"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, September 12, 2008

Akiiva na Kuwa Tayari - Rahisi

Wanawake ni kama mwezi na wanaume ni kama juaWanawake ni mfano wa mwezi (moon) katika mwitikio na uzoefu wa tendo la ndoa.
Wakati mwingine bila kujali ana mwenzi anayejua mapenzi (mwanaume) kiasi gani, anaandaliwa (foreplay) na kuwa hot kiasi gani au kuwa wet south pole kiasi gani, bado anaweza asifike kileleni wakati wa tendo la ndoa.
Si kwamba tu hawezi kufika kileleni, bali hitaji kufika kileleni.

Katika siku 28 za mzunguko wa siku za mwanamke, kuna siku akiwa
AMEIVA NA KUWA TAYARI
basi hupenda na kutaka afike kileleni.

Na siku zingine katika mzunguko hupenda tu kufanya tendo la ndoa kwa ajili ya kuwa close na mume wake na wala hajali kufika kileleni au kutofika.
Wakati mwingine anakuwa katika mzunguko ambao ni full moon, wakati mwingine ni half moon na wakati mwingine ni new moon katika stages zote hizo utendaji huwa tofauti ingawa anaweza kuwa na hamu ya sex na mumewe ingawa si lazima kufika kileleni na anajisikia raha na furaha kuwa hivyo.

Kwa upande mwingine, wanaume mwitikio wao ni mfano kwenye sex ni mfano wa jua kwa maana kwamba kila asubuhi huchomoza na smile la nguvu.
Hakuna nusu jua wala robo jua wala jua jipya kila siku ni jua lilelile na akisisimuliwa tu kimapenzi kileleni atafika tu.
Mwanaume akisisimuliwa, mwili wake automatically hutamani kufika kileleni na hawezi Kukosa hata kimoja.
Na hapa ndipo mwanaume huwa kwenye giza nene kutojua kwa nini mamsapu wake wala hajali kufika kileleni, na anaweza kufika mbali kwa kudhani kwamba kuna mushkeli.

Tatizo kubwa ni kwamba wanaume hupima uwezo na mafanikio ya tendo la ndoa kwa mwanamke kufika kileleni.
Kumlazimisha mwanamke kufika kileleni kila kukiwa na tendo la ndoa huweza kusababisha mwanamke kujisikia haridhiki kwani inabidi wakati mwingine adanganye (fake orgasm) amefika kumbe wala na yeye alitaka sex just to feel close.

Tendo la ndoa tamu ni lile ambalo huacha hisia na kumbukumbu bila kusahaulika na wakati mwingine hufanywa kwa hiari bila kulazimisha mwanamke kufika kileleni, pia kuruhusu kila partner kupata kile anataka kwa mume kufika kileleni na mwanamke kama hana au ana mood kuweza kufika kileleni na zaidi apate physical affection.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kweli ni kitu cha ajabu sana ya kwamba Mungu alituumba binadamu tofauti. Lakini mimi nia swali sasa zile ndoa ambazo ni jinsia moja inakuwa kuwaje kama mwanamke ni mwezi na mwanaume ni jua. siku njema

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta!
Asante kwa swali zuri.
Kwa upande wangu naamini ndoa za jinsia moja ni kinyume na Neno la Mungu na ni laana na sina majibu na huwa sina mpango wa kujifunza lolote zaidi ya kwamba ni ukengeufu na dhambi mbele za Mungu.
Ndoa ni mume na mke ambao wanakubali kuishi pamoja kwa agano na Mungu.

Sina majibu zadi ya hayo.
Ubarikiwe na Bwana

Anonymous said...

Tukubaliane Mungu alituumba Na kutufanya mwili mmoja ili Tucheze,Tuoge,Tulale Pia tufurahie miili yetu pamoja.Tendo la ndoa lina umuhimu Kama kulachakula,kulala,kufanya mazoezi NK.Tofauti ni ugumu wa kuongelea masuala hayo ya mapemzi na bibiee na pia kuhusu hisia za kila mmojawapo- MSAFIRI