"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, August 7, 2008

Risasi za kutosha, Fanya haya!

Mwanaume hutakiwi kucheza mbali na hizi mbogamboga kama unahitaji kuwa na risasi za kutosha kwa ajili ya bunduki yako.

Je, nini kifanyike kuwa na sperms za kutosha?

Fanya mazoezi mara kwa mara na pia mazoezi ya kukaza misuli ya PC.

Kula vyakula vyenye viini muhimu na kuachana vyakula vyenye asilimia kubwa ya fat bali vyenye protein, mboga za majani, nafaka nzima, punguza kunywa caffeine.

Epuka sehemu zenye joto (hasa kwenye testicles zako),

usivae nguo zinazobana sana,

Tendo la ndoa kwa kupishana siku tatu kwani kufanya sex kwa mfululizo hupunguza uwingi wa sperms.

Kuachana na tabia za kuvuta sigara au kunywa pombe, sigara na pombe husababisha maini kutofanya kazi vizuri.

epuka kuoga maji ya joto sana hasa sauna.

Punguza unene (nyama zembe) husababisha homoni kushindwa ku-balance utendaji.

Hakikisha mwili wako na akili zako zina afya njema kwa kuhakikisha upo mbali na stress.

Kama unaweza Hakikisha unaufanyia massage mwili wako kwa kutumia herbal oil, hii husaidia mzunguko wa damu kuwa safi hadi kwenda sehemu kurahisisha utendaji au uzalishaji wa mbegu.

Fanya mapenzi au tendo la ndoa asubuhi sana au mchana kwani kiwango cha sperm huwa juu sana.

Hivyo basi, kama unatafuta mtoto ni vizuri tendo la ndoa kufanyika asubuhi sana au mchana wakati sperms zinakuwa za kiwango cha kutosha.

Je, kuna uhusiano kati ya chakula tunakula na sperms kuwa nyingi?

Ndiyo, chakula ni muhimu sana kwa ajili ya utendaji wa mwili wako na kuzalishwa kwa sperms za kutosha.

Kwenye chakula kuna madini ya Zinc ambayo husaidia sana kupunguza mwili usizeeke mapema na pia ina stabilize DNA katika kuzalisha Sperms.

Ukosefu wa madini ya zinc huweza kusababisha infertility kwa wanaume.

Je, ni chakula gani chenye Zinc kwa wingi?

Chakula chenye zinc kwa kiasi kikubwa ni oysters ambao wanapatikana baharini.

Pia vyanzo vingine vya madini ya zinc ni protein ya wanyama kama vile kitimoto, nyama ya ng’ombe, na kuku.

Pia maharage, karanga, mbegu za maboga na alizeti huwa na kiwango kizuri sana cha zinc na ni muhimu wanaume kuchangamkia kwani inakupa uhakika wa kuzalisha sperms zenye viwango na zinazoweza kufanya trip iliyokamilika na kusafiri salama hadi mwisho wa safari.

No comments: