuwa wamefunga ndoa au

Anonymous said...

MMMMMMMMM Hiii sijapendezwa nayo Akha hata aibu huyo bwana hana, Lakini Je mlalamikaji alikuwa na cheti cha ndoa au ndo aliambiwa we tuzaeee tu kisha nitakuoa????? Msafiri.