"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, August 4, 2008

Wataweza?

Sasa familia imeongezeka na nimepewa watoto wawili zaidi bure (rahisi kuwatambua kwenye picha).
Nimeamua kwenda nao moja kwa moja kijijini kwangu Wangama - Njombe Tanzania nao wakale vumbi kidogo, ugali na viazi then nione wame - adapt vipi kiasi cha kuwarudisha angalau Dar es Salaam wakae kidogo kabla ya kuwarudisha kwao.
Nimeanza na zoezi la kutembea pekupeku kwanza
(Kidding!)

3 comments:

Fikirikwanza said...

he!he!!
huo mfyedegalo sijawahi uona. Au ni wakikanada?

markus mpangala said...

hakika umeniacha hoi kabisa yaani nimekumbuka zama zile ukipata kandambili tu sherehe unajigamba na mikogo ya hapa na aple,unajiona wewe gangwe kisa uacha kutembea pekupeku. Umenikumbusha binti mmoja toka Bavari ujerumani alikuja nyasa hapa basi alipoon atunatembea pekupeku naye kawa anafanya hivyo,akaanza kucheza ligambusa ndugu yaani leo umenifanya nicheke sana na kuanzia kesho natembea pekupeku tena

Lazarus Mbilinyi said...

Basi kama kucheka ni tiba, Hongera sana kwa kucheka.

Hawa lazima wapite kwenye barabara ya kokoto nione kama wataweza pekupeku then tu naenda porini kutembea kwenye pori lililochomwa moto pekupeku.
Huo ndo mtihani wao wa "streetwise" za Africa.

Upendo daima!