"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, September 30, 2008

Kila mtu na kiatu chake

Watu wengi hudhani kwamba mwanaume akiwa mrefu basi na uume wake huwa mrefu hiyo si kweli.
Ingawa ni kweli kwamba kila mwanaume ana size tofauti ya uume kama wanaume wanavyotofautiana size ya miguu.

Katika kituo cha utafiti cha Masters and Johnson walipima uume wa wanaume 300 na kupata vipimo ambavyo vilionesha mwanaume ambaye alikuwa na uume mrefu sm 14 (5.5 in) alikuwa na kimo urefu wa sm 170 na mwanaume aliyekuwa na uume mfupi sm 6 (2.25in) kuliko wote alikuwa na kimo urefu sm 180.
Pia urefu wa uume hauna uhusiano na rangi ya mtu.

NB: Hata hivyo sikubaliani na hizi data kwani wanaume wa kijapan, korea na China wengi ni wadogo sana huwezi kulinganisha na Africa naamini hata size ya bunduki zao zitakuwa tofauti.

Je, uume ukisisimuliwa huwa na urefu kiasi gani?
Asilimia kubwa ya uume (karibia zote) huwa na urefu sawa zikisisimuliwa na kuwa tayari kwa ajili ya tendo la ndoa.
Uume ambao huwa mfupi kawaida husisimka na kuongezeka asilimia 100, wakati ule mrefu husisimka na kuongezeka kama asilimia 75 hii ina maana kwamba hata mwanaume mwenye uume mdogo ana built in compensation factor ili kufikia kiwango kinachotakiwa na kuwa sana na wale wenye bunduki ndefu na wanaume wote kuonekana wanauwezo wa kuwafikisha mwanamke pale anatakiwa kufika.


Je mwanamke yeye inakuwaje.
Kawaida uke huweza kuchukua uume wowote na size yoyote kama umesisimuliwa inavyotakiwa.
Kawaida uke wa mwanamke ambaye hajazaa ni wastani wa ireful wa sm 7.5 na mwanamke ambaye amewahi kuzaa huwa tofauti kidogo.
Na akiwa amesisimka uke wa mwanamke huweza kuongezeka urefu hadi sm 10, hii ina maana kwamba uume wowote unaweza kuingia labda itokee huyo mwanaume ana uume ambao umezidi sm 10.

Uke una uwezo wa ajabu kupanuka hasa pale kikiingia kitu chochote kirefu kuliko kawaida.
Utafiti unaonesha kwamba uke huweza kuongezeka size mara 150 au 200 zaidi ya size ya kawaida baada ya kusisimuliwa.
Hii ina maana kwamba mwanamke akisisimuliwa vizuri huweza ku accommodate uume wa aina yoyote.
Ila jambo la msingi ni maandalizi na si shughuli yenyewe kwani maandalizi mazuri hupelekea uume na uke kusisimka kiasi kinachotakiwa.

Na mwanaume kama una kiatu kirefu na kikubwa hakikiksha unamuandaa vizuri mke wako ili aweza ku-accommodate kiatu chako kwani anauwezo wa kuongeza size yake mwenyewe maradufu na kinyume chake ni kutesana na kuumizana.

Monday, September 29, 2008

Nambari One

Kila mmoja anapoacha baba na mama na kuanza maisha mapya na yule amempendaye, basi huwa amefanya uamuzi ambao ni wa maana na busara sana.
Mambo huwa ovyo sana, na huwa inakatisha tamaa sana unapoona mtu ambaye ulichukua uamuzi wa kuishi naye maisha yako yote anabadilika na kuweka vitu vingine kuwa namba moja badala yako.

Mwanaume au mwanamke anapoweka kitu kingine kuwa msingi kwake, kitu cha maana kwake, namba moja kwake na kutumia muda wote na uwezo wake wote kwa ajili ya hicho na mke au mume kuwa kitu cha pili yaani namba mbili.
Bila kumuweka mwenzi wako kuwa namba moja ujue hakuna kitu unaweza kununulia kwa pesa hapa duniani kikamridhisha na kuona unamjali na kumsikiliza.
Kwani hujasikia wanawake wengi ambao waume zao ni watu maarufu na wenye pesa wanalalamika kwamba bado hawahitaji pesa au vitu, wanachohitaji kupata muda na kupewa nafasi ya kwua pamoja, kusikilizwa na kujiona wanaume wanawajali.

Wapo wanaume ambao business ndo kimekuwa kitu cha kwanza kwake na mke anakuwa ziada na hata hudiriki kutoa pesa au vitu ili mke aridhike na kuona anamjali. Hii haina maana usifanye business ila lazima mke apewe muda wa pamoja na wewe na yeye kuwa muhimu.
Wapo ambao utadhani walizaliwa na TV na akiwa na TV mke au mume si lolote, TV anakuwa mke au mume.

Wengine hujikuta wanahangaika na kazi za kanisa (kazi za kanisa zingine si kazi za Mungu) fahamu ukristo wa kweli ni ule kanisa kuanzia nyumbani kwa mke na mume kuwa na amani ya kweli na maisha ya upendo kwa kutanguliza na kumjali mwenzako.
Wengi kazi za ofisini ndo zimekuwa mume au mke, Kumbuka kazi zipo ulizikuta na utaziacha mume au mke ni namba moja.

Wengine watoto ndo wamekuwa wa maana kuliko mume au mke nao pia wamewakuta na watawaacha wenyewe na maisha yenu, watoto wanahitaji upendo lakini isiwe wao wakasababisha mke au mume awe wa mwisho katika kusikilizwa.

Bila mume na mke kila mmoja kumpa nafasi ya kwanza mwenzake basi itakuwa ngumu sana kuwa na ndoa bora kama Mungu alivyopanga.

Sunday, September 28, 2008

Jumapili Njema

Nakutakia Jumapili njema yenye baraka na amani huku ukuburudika na nyimbo mbili kutoka kwa waimbaji wa Injili Africa.

Saturday, September 27, 2008

Each day you are provided with ample opportunity to choose between peace and conflict.
Just for today, make peace your modus operandi.
Lucy MacDonald

Friday, September 26, 2008

Wanautwika haraka!

Wanawake siku zote (si wote) wakinywa pombe kidogo tu hulewa na kuonekana wameutwika ile mbaya kuliko wanaume.
Wengine huenda mbali zaidi hata kujikojolea na kujisahau kabisa mahali walipo hubaki hapo hadi kilevi kitoke na wengine hata wakiutwika hukaa muda mrefu sana ili fahamu ziwarudie na fahamu zikirudi wengine huwa tayari mambo kadhaa mabaya wameshafanya au wamefanyiwa.
Why?
Timu ya wanasayansi ikiongozwa na Profesa Charles Lieber kutoka Mount Sinai School of Medicine New York Marekani, wamegundua kwamba wanawake wanakosa au wana upungufu mkubwa wa Enzyme ijulikanayo kwa jina la Gastric alcohol dehydrogenase (ADH), hii Enzyme huvunjavunja kilevi (alcohol) kabla ya kuingia kwenye damu.
Hii ina maana kwamba mwanamke akinjwa pombe kilevi huenda moja kwa moja kwenye damu bila kuchunjwa wala kuvunjwavunjwa kwanza kupunguza nguvu na sumu ambazo zinaweza kuwa kwenye pombe.

Pia wanatoa tahadhari kwamba wanawake wanaweza kuathirika zaidi na magonjwa yanayohusiana na ulevi haraka kuliko wanaume kama vile Cirrhosis ya Ini na Dementia

Pia wapo wanaume hutumia kilevi kama chambo kuwapata wanawake kwani wanafahamu kiwango sawa mwanamke hulewa zaidi.

Kumbuka ulevi ni mbaya kwa wanawake na wanaume husababisha familia mambo kwenda ndivyo sivyo.

Hutahukumiwa kwa kuwa ulikuwa mlevi bali kwa sababu ulikataa yule anayeweza kuondoa kiu ya kilevi yaani Kristo.
Dada kautwika hadi anajihisi yupo kwenye Queen bed yake home.
Pombe si chai au soda

Katika pitapita nimekutana na huyu Fireman!

Ndoa ni Marathon

John Stephen Akhawari ni mtanzania mwenye sifa ya pekee kwa kumaliza marathon na si kushinda. Kwa maelezo zaidi soma hapa:
http://mbilinyi.blogspot.com/2008/08/maisha-nayo.html Ndoa inafanana sana na ukimbiaji wa mbio ndefu (marathon) na hutoa matokeo mazuri sana pale wanandoa wanapofahamu kwamba mbio za ndoa yao si mbio fupi (sprint)
Sababu kubwa inayofanya wakimbiaji wa mbio fupi kushindwa kukimbia mbio ndefu (marathon) ni kwa sababu akili zao wameziwekwa au zimezoeshwa kukimbia mbio fupi (mita 100 tu) na si zaidi ya hapo.
Mawazo yao kichwani ni mita 100 tu na kuwaambia wakimbie mita 1000 husababisha kushindwa hata kabla hawajakimbia kwa sababu ya mindset zao na mazoezi na malengo ya taaluma zao.
Hatujawahi kusikia mkimbiaji maarufu wa mbio fupi (sprinter) ameweza kupata medali ya mbio ndefu (marathon), ni vigumu mno.

Kwa nini ndoa nyingi huishia njiani?
Ndoa nyigi (si zote) huishia njiani kwa sababu wanandoa huanza safari ya ndoa kwa kuwa wakimbiaji wa mbio fupi badala ya mbio ndefu yaani marathon.
Hujazwa na mawazo ya furaha muda mfupi badala ya kuangalia mbali zaidi miaka 100 ijayo.
Akiumizwa kidogo au kukutana na tatizo kubwa au shida nzito au jaribu kubwa hujiona kama hastahili kuumizwa na pia kama mwenzake anampenda basi amisha ya ndoa ni raha na mstarehe.

Mkimbiaji mzuri wa marathon hawezi kuacha kukimbia akipata maamivu kwenye miguu, au kuchoka au mushikwa na misuli au kukumbana na hali mbaya ya hewa jua kali au baridi kali huwa hakati tamaa huendelea kukimbia huku akivumilia kwani lengo ni kuhakikisha anamaliza hadi mwisho.

Wanandoa wengi huamini kwamba kama umempenda mtu basi ndoa itakuwa rahisi na mteremko kama nyikani kwenye mawindo, waulize wanandoa wote ambao wamekaa kwenye ndoa zaidi ya miaka 10 acha miaka 50, wote watakwambia walipitia hatua zote za kukutana na matuta, siku za giza nene, siku ambazo hujisikia kama mume au mke hafai tena kwa kuwa lengo ni mbio ndefu ndoa zao bado zina Baraka hadi leo.

Usiwe mkimbiaji wa mbio fupi, anza kujizoeza kuwa mkimbiaji wa mbio ndefu za ndoa yako.
Wakati unakimbia marathon kuumia au maumivu ni kitu cha asili hakikwepeki kilichopo ni kupambana tu.
Bila kuwa na maumivu huwezi kumaliza marathon na bila kumaliza marathon huwezi pewa medali.
Biblia yenyewe inasisitiza pia kwamba duniani shida hazikwepeki na lazima tuzishinde
(Yohana 16:33)

Kuachana na kumkimbia mwenzako si jibu kwani hata ukae mwenyewe bado utakutana na shida acha zile za upweke na Ukisema utafute mwanaume/mwanamke mwingine huyo ndo atakupa shida mpya kabisa ambazo zitakupeleka ground zero tena.

“If you are defeated in your mind, you are already lost the battle”
In life there is no success without hardship, it is part of life.

Thursday, September 25, 2008

Karudi Mwenyewe!

Mzee Hibwa had an argument with his wife who got too angry, packed her bags and went back to her parent’s home.
Unfortunately for her, she had to pass her husband's home everyday as she went to and from work and even to the shops.
Days passed and still Mrs. Hibwa did not go back to her house until Mzee Hibwa realized that she was not coming back and he decided to go to supermarket in town and he bought five XXL ladies panties (Chupi) in five different colours.

Then here comes Hibwa's wife passing by her house going to her parent’s home only to see one XXL Red panty hanging from the kamba ya kuanikia nguo, she pretends to ignore it!

The following day there is a XXL Pink panty hanging on the line....she once again pretends to ignore it but she is fuming inside.

The next morning there is a Blue panty hanging on the kamba and guess what? She couldn't hold it any longer...... ....
Mzee Hibwa sees his fuming wife approaching him,
"Hibwa wee Hibwaaaaa Hiibwa .........no fat woman of yours will make me leave my home, I am back........ ." .."Sasa mlete huyo mwanamke wako mnene nimwonyeshe, siogopi unene mimi kama ni mijinyama hata kwenye sambusa ipo" "...kwa taarifa yako sasa leo nimerudi na siondoki hapa ng'o...

Source: Mtandao


Wednesday, September 24, 2008

Wanaume Huchochea Mwendo!

Wanawake hupunguza mwendo wakati wanaume huchochea na kuongeza mwendo.
Wanawake hupenda kuguswa mwili mzima (mwili wake wote ni single sex organ) linapokuja suala la kusisimuana kimapenzi.
Ni mara chache sana wanaume hufahamu mwanamke anahitaji nini linapokuja suala la mapenzi na hata kama anafahamu basi akiingia chumbani baada ya muda kidogo anasahau na kuendelea kufanya kile anataka yeye.

Mwanamke anahitaji mwanaume mwenye mikono slow wakati wa kusisimuliwa na kuandaliwa kuwa tayari kwa tendo la ndoa, hata hivyo mwanaume akishakuwa amesisimka husahau na kuendelea kuwa na mikono mwepesi kukimbilia sehemu muhimu ambazo mwanamke husisimka zaidi akidhani wote wanahitaji mwendokasi sawa.
Ni jukumu la mwanaume kufahamu mahitaji ya mwanamke wakiwa faragha hii ni kuhakikisha mwanamke anaridhika kupata kile anastahili.

Tendo la ndoa ni uzoefu wa tofauti kwa mwanamke na mwanaume pia, raha anayoipata mwanaume hasa akishasisimka ni hitaji kubwa la kutaka kuingiza na kutoa (release), kama vile nguvu ya kutaka kutoa risasi kwenye bunduki.
Mwanamke yeye akishasisimka na kuwa wet huwa na hitaji kubwa la kupokea, yaani hitaji la kutaka kitu kuingia ndani yake.

Kwa kuwa mwanaume huwa na nguvu hasa ya kutaka kutoa sperms ili kufika kileleni hivyo akishasisimka tu anatamani kuingiza na kutoa, wakati huohuo mwanamke akishasisimka huwa anakuwa na hamu kubwa ya kupokea, kuingiziwa kitu na kujaziwa hadi aridhike, hivyo basi kama mwanaume ana mwendokasi na kumaliza haraka hitaji la mwanamke kutaka kujaziwa raha inaweza isifike mahali panapotakiwa na matokeo yake hujisikia ametumiwa tu na mwanaume kufanikisha raha yake ya kuingiza na kutoa vitu vyake.

Jambo la msingi ni kuhakikisha mwanamke anaandaliwa na kupokea raha ya kutosha hata kabla mwanaume yaja release na kumaliza raha yake.

Mwanaume anahitaji kuwa mtundu kuhakikisha anaanza kwanza na layers ambazo si sensitive moja baada ya nyingine huku akiwa na mikono slow ili kuhakikisha mwanamke anapata raha ya mwili mzima kabla ya kupokea kitu.

Kumbuka!
Mwitikio wa kusisimuliwa kwa mapenzi kwa mwanamke ni mzunguko unaohusisha saikolojia, mazingira na homoni pia anaweza kuathiriwa sana na hisia, mawazo, lugha, utamaduni na sababu za kibaolojia, hivyo kitu cha msingi ni kuhakikisha kabla ya kufika mbali ana hamu na anatamani tendo la ndoa.

Tuesday, September 23, 2008

Bei ya Ndoa

Mpaka kifo kitakapotutenganisha! Kama upo kwenye ndoa na upo kwenye tatizo kubwa, shida au mgogoro wowote na unajisikia kama ni wewe mwenyewe tu mwenye Matatizo ya ndoa, ukweli hupo mwenyewe kwa sababu kutokuwa na Matatizo hakufanyi ndoa kuwa imara bali ndoa huwa imara kwa sababu wanandoa wanajua jinsi ya kupambana na Matatizo kwa pamoja vizuri.

Ndoa imara na zenye afya zinajua jinsi ya kupambana na hali ngumu.
Ni kawaida kila ndoa kukutana na mambo magumu katika safari ya maisha duniani.
Wakati mnaendelea na mahusiano iwe uchumba au ndoa mnaweza kukutana na tuta kubwa la ugonjwa, kuachishwa kazi, kupoteza nyumba, kifo cha mmoja katika familia yenu kama vile wazazi, biashara kuyumba kabisa au kufirisika, hapo utafanyeje?
Tumesikia mara nyingi sana watu wakiwakimbia wapenzi wao au wake zao au waume zao pale moja ya hayo linapotokea.

Ukweli ni kwamba huwezi kujua ndoa yako au uchumba wako ni imara kiasi gani hadi pale utakapojaribiwa.

Matatizo yakitokea mara nyingi huweza kuvunja mahusiano vipande vipande mume huku na mke huko au wachumba kila mmoja kuachana na mwezake.
Lakini habari njema ni kwamba, wanandoa au wachumba ambao wanaweza kupita katika ugumu wowote pamoja kwa kushikamana kama super glue huwa na mahusiano imara yaliyoyoshikamana kwa nguvu za ajabu na kuwa na upendo imara kuliko mwanzo.

Wengi hujiuliza kwa nini hili litokee kwetu tu?
Kwa nini Mungu amenitupa kiasi hiki?


Mary mwalimu wa shule ya msingi huko Njombe anasimulia kwamba mume wake amefirisika biashara yake na baadae wakapata pigo lingine nyumba yao ikaungua moto yote pamoja na mali zote.
Iliwalazima kujihifadhi kwa majirani, hata hivyo anakiri kwamba hakuna wakati wamewahi kuwa karibu na kujisikia kitu kimoja tangu waoane miaka 5 iliyopita, kwao Matatizo yamejenga ndoa yao.

Ndoa si kunywa soda kila siku ukipata kiu, si kuwa na pesa kila siku, ndoa ni kazi, kazi inayohitaji kujitoa, hata hivyo matokeo ya kushirikiana pamoja hasa wakati wa shida kwa kushikamana bila kujali ugumu unaotokea ndoa huwa imara na yenye afya ya ajabu.

Wengine likitokea tatizo kwenye ndoa au uchumba solution ni kuacha na kutafuta mwingine, huo ni ujinga, kila binadamu ana Matatizo yake mapya kabisa na ovyo kabisa.

Jaribu kufikiria kwa nini ulimkubali na kuona anakufaa?


Are you the part of the problem or part of the solution?

Monday, September 22, 2008

Wewe Ungesemaje?

Nimeulizwa swali na mtoto wangu Emmanuel (Miaka 5); nimjibu bila kusitasita pia wazi kabisa kwa ukweli mtupu.
Ameniuliza:
Je, nani nampenda zaidi kati yake (Emmanuel) na mama yake (mke wangu)?
Ili kumjibu swali lake ilibidi nifikirie sana na kuwaza hadi miaka 80 ijayo na zaidi, pia miaka mingi hata kabla yeye mwenyewe hajazaliwa.

Nimemwambia wazi kabisa kwamba nampenda kwa sababu ni mtoto wangu, ila linapokuja suala la nani nampenda zaidi nimemwambia nampenda zaidi mama yake ambaye ni mke wangu na sababu kubwa ya msingi ya kumpenda zaidi mke wangu kuliko yeye ni kwamba;
Yeye kwanza alinikuta mimi tayari naisha na mama yake yaani alinikuta mimi naisha na mpenzi wangu ambaye ni mama yake na ataniacha na mama yake ambaye ni mke wangu akiwa mkubwa.

Ataenda kwa mke wake na huko nikitaka kuja au kumtembelea acha kuishi na yeye; nitatakiwa kumuomba ruhusa ili anikubali.

Ndiyo maana nampenda zaidi mama yake kwani yeye ni mpitaji tu siku akiwa mkubwa hata nimwambie abaki hatakubali au mke wake hatakubali hivyo nampenda zaidi mke wangu ambaye naweza hata kufia kifuani mwake.
Hii haina maana kwamba simpendi, nampenda sana na kumpa mahitaji yake na haki zake, ila likija suala la mke wangu yeye ni namba moja.

Je, mwenzangu ungeulizwa kati ya mke na mtoto au mume na mtoto yupi unampenda zaidi ungesemaje?
Na ungetoa sababu zipi?

Sunday, September 21, 2008

Jumapili Njema

Nakutakia Jumapili njema kwa wimbo Uitwao Haleluya Kembo ambao umeimbwa na mabinti wa DRC- Congo

Saturday, September 20, 2008

Kitinda Mimba

Eti vitinda mimba wengi hudeka sana? Wataaalamu wa masuala ya haiba na saikolojia ya watu wana mengi ya kusema kuhusu nafasi unayozaliwa katika familia (birth order) na athari zake.
Ukweli ni kwamba watoto kuwa tofauti kitabia hutokana nafasi yako katika kuzaliwa (wa kwanza, katikati au mwisho) ktk familia, aina ya wazazi, idadi ya watoto na wakati mwingine mazingira na malezi.
Kwa mfano ukizaliwa peke yako automatically utakuwa na tabia aidha za kifungua mimba au kitinda mimba.

Kitinda mimba wengi huwa ni watu ambao wanajichanganya sana kwani tangu watoto huwa wanakuwa na hali ya kujihusisha na wengine na si watoto wa kuchungwa sana kama kifungua mimba hivyo huwa na ujasiri wa kufanya jambo lolote hata kama lina risk kubwa.

Pia kitinda mimba huwa na tabia tofauti kwani wazazi huwa hawaelekezi nguvu nyingi kama kifungua mimba (hawako strictly sana) na pia kitinda mimba yeye siku zote hubaki mtoto tu kwani hana mwingine chini yake na kila analosema na kufanya kwa wazazi huhurumiwa kwa kuwa yeye ndo mtoto.

Hawa vitinda mimba mara nyingi hupewa kila wanachohitaji hadi wanakuwa spoiled na matokeo yake huwa wanadeka sana.
Pia hawa huwa hawaogopi maisha kila kitu hukiona rahisi tu hawana shida sana ya kuwaza kwamba maisha ni vita badala yake huona maisha kama zawadi tu ni kuishi.

Je, unahisi kuoa au kuolewa na kitinda mimba huweza kuathiri ndoa kwa kiasi fulani?

Hawavumi lakini wamo!
Hawa ni wananchi wa Papua New Guinea wakihakikisha na wao hawapitwi mbali na ICT.
Ukitaka kujua ni akina nani angalia wanaume wamevaaje au bonyeza http://mbilinyi.blogspot.com/2008_07_01_archive.html

Friday, September 19, 2008

Kifungua Mimba

Kwa kuwa u kifungua mimba nahisi unaweza kuwa kiongozi mzuri au rais! Emmanuel Lazarus Mbilinyi
Kuna imani nyingi za kweli na za uwongo kuhusiana na mtoto wa kwanza kuzaliwa yaani kufungua mimba.
Pia ni kweli kwamba kwa wazazi, mtoto wa kwanza kuzaliwa awe kike au wa kiume huwa kuna kuwa na uzoefu wa tofauti sana na huleta challenge kubwa mno kwa wazazi.

Watafiti wengi na Wanasaikolojia wengi wana imani kwamba mtoto wa kwanza kuzaliwa huwa na sifa tofauti na watoto wanaofuatia na hata mtoto wa mwisho kuzaliwa yaani kitinda mimba na pia kumekuwa na migongano mingi sana kukubaliana kwamba kifungua mimba huwa tofauti na watoto wengine, wengi wanakataa kabisa na wengine wanakubali.

Zifa zifuatazo huendana sana na mtoto wa kwanza kuzaliwa kama vile kuwa na Akili (intelligence), hii hutokana na kuwa na exposure kubwa na watu wazima tangu akiwa mdogo kitu ambacho humpa uzoefu wa tofauti.

Pia vifungua mimba wanajulikana vizuri sana kuwa na uwezo wa kuongoza au kuwa viongozi labda hii ni kutokana na kupewa jukumu la kuongoza wenzake wanaofuatia tangu akiwa mtoto.
Utafiti unaonesha kwamba marais wengi wa marekani walikuwa ni vifungua mimba katika familia zao.

Pia vifungua mimba wengi ni watu ambao wapo organized ni watu ambao wakipewa project ni moja ya watu ving'ang'anizi huhakikisha wanamaliza.

Utafiti pia unaonesha kwamba vifungua mimba wengi hujiamini sana, hii ni kutokana na wazazi kuwapa support kubwa tangu siku ya kwanza wanapozaliwa.

Kama wewe ni mzazi je, ulijisikiaje ulipopata kifungua mimba wako?

Na kama wewe si kifungua mimba kama mimi je, unaamini haya ni ya kweli?

Thursday, September 18, 2008

No one falls in love by choice,
it is by CHANCE.
No one stays in love by chance,
it is by WORK.
And no one falls out of love by chance,
it is by CHOICE

Mama na Mwana!

Vitu vingi ambavyo mtoto wa kiume hujifunza kwanza, hufundishwa na mama yake na hii humfanya mama kuwa mtu wa tofauti kwa mtoto wa kiume. Kwa mtoto wa kiume mama ni mfano wa kuigwa kwa kuwa ndiye anayempa picha kamili kufahamu wanawake wanakuwaje.
Sauti ya kwanza kuisikia na tabasamu la kwanza kulipata hutoka kwa mama yake, na watoto wengi huanza kutamka nena Mama mapema kuliko Baba.

Ni mara nyingi sana kuona watoto wa kiume wakiiga baba zao na kutaka kuwa kama baba zao hata hivyo mama huathiri sana maisha ya mtoto wa kiume katika mahusiano na wasichana (uchumba hadi ndoa).
Kuna msemo kwamba mtoto wa kike huelekeza antenna yake kwa baba na mtoto wa kiume huelekeza antenna yake kwa mama hata hivyo mama huweza kumfundisha vizuri mtoto wa kiume kuwa caring and loving.

Upendo wa mama kwa mtoto wa kiume unavyozidi kuwa strong huwa wanajenga bond ambayo huwezesha mama na mtoto wake wa kiume kushikamana kiasi kwamba ikitokea mtoto wa kiume akapata mchumba au mke mama hujisikia kupungukiwa kitu na hatimaye mama huanza kuingilia ndoa au mahusiano ya mtoto wake.
Hii hutokana na gap la nafasi (upweke) ambayo mtoto wake aliijaza na sasa kahamishia kwa yule anampenda mchumba au mke.
Wakati mwingine hii huenda mbali zaidi kwani wapo watoto wa kiume ambao hata maamuzi yao ndani ya ndoa zao na mahusiano kila kitu huamriwa na mama zao.
Pia hufika mahali kijana wa kiume huweza hata kudai huduma kama zile alikuwa anapata kwa mama yake kama vile vyakula na baadhi ya tabia.

Ukweli unabaki kwamba mtazamo wa ulimwengu kwa mtoto wa kiume huathiriwa zaidi na malezi ya mama.

“Mwanangu, shika maagizo ya baba yako, Wala usiache sheria ya mama yako”
Mithali 6:20

Wednesday, September 17, 2008

When one door of happiness closes, another opens;
but often we look so long at the closed door that we do not see the one which has been opened for us.
Also
To Forgive is the Highest, most Beautiful form of Love.
In return, you will receive untold Peace and Happiness.
Robert Muller

Baba na Bintiye!

Kuna tafiti nyingi zimefanywa ili kuangalia ni jinsi gani baba anaweza kuathiri maisha ya mahusiano ya mtoto wake wa kike na wanaume wengine akiwa mkubwa.
Ukweli ni kwamba baba huathiri sana future ya binti yake katika mahusiano na wanaume.

Baba ni role model na mwanaume wa kwanza kwa binti kujua anaweza kuongea nao vipi na hata socialization na wanaume wengine baadae akiwa shule au katika maisha yake.

Pia utafiti uliofanywa na Vanderbilt University huko New Zealand, umeonesha kwamba watoto wa kike ambao huwa karibu (close & supportive) na baba (au wazazi) huchelewa kubalehe kuliko watoto wa kike ambao huwa mbali na baba (Wazazi).
Hii ina maana kwamba watoto wa kike ambao hupata upendo wa baba huweza kuzalisha homoni za pheromones zinazozuia kubalehe haraka, na wale ambao hukosa upendo na ukaribu wa baba hizo homoni za pheromones huchochea kuwahi kubalehe kwa binti hasa kutokana na binti kujihusisha na wanaume ambao ni nje ya familia.

Pia utafiti huo umeonesha antenna za mahusiano za mabinti hujielekeza kwa baba zaidi kuliko kwa mama tangu binti anapokuwa mdogo hadi anakuwa mtu mzima hii ina maana kwamba maisha ya baba pamoja na malezi yana effect kubwa sana kwa binti yake na mahusiano yake akiwa mkubwa.
Hii ina maana kwamba maisha ya ndoa ya binti hutegemea pia baba aliishi vipi na binti yake pamoja na mama yake na familia kwa ujumla.

Hata hivyo katika jamii bado tunakutana na akina baba ambao ni wanatunza familia, wengine huthalilisha mabinti zao, wengine hukimbia watoto wao (anaweza kuwa wa kike), wengine hutesa mama wengine hupendelea watoto wao wakiume na kuacha binti na mama yake.

Baba uwe makini!

Sources: http://findarticles.com/p/articles/mi_m0FCR/is_4_35/ai_84017198/pg_1?tag=artBody;col1
http://www.sciencedaily.com/releases/1999/09/990927064822.htm

Tuesday, September 16, 2008

Wanawake ni kama Mawimbi

Mwanamke akijisikia vizuri basi furaha yake humpeleka kuwa juu sana (peak) na mood ikibadilika basi hali yake hubadilika ghafla na kuvunjika hadi chini kabisa kama mawimbi, wakati huohuo akiwa chini (low) sana kihisia anaweza kubadilika mood tena na kuanza kupanda juu kama mawimbi.
Wakati akiwa juu kileleni katika hisia zake basi hujisikia vizuri hata hutoa upendo wake kwa wengine na pia kitendo cha kuwa chini sana husababisha upweke ndani yake na hapo ndipo anahitaji mwanaume au mtu yeyote ambaye anaonesha caring na kumsikiliza.
Anaokuwa chini kihisia basi love tank yake emotionally huhitaji kujazwa!
Je, dada zetu na mama zetu huwa mnajisikia kupanda na kushuka kwa mood kama mawimbi?
Tujadili!

Monday, September 15, 2008

The world is a great mirror.
It reflects back to you what you are.
If you are loving, if you are friendly, if you are helpful, the world will prove loving and friendly and helpful to you.
The world is what you are.
Thomas Dreier

Maksi ni zilezile!

Zawadi ni zawadi, muhimu ni Caring anayopata kutoka kwa mwanaume Wanaume wengi (si wote) hudhani kwamba kumpa mwanamke zawadi kubwa, au kumnunulia kitu cha thamani kubwa kama gari au nyumba au kumfanyia jambo kubwa kunampa alama kubwa (maksi) na ni kuonesha mapenzi makubwa na kwamba kwa kufanya hivyo basi mwanamke hastahili kutokuwa na furaha.

Ukweli ni kwamba kila zawadi au jambo unalofanya kwa mwanamke lina nafasi sawa au maksi moja tu kati ya mia, hivyo basi ukimnunulia gari unapata maksi moja, ukimjengea nyumba unapata maksi moja, ukimnunulia pipi unapata maksi moja, ukimbusu unapata maksi moja, ukimsaidia kufua nguo unapata maksi moja, ukimpeleka vacation nje ya nchi unapata maksi moja, ukimkumbatia unapata maksi moja, ukimpa neno la kumtia moyo unapata maksi moja nk.
Ukiongea naye kwa kumsikiliza unapata maksi moja, ukimununulia chocolate unapata maksi moja, ukimnunulia kiatu cha kisasa unapata maksi moja pia.
Kwa mwanamke zawadi zote zina thamani sawa, iwe kubwa au ndogo, kumfanyia vitu vidogo vina thamani sawa na kumfanyia mambo makubwa, hii ina maana kwamba kumpa zawadi kubwa au zawadi ndogo humpa furaha sawa.

Mfano
James ni Daktari kwenye hospitali moja kubwa jijini DSM Tanzania na kazi yake ina pesa nyingi sana kiasi kwamba familia yake imeweza kujenga nyumba, kusomesha watoto, kununua gari na kulipa bills kwa ajili ya mahitaji muhimu ya familia yao.
Daktari James anaamini Mkewe Mariamu anastahili kuwa na furaha kwa sababu fedha anazopata zinawezesha wao kuwa na maisha bora na pia haoni umuhimu wa yeye kusaidia mkewe kazi ndogondogo na kuwepo nyumbani kwa ajili ya kukaa na familia, hivyo wakati mwingie huchelewa nyumbani kuendelea kufanya kazi ili apate pesa nyingi mke afurahi zaidi.

Mkewe Mariamu ni mama wa nyumbani, yeye hufanya kazi za pale nyumbani na zaidi huhakikisha kila kitu pale nyumbani kipo in order.
Mkewe Mariamu analalamika kwamba mumewe kwanza anachelewa nyumbani, pili hasaidii kazi ndogo ndogo za pale nyumbani, hana muda na mumewe anajisikia upweke na anajisikia mumewe hamjali.

Daktari James naye haoni sababu kwa mkewe kulalamika na Kutokuwa na furaha kwani yeye anapata pesa nyingi kuipa support familia na ameshajenga nyumba na kuinunulia familai gari.
Anaamini kuwa na pesa nyingi ni zawadi tosha kwa mke na mke anastahili kuwa na furaha.
Pia James anaamini kuwa anapofanya kazi kubwa ya udaktari na kupata pesa nyingi hastahili kufanya kazi ndogo ndogo pale nyumbani kumsaidia mkewe.

Anaamini pay cheque yake ina point nyingi (maksi 80) kuliko pengine kumsaidia mkewe kutandika kitanda (maksi 1) hajui kwa mwanamke kuwa na pay cheque kubwa kuna maksi moja na kumsaidia kutandika kitanda kuna maksi moja tu.

Unapotaka kumuelewa mwanamke huhitaji kuwa logical bali emotional, mwanamke yupo after romance, jinsi unavyompenda, unavyomsaidia vitu vidogo, unavyomsikiliza, unavyombembeleza, unavyompa muda wa kuwa pamoja na kufurahia, unavyombusu, unavyomkumbatia, unavyomtia moyo, unavyocheza naye nk, kwake ni muhimu kuliko kununua gari au nyumba na kuamini kwamba hapo mwanamke atakuwa na furaha na hana sababu ya Kutokuwa na furaha.
Unaruhusiwa kumfanyia mambo makubwa sana lakini kumbuka anza kwa kumfanyia mambo madogomadogo kwanza.

Kwa kuwa umefanya mambo makubwa haina maana kwamba hutakiwi kufanya mambo madogo na kwamba mambo makubwa au zawadi kubwakubwa ukimpa hana sababu ya Kutokuwa na furaha na kuona unamjali.

Sunday, September 14, 2008

Saturday, September 13, 2008

Miaka 80 ya Ndoa

Frank na Anita Milford wakati wa Aniversary ya miaka 80 ya Ndoa yao Huko Uingereza wanandoa wazee Frank miaka 100 na Anita miaka 99 hivi karibuni waliadhimisha sherehe yao ya kumbukumbu ya Ndoa Kutimiza miaka 80


Walikutana mwaka 1926 na kuoana tarehe 26 Mei 1928, wamebarikiwa kuwa na watoto wawili, wajukuu watano na vitukuu saba
(Kweli familia za kizungu hawazaliani)


Wao wanakiri kwamba na kushauri kwamba ili ndoa idumu kuna umuhimu wa wanandoa kumaliza tofauti zao kabla ya kwenda kulala kitandani na pia kutumia muda mwingi pamoja.

Pia Malkia wa Uingereza amewatumia zawadi ya kadi ya kuwapongeza wanandoa hawa kutimiza "Oak Annivesary" ya ndoa yao kitu ambacho kutokana na kumbukumbu za kitabu cha Guinness wanandoa waliovunja rekodi nchini Uingereza walifikisha miaka 81.

Nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa mafanikio makubwa kama hayo, naamini ni mfano tosha kwa sisi ambao safari bado bichi kabisa na ndefu maana miaka 80 pamoja si haba milima na mabonde bado ipo mbele.

Wanawake tu!

Hapo ni wanawake tu, mwanaume huruhusiwi

Ni jambo la kawaida kutenganisha wanawake na wanaume wakiwa jela Prisons, mabweni, au kutumia vyoo, baadhi ya michezo na hata shule.
Hata hivyo kuna baadhi ya nchi utumiaji wa mabasi ya abiria (public transport) suala la kutenganisha wanaume na wanawake halikwepeki.
Abiria hutenganishwa aidha kwa kila jinsia kutumia mabasi yake ( wanaume mabasi yao na wanawake mabasi yao) au basi moja linalotenganisha wanaume mbele na wanawake nyumba.

Kuna nchi kama Japan, Misri, India, Taiwan, Brazil, Mexico, Belarus na ufilipino nk wameamua kutenganisha huduma ya mabasi kwa kuwa na mabasi ya wanawake (women only buses) na mabasi kwa ajili ya wanaume hii ni kutokana na vitendo vya kidhalilishaji ambavyo wanawake wamekuwa wanapata kutoka kwa wanaume wahuni na ili kunusuri hiyo hali sasa kila jinsia na mabasi yake.
Huu usafiri huweza kuwa muda wote au muda fulani katika siku na inaweza kuwa kwenye train (subway) au mabasiPicha juu Basi la wanawake mengine huendeshwa na wanaume na mengine huendeshwa na wanawake wenyewe.

Pia zipo baadhi ya dini hutenganisha waamuni wanawake na wanaume wakiwa kwenye ibada kiasi kwamba ibada inapoendelea hakuna kuonana wanawake na wanaume.
Na zipo dini zingine zimetenganisha milango ya kuingilia ndani ya nyumba zao za ibada.

Sijajua sababu hasa ni ipi, au wasitamaniane? yaani hadi kwenye nyumba za ibada?

Picha juu ni Wanafunzi wa shule (DSM) wakiwa wameduwaa baada ya Konda kuwaambia wakiingia tu angewafanyia kitu mbaya
(Globalpublishertz)


Wakati nchi kama Tanzania hata suala la mabasi ya wanafunzi limeshindikana Serikali ikiwa imeshona masikio kwa super glue na kushindwa kutatua hili tatizo.

je, hili la wanawake na kuwa na mabasi yao hasa kutokana na wanawake kudhalilishwa linaweza kufanyika?

Friday, September 12, 2008

“The road of life twists and turns and no two directions are ever the same.

Yet our lessons come from the journey, not the destination.”

Akiiva na Kuwa Tayari - Rahisi

Wanawake ni kama mwezi na wanaume ni kama juaWanawake ni mfano wa mwezi (moon) katika mwitikio na uzoefu wa tendo la ndoa.
Wakati mwingine bila kujali ana mwenzi anayejua mapenzi (mwanaume) kiasi gani, anaandaliwa (foreplay) na kuwa hot kiasi gani au kuwa wet south pole kiasi gani, bado anaweza asifike kileleni wakati wa tendo la ndoa.
Si kwamba tu hawezi kufika kileleni, bali hitaji kufika kileleni.

Katika siku 28 za mzunguko wa siku za mwanamke, kuna siku akiwa
AMEIVA NA KUWA TAYARI
basi hupenda na kutaka afike kileleni.

Na siku zingine katika mzunguko hupenda tu kufanya tendo la ndoa kwa ajili ya kuwa close na mume wake na wala hajali kufika kileleni au kutofika.
Wakati mwingine anakuwa katika mzunguko ambao ni full moon, wakati mwingine ni half moon na wakati mwingine ni new moon katika stages zote hizo utendaji huwa tofauti ingawa anaweza kuwa na hamu ya sex na mumewe ingawa si lazima kufika kileleni na anajisikia raha na furaha kuwa hivyo.

Kwa upande mwingine, wanaume mwitikio wao ni mfano kwenye sex ni mfano wa jua kwa maana kwamba kila asubuhi huchomoza na smile la nguvu.
Hakuna nusu jua wala robo jua wala jua jipya kila siku ni jua lilelile na akisisimuliwa tu kimapenzi kileleni atafika tu.
Mwanaume akisisimuliwa, mwili wake automatically hutamani kufika kileleni na hawezi Kukosa hata kimoja.
Na hapa ndipo mwanaume huwa kwenye giza nene kutojua kwa nini mamsapu wake wala hajali kufika kileleni, na anaweza kufika mbali kwa kudhani kwamba kuna mushkeli.

Tatizo kubwa ni kwamba wanaume hupima uwezo na mafanikio ya tendo la ndoa kwa mwanamke kufika kileleni.
Kumlazimisha mwanamke kufika kileleni kila kukiwa na tendo la ndoa huweza kusababisha mwanamke kujisikia haridhiki kwani inabidi wakati mwingine adanganye (fake orgasm) amefika kumbe wala na yeye alitaka sex just to feel close.

Tendo la ndoa tamu ni lile ambalo huacha hisia na kumbukumbu bila kusahaulika na wakati mwingine hufanywa kwa hiari bila kulazimisha mwanamke kufika kileleni, pia kuruhusu kila partner kupata kile anataka kwa mume kufika kileleni na mwanamke kama hana au ana mood kuweza kufika kileleni na zaidi apate physical affection.

Thursday, September 11, 2008

Listening


“Listening is a magnetic and strange thing, a creative force. The friends who listen to us are the ones we move toward. When we are listened to, it creates us, makes us unfold and expand.”

Mwanamke ni Kusikilizwa!

Mashitaka mengi tunayopata wanaume kutoka kwa wake zetu ni kwamba;
Huwa hatuwasilikizi na pia hatuwajali”

Kumsikiliza mwanamke anapoongea ni pamoja na kuachana na kile ulikuwa unafanya, concentrate kwenye kile anaongea, kusikiliza hisia zake zinaongelea kitu gani na si kile mdomo unaongea tu.

Wanaume tunahitaji kufahamu kwamba wanawake mara nyingi huongelea matatizo yao kwa maana ya kuwa karibu na sisi na kupata ahueni kutokana na matatizo yanayaowapata, si lazima mwanaume kuanza kutoa solution ya matatizo anakwambia.

Kama tulivyosema huko nyuma kwamba mwanamke akipata matatizo hutafuta mtu maalumu wa kuongea naye, kumshirikisha hisia zake na kile kitendo cha kuongea humpa ahueni (relief) hivyo basi mwanaume kazi kubwa ni kumsikiliza na zaidi sana kuhakikisha anafahamu kwamba unamsikiliza.

MFANO
Mariamu anarudi nyumbani akiwa hoi na kazi pamoja na kusumbuliwa na bosi wake.
Anaporudi home anajisikia ni vizuri kuongea na mumewe.
Fikiria Mariam ana wanaume wawili mmoja wa kweli (James) na wa pili ni kwa ajili ya kutufanye tuelewe mfano (Kelvin).
Unadhani ni mume yupi kati ya James na Kelvin atakuwa amempa ahueni kwa matatizo yake na pia atakuwa alikuwa anamsikiliza?

Mariam: Kazi yangu ni ngumu sana hadi nakosa muda wa kupumzika!
James: Kwa nini usiache hiyo kazi na tafuta kazi nyingine ambayo utakuwa na muda.
Kelvin: Ooh! Pole sana inaonekana leo ulikuwa na siku ngumu sana mke wangu!

Mariamu: Yaani siamini nimeshindwa kumpigia simu Shangazi leo!
James: Usihofu atakuelewa, si anajua upo busy.
Kelvin: Ooh Pole sana mke wangu, unajua kupenda wewe ndo maana nakupenda!

Mariamu: Unajua shangazi ana mapito magumu sana so ananihitaji kuongea naye:
James: Una wasiwasi mno na wewe, kwa nini unajisumbua wakati upo busy na kazi yako.
Kelvin: Pole sana najua leo umechoka, sogea basi nikukumbatie nimekumis sana leo.
(Mariam na Kelvin wanakumbatiana na Mariam ana relax)

NB: Mariam anakasirika na anamwambia James siku zote hunisikilizi na hunijali.
Pia anamwambia Kelvin:
"Kila siku napenda sana kuongea na wewe, unanifanya kuwa mtu wa furaha, asante sana kwa kunisikiliza, najisikia raha."

Ukweli ni kwamba James alikuwa anasikiliza, lakini kwa lugha ya mwanamke alikuwa hasikilizi kwa kuwa alikuwa anajitahidi kutoa solution kwa yale alikuwa mkewe Mariam anamwambia.
Kwa upande mwingine, Kelvin alikuwa anasikiliza kwa sababu alikuwa anaongea lugha ambayo mwanamke anaielewa na anaitaka na alikuwa anampa kile mwanamke anahitaji.

Je, wewe ni James au Kelvin?

Wednesday, September 10, 2008

Mistakes

If you have made mistakes, even serious ones, there is always another chance for you.
What we call failure is not the falling down, but the staying down.
Mary Pickford

Nimeachwa na Nimeumizwa, nifanyeje?

Binadamu yeyote ameumbwa na asili ya uwezo wa kuponya maumivu au kuumizwa hisia zake.
Kama imetokea umeachwa na mpenzi wako ambaye ulitegemea mnaweza kuwa na maisha ya pamoja baadae usiogope.
Kwanza mshukuru Mungu kwa kuwa amekuacha sasa kuliko kukuacha baada ya kufunga ndoa.
Kitendo cha kuachwa na mchumba au mtu ambaye mlikubaliana kuwa wachumba na hatimaye ndoa kweli huumiza sana.

Wala usiogope maumivu ya kuumizwa na mapenzi, ogopa moyo ambao hauwezi kupenda tena.
Mara nyingi tunapoumizwa katika mapenzi au mahusiano tunapata maumivu makali sana na wengine hushindwa hata kwenda kazini, wengine hushindwa kupata hata usingizi kwa siku kadhaa, wengine huamua kuchukua uamuzi wa hata kupigana na kushitakiana kwa kupotezeana muda hata hivyo ni kwa sababu ya maumivu.
Wengine huweka nadhiri kwamba hawatapenda tena nk.
Kitu cha msingi kwanza ni kukubali (admit) kwamba upo kwenye maumivu na kwamba umeumia.
Hata ufanyeje huwezi kukimbia maumivu kwenye mapenzi, utaendelea kupambana hizi hisia upende usipende.
Ukiumizwa umeumizwa haijalishi utaamua kuwa kama mtoto kuumia na kuachia au kuwa ngangari kwa kubaki na maumivu ndani.

Kitu cha pili baada ya kubali umeumizwa ni kuachilia ile hali kwa kufanyia kazi kama unaweza kulia machozi lia sana kwani kulia machozi huleta relief na kujisia mwepesi then endelea kufurahia na kuona ni jambo la kawaida na pia wewe si mtu wa kwanza kuachwa na kuumizwa kwenye mapenzi.

Haina haja kuanza kukataa kwamba hukupenda au hukuwa katika upendo wa ndani na huyo aliyekuumiza.
Ulimpenda kwa sababu kulikuwa na sababu ya msingi na kitendo cha mahusiano kuharibika hii haina maana kwamba ulipenda vibaya au ulifanya jambo baya.
Kupenda mtu ni process ambayo ilikupasa wewe kuwa mtu anayependa, na hivyohivyo hata kama umeumizwa jambo la msingi ni kuendelea kujipenda mwenyewe na kujiamini kwamba wewe hukufanya kosa lolote na kwamba bado una nafasi kubwa zaidi ya kupata mtu wa kupendana na wewe upya.
Unatakiwa kuvaa positive focus kujipenda au kujikubali mwenyewe na baada ya hapo onesha upendo kwa wengine.
Kumbuka huwezi kupenda mtu then usipate maumivu hakuna kitu kama hicho, unavyopenda zaidi ndivyo mambo yakienda vibaya utapata maumivu makali zaidi.

Maumivu ni sehemu ya urithi wa mapenzi.

Huwezi kumbadilisha mtu mwingine, lakini unaweza kubadilisha jinsi unavyojihusisha na watu wengine.
Huwa Inachukua watu wawili kujenga na kuendeleza mzunguko wa mgogoro, lakini inamchukua mtu mmoja tu kumaliza mgogoro, kwa kufanya mabadiliko ndani yako unaweza kumaliza mgogoro, kuponya maumivu ya kuumizwa na wakati mwingine kurejesha upendo wa kweli kwa yule unayempenda.
Hofu, mashaka, na kukasirishwa huweza kubadilishwa na upendo na ushirikiano na hatimaye unapata suluhisho la tatizo na hatimaye peace of mind.

Una kila kitu kinachoweza kukuwezesha kuponya maumivu ya kuachwa na mpenzi, jiamini.

Tuesday, September 9, 2008

Mwanaume hakwepi, atakuona tu!

Tabasamu hufungua dirisha la Upendo na kujiamini.
(Picha kwa hisani ya Yusta M.) Mungu alituumba wanadamu kwa namna ambayo mwanaume huvutiwa na mwanamke kama sumaku hata hivyo kuna wakati mtu hujikuta nguvu ya jinsi tofauti kuvutwa na yeye inakuwa hakuna.
Hali huwa mbaya zaidi kwa akina dada hasa wale ambao muda wa kuolewa umefika na hakuna dalili ya mwanaume yeyote kuvutiwa naye.

Wanaume hutafuta mwanamke ambaye anavutia, mrembo, anafurahisha kuwa naye pamoja.
Mwanamke ambaye mwanaume hujisikia proud kuwa naye, anayeongea kirahisi bila kulalamika, ambaye anajiamini, anayejifahamu yeye ni nani bila kuyumbishwa na upepo wa aina yoyote.
Lakini kuna mambo matatu muhimu sana kwa mwanamke na yakiwa sehemu ya maisha yake basi mwanaume atafanya kila analoweza kuhakikisha anakuwa ndani katika maisha yake na kumpa chochote anahitaji.

Lengo ni mwanamke kujizoesha yafuatayo kuwa sehemu ya maisha yake na hatimaye mwanaume kuvutiwa naye.

Mwanamke mwenye tabasamu
Hii ni silaha yenye nguvu na ya uhakika kwa mwanamke.
Mwanamke mwenye tabasamu anarahisisha kwa mwanaume kumuona ni mwenye kujiamini na mchangamfu.
Wanawake wengi huwa na woga jinsi ya kuonekana mbele ya mwanaume na matokeo yake hubania tabasamu, kitu ambacho hupunguza attraction kwa mwanaume.
Pia tabasamu ni alama ya kukubaliwa, wanaume mara nyingi huhitaji message inayompa usalama kwamba mwanamke anaye kutana naye kuna usalama hata kabla hajajitambulisha.

Mwanamke anayeongea na kusikiliza bila kuwa ndo muongeaji (dominate)
Wanaume nao hupenda kusikilizwa, mwanaume huhitaji mwanamke ambaye anachonga sana na yeye kuishia kuwa msilikizaji tu.
Wanaume wengi ni kweli huwa wanategemea mwanamke kuwa mwongeaji pia hawako tayari kuwa wasikilizaji tu.
Mwanamke anayeongea na kusikiliza bila kung’ang’ania kuongea mwenyewe tu wanaume huwafurahia sana na hapo uwezekano wa kuolewa naye huongezeka.

Mwanamke anayevaa kimwanamke
Tunafahamu kwamba wanaume huvutiwa na vile wanaona (visual). Wanawake pia hujisahau kwamba wanaume huvutiwa na wakati mwingine kuchanganyikiwa kabisa na vile mwanamke unaonekana kwa nje kuanzia mavazi.
Kama unataka kuonwa na wanaume Hakikisha unajua na kupanga vizuri utoke vipi kwa pamba zako.
Kwa kadri mwanamke anavyovaa nguo soft (feminine) ndipo wanaume huwezi kumuona, hapa nina maana kuvaa kama mwanamke.

Monday, September 8, 2008

Wanaume na kushauriwa!

Hata mwanaume anapoendesha gari tu, mwanamke inabidi kuwa makini unatoa ushauri baada ya kuombwa na yeye au unatoa tu kwa sababu unampenda?
Je, utajibiwa au mzee anaamua kula jiwe na kuumiza hisia zako? Ilitokea siku moja Mzee Mlyabange na Mkewe Tuladzuma walikuwa wanaendesha gari lao kuelekea kwenye sherehe za harusi posta mpya jijini DSM.
Mzee Mlyabange ndiye alikuwa anaendesha gari.
Wakati wanadhani wamefika eneo la sherehe ilidhihirika kwamba ni dhahiri walikuwa wamepotea njia.
Mara moja Mkewe Tuladzuma akamshauri mumewe waombe msaada kwa watu wawaelekeze jengo sahihi na sehemu sahihi ya sherehe, maajabu mumewe alijibakia kimya bila kuongea wala kujibu chochote.
Mzee Mlyabange aliendelea kuendesha huku anatafuta jengo hadi alifanikiwa kufika na kupata jengo sahihi la sherehe.

Kihisia mkewe Tuladzuma aliumia sana hasa kwa kitendo cha mumewe kubaki kimya na kuonesha kutomsikiliza na kumjali pale alikuwa anamshauri watafute msaada kuulizia njia na jengo sahihi.

Kwa upande wa mke wake (Tuladzuma) kitendo cha kutoa ushauri kwa mumewe ni kuonesha anampenda ndiyo maana alimshauri watafute msaada kwa watu wengine.
Na Mzee Mlyabange kwa upande wake alikuwa amekwazika sana na kitendo cha mkewe kumshauri kwani mzee alihisi kama vile mke wake hamuamini na hatamfikisha kwenye sherehe. Kwake haukuwa ushauri bali Dharau na kuelezea kwamba mwanaume hawezi.

Tofauti kubwa iliyopo kati ya wanawake na wanaume ni kwamba wanaume huwa hawapendi kupewa ushauri au kushauri mtu hadi wao wenyewe waombe.
Pia wanaume wana asili ya kujitatulia Matatizo yao wenyewe (kama kwenda pangoni) isipokuwa aombe mwenyewe.
Mkewe Tuladzuma hakujua kwamba kitendo cha mumewe kupotea njia hakikumaanisha apewe ushauri bali atiwe moyo na support kwamba atapata njia na kuonesha kumpenda zaidi.

Ukweli ni kwamba mwanamke katika ndoa au mahusiano anapoamua kutoa ushauri ambao hajaombwa (unsolicited) au kujaribu kusaidia kiushauri mwanaume bila kuombwa huwa hajui ni kiasi gani huwa inachukiza sana mwanaume na matokeo yake unaweza kuona mwanaume anakujibu kwa mkato au mwanaume anakula jiwe na kukuacha umeumia hisia zako.

Unapomshauri mwanaume kwa jambo dogo kama kuendesha gari na kupotea njia mwanaume hujiona kama vile umemdharau kwa jambo dogo sana je jambo kubwa utamuamini?

Tangu kale wanaume ni mafundi, ni wataalamu, ni heros, ni mashujaa, ni experts, ni watatuzi wa Matatizo sasa unapompa ushauri bila kuombwa ni kama unamfanya yeye hana lolote.

Naamini jambo la msingi ni wewe mwanamke kusoma saikolojia za mume wako na jinsi ambavyo huwa anaitikia ushauri wako, kwani kuna wakati unatakiwa kumtia moyo na kuonesha upendo kuliko kushauri au kulalamika tu kwamba hajaweza kufanya hiki na kile.

Pia kumbuka mwanaume kujiamini kwingi hutokana na mafanikio anayopata kutokana na ufanisi, uwezo na taaluma yake na kitendo cha kumshusha humuumiza sana.
Pia wanaume huwa hawapendi kuongelea kuhusu Matatizo yao hadi yeye mwenyewe akueleze na pia hupenda kutatua Matatizo kivyao kwani huamini kwamba likitokea tatizo lazima yeye ndiye atoe solution.

Sunday, September 7, 2008

Jumapili Njema

Kuwa na hofu ya Mungu ni jambo la msingi ili kuweza kuishi maisha safi na kuwa watu wazuri katika jamii zetu. Je, ukiitwa leo mbele ya haki una uhakika utawekwa mahali pema peponi? Usisubiri kiongozi wako wa dini akupe sala inayokuhakikishia utaenda mahali pema peponi, anayeweza kukuhakikishia ni wewe mwenyewe unavyoishi sasa.

Sikiliza kwa makini maneno ya wimbo huu kutoka kwa Kwaya ya Mamajusi - Majengo Moshi Tanzania.

Nakutakia Jumapili njema

Mungu akubariki sana!

Tukikimbilia pangoni tuache!

Wengine mnaiga, wanaume ndo wanajua siri ya kukimbilia mapangoni wakipatwa na shida au matatizo ya msongo wa mawazo na wakitoka huko wanakuwa bomba sana. Moja ya tofauti kubwa kati ya wanaume na wanawake ni jinsi ya kukabiliana na msongo wa mawazo.
Mwanaume akiwa na msongo wa mawazo hujitenga, huwa mwenyewe na huwa mkimya na hataki kuguswa wala kuongeleshwa na mtu yeyote, wakati mwanamke hujisikia kuogopa na kuathirika kihisia.
Mwanaume hujisikia ahueni atakaposhughulikia tatizo lake yeye mwenyewe bila kuhitaji msaada wakati mwanamke hujisikia ahueni pale atakapokuwa anazungumza au kuongea kuhusu Matatizo yake na mtu mwingine anaweza kuwa mume wake au mtu yeyote anayemwamini.
Mwanaume akipata msongo wa mawazo iwe kukasirishwa kazini, au Matatizo yoyote hujitenga na kwenda kwenye pango (cave) lake katika akili zake ili kuendelea kupambana na kupata solution ya tatizo lake peke yake.
Huwa anakuwa anajihusisha zaidi na kushughulikia tatizo lake na kuwa kama vile amepoteza uwezo wa kutoa ushirikiano kwa mke au mpenzi wake kwa zaidi ya asilimia 95.
Hujitenga, huwa mbali kimawazo, huwa kama amejisahau kwamba ana mke ambaye anahitaji kumsikiliza.
Anakuwa yupo kimwili na si kiakili kwani asilimia 95 zinakuwa kwenye kushughulika na tatizo lake.
Akiwa katika hali ya msongo wa mawazo inakuwa ngumu sana kumpa mwanamke attention kubwa na hisia ambazo mwanamke anastahili.
Na ikiwa atapata solution kwa tatizo lake basi haraka sana atatoka kwenye pango lake ambapo alikuwa amejificha na kurudisha ushirikiano kwa mke au partner wake kama kawaida.
Na kama hatapata majibu ya Matatizo yake basi anaweza kukwama huko kwenye cave lake kwa muda mrefu zaidi.
Wakati mwingine ili wasikae muda mrefu kwenye pango utaona wanaume wanapenda sana kusoma magazeti, kuangalia news kwenye TV, kufanya mazoezi nk.

Kwa mfano!
Mzee Mlyabange na mkewe Tuladzuma wote wamerudi nyumbani hoi wakiwa na msongo wa mawazo baada ya mabosi wao kuwakasirisha huko kazini.
Baada ya kufika nyumbani Mzee Mlyabange anaamua kupoteza mawazo yake kwa kujisomea gazeti la Kilimo cha kisasa na hataki kabisa kusumbuliwa na mtu kwani bado anatafakari jinsi ya kupata solution baada ya bosi kumkasirisha kazini.
Wakati huohuo mkewe naye (Tuladzuma) baada ya kurudi home huku amechoka na kelele za bosi anataka kuongea na mumewe Mlyabange ili kupata ahueni ya visa vya bosi.
Hii ina maana kwamba Mzee Mlyabange baada ya kutatizwa na bosi ameamua kukimbilia kwenye cave lake hataki kuongeleshwa na mtu na wakati huohuo na mke wake naye (Tuladzuma) anataka kusikilizwa na mumewe kwani bosi naye kamjeruhi.
Bila shaka kila mmoja akiamua kufanya kile anataka hata kama wanapenda sana bado kutakuwa na zogo na kukwazana ajabu.
Mzee Mlyabange atadhani mkewe Tuladzuma anachonga sana na hataki kumpa muda, na Mke naye atamuona mzee hamjali na hataki kumsikiliza.

Hili ni tatizo la mahusiano mengi na ili kutatua tatizo hili haitategemea ni kiasi gani Mr. Mlyabange anampenda kiasi gani mkewe Tuladzuma bali ni kuhusiana na uelewa wao wa tofauti zilizopo kati ya mwanaume na mwanamke na jinsi ya kumpa mwenzake kile anastahili.
Mwanaume akipatwa na msongo wa mawazo au tatizo, kama wewe ni mwanamke kwanza utajua tu hasa jinsi anavyojiweka kivyake na hata ukimuuliza je, unatatizo lolote?
Bila shaka jibu utakalopata mwanaume atakwambia hakuna shida nipo safi tu na pia atakwambia shida yake haikuhusu wala usijali
(hata kama ni usiku wa manane usingizi hana bado atakwambia hakuna shida yoyote hapo hua jamaa yupo pangoni usimsumbue)
Ujue hapo yupo kwenye pango (cave) anahitaji muda wake mwenyewe ili ashughulikie tatizo lake.
Kuendelea kumsemesha ni sawa na kuendelea kumfuata kwenye cave lake na matokeo unaweza kuliwa au kuumizwa na nyoka anayelinda cave lake (hasira, matusi, kupigwa, kutokujibiwa chochote au kuvurugana kabisa)
Kitu cha msingi kama ni mwanamke ukishaona dalili za kuwa jamaa ameenda pangoni wewe ni kuachana naye, fanya vitu vingine kujipa raha zako mwenyewe ndipo utashangaa jamaa katumia muda kidogo kukaa huko mapangoni.

Kumchungulia mwanaume pangoni au kumfuata pangoni na hata kuendelea kumsemesha akiwa pangoni hakumfanyi awahi kutoka pangoni, bali kunaweza kusababisha akwame huko na kubaki huko kwa muda mrefu zaidi. Dawa ni kumpa muda wa kutosha na kuachana naye kabisa hadi amalize muda wake na atarudi mwenyewe.

Saturday, September 6, 2008

Mzee Jongwe na mabaluni yake, yakipasuka hana lake tena! Life is too short to wake up with regrets.
So love the people who treat you right.
Forget about the one's who don't.
Believe everything happens for a reason.
If you get a second chance, grab it with both hands.
If it changes your life, let it.
Nobody said life would be easy, they just promised it would be worth it.
Friends are like balloons; once you let them go, you can't get them back.
So I'm gonna tie you to my heart so I never lose you.

Si upendo tu bali kuelewa tofauti

Hata kama mwanaume na mwanamke wanapendana sana bila kujua tofauti zilizopo kati ya mwanaume na mwanamke bado migongano haiwezi kukwepeka. Wakati mwingine migongano inayotokea katika ndoa au mahusiano si kwa sababu wahusika wamepoteza upendo wa kweli baina yao bali ni kutofahamu tofauti iliyopo kati ya mwanaume na mwanamke.
Yaani wengi (si wote) hugombana, huzira, huumia, hukasirikiana, kukwazana na wakati mwingine kuzipiga si kwa sababu hatupendani bali hatufahamu tofauti kubwa zilizopo kati ya mwanamke na mwanaume.

Kwa nini mwanaume akipatwa na tatizo au shida au msongo wa mawazo huwa mkimya na kutotaka kuongea na mtu hata mpenzi wake?


Kwa nini njia nzuri kwake kujisikia relief (ahueni) ni kutoongea na wakati mwingine huamua kusoma gazeti au kuangalia TV au kutulia kimya peke yake?


Na je, kwa nini hata mke (au mpenzi wake) au mtu yeyote akiaanza kumuongelesha bado jibu analopata ni kwamba hata tatizo na anasema niache mwenyewe, wakati huohuo unajua kabisa huyu ana kitu kinamuumiza kwenye akili yake?

Je, unapomuongelesha unakuwa unamsaidia au ndo unazidi kumsumbua na kufanya awe mkali zaidi?

Kabla ya kupata majibu ya maswali hayo hebu tuanza kwa kuangalia tofauti za kawaida zilizopo kati ya wanawake na wanaume.

Wanawake hupenda kuongelea kuhusu watu, wakati wanaume hupenda kuongelea kuhusu vitu. Ndiyo maana umbeya mwingi hupatikana kwa wanawake kuliko wanaume (si wote).
Wanawake ni waongeaji wazuri faragha, wakati wanaume ni waongeaji wazuri mbele za watu. Ndiyo maana mara nyingi kwenye halaiki wanaume ndo videdea wa kuchonga.
Wanawake wanalia machozi mara tano zaidi ya wanaume, ndiyo maana ukiona mwanaume (si wote) anatoa chozi ujue leo yamemfika.

Wanawake ni wepesi kuomba msaada hasa wakipotea njia, wakati wanaume ni wagumu sana kuomba msaada wakipotea njia.
Wanawake huathiriwa sana na kuguswa na harufu, wakati wanaume huathiriwa sana na kile wanaona kwa macho.
Wanawake tangu mtoto mdogo huwa na uwezo wa kuongea huku anakuangalia machoni au usoni wakati wanaume huchelewa sana kuwa na hii sifa.
Wanawake huathiriwa sana na watu wengine, wakati wanaume hujiangalia yeye mwenyewe kwanza.
Wanaume (si wote) ni waongo kuliko wanawake.

Tutaendelea na kuangalia tofauti zilizopo!