"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, August 19, 2008

Ukiwa 'Single" Jiamini

Ukijiamini una kuwa huru kimawazo na kutokuwa tegemezi kusubiri wengine wakupe furaha. (Picha kwa hisani ya dada Y. Mtei Arusha - Tanzania)
Ukiwa single unahitaji kujiamini kwani wewe mwenyewe ni chanzo cha furaha, upendo amani na maamuzi mbali mbali ya kila siku katika maisha yako.
Lakini linapokuja suala la sex wapo wanaothani kwamba kuwa na mtu ambaye una share naye mapenzi au sex unaweza kupata furaha ya kweli na na wewe kujiona mtu unayejua kutoa upendo kwa wengine.
Hii hupelekea kuwa tegemezi kimwili, hasa linapokuja suala la hisia zako na matokeo yake unakuwa target rahisi kwa partner asiye sahihi (partner from hell) anayeweza kukuumiza moyo wako.

Kwa hiyo ufahamu na elimu ya kujiamini ni vitu muhimu sana vinavyoweza kukusaidia usiweze kupata maafa yanayoweza kukuangamiza na kuuumiza moyo wako kuuvunja vipande vipande hasa wakati huu ambapo unatafuta mwenzi wa maisha.

Kujiamini hujengwa kwa msingi wa mafanikio ya kitu kimoja kwanza.
Mafanikio huzaa mafanikio na kushindwa kuzaa kushindwa.
Tunapojifunza kitu kipya kama vile kuendesha gari mara ya kwanza huwa tunakuwa na hofu ya kushindwa na tukishaweza tunaendelea kujiamini na kuweza zaidi na zaidi..
Mafanikio madogo madogo ni ngazi za kupanda kupelekea mafanikio makubwa.
Kwa hiyo Kukosa kujiamini (self confidence) kunaweza kukufanya kuwa dhaifu katika hisia zako na maisha yako kwa ujumla.
Unahitaji kufahamu kwamba hata kama huna mwanaume au mwanamke bado maisha yanaweza kuwa ya furaha na yenye kukupa amani.

Kutojiamini kunaweza kukufanya upoteze nafasi (opportunities) nyingi katika maisha yako na pia Kukosa uwezo ulionao kujiendeleza na kufanya mambo makubwa katika maisha.

When you have confidence, you can have a lot of fun.
And when you have fun, you can do amazing things.
If you have no confidence in self, you are twice defeated in the race of life.
With confidence, you have won even before you have started.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Yote yaliyoandikwa ni kweli. Lakini kuna nchi nyingine bado wana mila na desturi zile za kusema kwa nini msichana/mvulana huyo hajaolewa/hajaoa mpaka leo. Ana shida gana na wanaanza kusema labda tumpeleke kwa mganga.Kwani wao hawaamini kwa nini husiolewa au oa unangoja nini. Ila kwa ughaibuni hilo si tatizo nimeona wengi wanayafurahia maisha yao ya kuwa single wanasema wanauhuru

Lazarus Mbilinyi said...

Si kweli kwamba Ukiwa single unakuwa na matatizo au kasoro, hata kama ni binti umri kujikuta umri unaenda na huolewi hii ni kumaanisha kwamba una matatizo, kwanza idadi ya wanaume na wanawake duniani na jamii nyingi wanawake ni wengi kuliko wanaume so kama kila mwanaume anatakiwa kuoa mwanamke mmoja basi wanawake wengi watakuwa single.
Ila jambo Kubwa na muhimu ni kwamba wanawake single wengi ni single kwa sababu bado wanatafuta mwanaume bora kuolewa naye.
Ni vizuri jamii zetu zikafika mahali zikafahamu kwamba kuwa single si kumaanisha una matatizo na badala yake waone ni kitu cha kawaida.
Wapo wanandoa wengi sana wanaishi maisha ya upweke zaidi kuliko wale ambao ni single.
Pia jambo ka msingi ni kupata mtu anayefaa kuishi na wewe kwenye ndoa na si kuolewa au kuoa ili na wewe uonekane umeoa nau kuolewa huku kila siku migogoro na kugombana.