"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, August 2, 2008

Tunayo Sifa!

Utafiti uliofanywa na Wilford Hall United States Air Force Medical Center and San Antonio Military Medical Center huko Marekani unaeleza kwamba watu watu weusi (African descent) miili yetu ina kisifa (genetic trait) ambayo inatufanya kuwa rahisi kuambukizwa na virus vya HIV tofauti na watu weupe.
Kisifa hicho ambacho pia husaidia pia kupambana dhidi ya maambukizi Malaria kinachochea maambukizi ya HIV kwa asilimia 11 zaidi katika bara la Africa ambalo gonjwa la UKIMWI limekuwa ni janga kubwa na watu wanazidi kuteketea.

Ukijaribu kuchunguza kwa makini hata nchini marekani watu weusi au jamii ya watu weusi ndiyo imeathirika zaidi ya UKIMWI na bara la Africa hasa kusini mwa jangwa la Sahara hali ni mbaya sana.

Je, huu utafiti una ukweli wowote?

Kwa habari zaidi soma link hii hapa chini
http://www.washingtonpost.com/wp-dyn/content/article/2008/07/16/AR2008071601539.html

No comments: