"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, August 23, 2008

Ukweli Kuhusu Wanaume

Wanaume viumbe wa ajabu sana, atakupa raha zote na ahadi kedekede, muhimu kutambua je, ni tamaa au upendo wa kweli? Ni vizuri wanawake wote wakajua kwamba:
Kufanya mapenzi kabla ya kuoana (premarital sex) na mwanaume haiwezi kukusaidia yeye ku – fall in love na au wewe kuwa mtu special kwake au kukuhakikisha mahusiano yanayoyumba yasimame vizuri au hata kusaidia mwanaume aji-commit kwako.

Mwanaume akiwa serious na mwanamke anayemtaka kumuoa ataweza kuvumilia sex kwa muda wowote mliokubaliana hadi ndoa.

Mwanaume anapokujia kuna mambo mawili kutoka kwake jambo la kwanza inaweza kuwa ni tamaa zake na jambo la pili ni upendo wa kweli.
Pia usichanganye hayo mambo mawili.

Kama mwanaume anakutaka kwa ajili ya tamaa zake, kitu cha maana anachokitaka kwako ni kutimiza malengo yake ya kukuchezea kwa ajili ya raha zake (sex).
He is just for fun
, hata kama atakuahidi mambo makubwa bado anakuwa lengo ni kukuchezea tu.

Kama mwanaume anakutaka kwa ajili ya upendo wa kweli, atakuwa tayari kuvumilia kukusubiri kwa sababu upendo wake ni zaidi ya sex, kwake maisha kwanza na yupo tayari kuvumilia.

Pia mwanamke kuwa bikira au mtakatifu (untouched) ni vitu ambavyo wanaume wanapenda sana, sababu ya msingi ni kwamba mwanaume akimpata mwanamke ambaye hajawahi kuwa na mwanaume mwingine hujisikia vizuri sana, anamwona ni mwanamke special na pia anampa feelings zaidi.
Hii ni kumaanisha kwamba jinsi mwanamke anavyokuwa na wanaume wengi kabla ya kuolewa hupunguza nafasi ya wanaume kujisikia vizuri kumuoa.

Njia nzuri ya kujua mwanaume anakupenda kwa upendo wa kweli uwezo wake wa kuwa serious na wewe ni jinsi anavyovumilia kuhakikisha mnaepuka sex kabla ya ndoa.

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

mmh hapo kazi ipo

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta firikia mmekubaliana kwamba hakuna kufanya mapenzi (sex) hadi siku ya ndoa, badala yake mwanaume anakuja kukwambia bila yeye kufanya mapenzi na wewe hawezi kukuoa na ili umridhishe asije akakuacha basi unakubali mfanye mapenzi, basi hapo fahamu kwamba kukubali kufanya mapenzi haiwezi kumfanya mwanaume asikuache wala akuone wewe ni special bali unajipunguzia uwezekano wa kuolewa. Kweli ni kazi kwani akina dada wengi huwa yanawashinda.
Lazima uwe na msimamo kwani mwanaume anaweza kuishia kukuacha kwenye mataa na huku amakuchezea pia ni dhambi.

Chemi Che-Mponda said...

Ninafahamu watu ambao wamesubiri hadi siku ya ndoa kufanya tendo la ndoa. Walisema kuwa ilikuwa raha kweli siku hiyo na wanashukuru kuwa walivumilia.

Lakini kweli utamaduni wa mjini Bongo kweli kuna kuvumilia. Zaidi ya kutembea na mwanaume anakuambia kuwa anataka uwe na mimba kwanza maana anataka kuhakikisha kuwa unaweza kuzaa!

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Chemi Che-mponda,
Kwanza nashukuru kupitia hapa na kutoa maomni yako.
Ni kweli siku hizi wapo wanaume wanasema bila kukupa mimba kwanza hawezi kukuoa.
Ni kama ujanja wa kisasa zaidi kwani wengi bado wameachwa kwenye mataa na hizo mimba.
Misingi ya ndoa hujengwa kwa kuvumiliana na mwanaume makini huvumilia na huko ni kujenga nyumba kwenye msingi imara tangu day one.

Anonymous said...

Thanks for This, Ila pia napenda kuongezea tu kuwa wengine si tamaa tu ya mapenzi bali hata kuwaachia maradhi. ILE TUFE WENGI. Tujali sana afya zetu na KUMUOGOPA MUNGU na pia kuwaepuka wale wenye tamaa ya ngono na si mapenzi ya kweli. Siku njema woteee na mungu Awabariki sana.
Msafiri - Arusha Tanzania