"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, September 23, 2008

Bei ya Ndoa

Mpaka kifo kitakapotutenganisha! Kama upo kwenye ndoa na upo kwenye tatizo kubwa, shida au mgogoro wowote na unajisikia kama ni wewe mwenyewe tu mwenye Matatizo ya ndoa, ukweli hupo mwenyewe kwa sababu kutokuwa na Matatizo hakufanyi ndoa kuwa imara bali ndoa huwa imara kwa sababu wanandoa wanajua jinsi ya kupambana na Matatizo kwa pamoja vizuri.

Ndoa imara na zenye afya zinajua jinsi ya kupambana na hali ngumu.
Ni kawaida kila ndoa kukutana na mambo magumu katika safari ya maisha duniani.
Wakati mnaendelea na mahusiano iwe uchumba au ndoa mnaweza kukutana na tuta kubwa la ugonjwa, kuachishwa kazi, kupoteza nyumba, kifo cha mmoja katika familia yenu kama vile wazazi, biashara kuyumba kabisa au kufirisika, hapo utafanyeje?
Tumesikia mara nyingi sana watu wakiwakimbia wapenzi wao au wake zao au waume zao pale moja ya hayo linapotokea.

Ukweli ni kwamba huwezi kujua ndoa yako au uchumba wako ni imara kiasi gani hadi pale utakapojaribiwa.

Matatizo yakitokea mara nyingi huweza kuvunja mahusiano vipande vipande mume huku na mke huko au wachumba kila mmoja kuachana na mwezake.
Lakini habari njema ni kwamba, wanandoa au wachumba ambao wanaweza kupita katika ugumu wowote pamoja kwa kushikamana kama super glue huwa na mahusiano imara yaliyoyoshikamana kwa nguvu za ajabu na kuwa na upendo imara kuliko mwanzo.

Wengi hujiuliza kwa nini hili litokee kwetu tu?
Kwa nini Mungu amenitupa kiasi hiki?


Mary mwalimu wa shule ya msingi huko Njombe anasimulia kwamba mume wake amefirisika biashara yake na baadae wakapata pigo lingine nyumba yao ikaungua moto yote pamoja na mali zote.
Iliwalazima kujihifadhi kwa majirani, hata hivyo anakiri kwamba hakuna wakati wamewahi kuwa karibu na kujisikia kitu kimoja tangu waoane miaka 5 iliyopita, kwao Matatizo yamejenga ndoa yao.

Ndoa si kunywa soda kila siku ukipata kiu, si kuwa na pesa kila siku, ndoa ni kazi, kazi inayohitaji kujitoa, hata hivyo matokeo ya kushirikiana pamoja hasa wakati wa shida kwa kushikamana bila kujali ugumu unaotokea ndoa huwa imara na yenye afya ya ajabu.

Wengine likitokea tatizo kwenye ndoa au uchumba solution ni kuacha na kutafuta mwingine, huo ni ujinga, kila binadamu ana Matatizo yake mapya kabisa na ovyo kabisa.

Jaribu kufikiria kwa nini ulimkubali na kuona anakufaa?


Are you the part of the problem or part of the solution?

3 comments:

Thinker said...

Ndoa sidhani kama mtu anaruhusiwa kuibomboa ,ila huo unao itwa uchumba nadhani kuubomoa inaweza kuwa one of the best solution ili siku usije ukaanza kufikiria kubomoa ndoa. Matatizo ambayo hanatokana na mmoja kati ya wahusika na ambayo yanaweza kuzuiliwa ni vizuri yakachujwa kwenye uchumba. Lakini matatizo ambayo yapo nje ya uwezo wa binandamu yoyote nadhani ni bora watu wakasimama nayo hadi washinde kwani mwisho wake huwa bora haijalishi ni wachumba au wanandoa swala ni kutafuta solution.

Anonymous said...

Nawasalimu kwa jina la bwana, Upo sawa kabisa kaka mbilinyi na pia tukumbuke kuwa kuna kesho jana,leo,kesho na vitu kama hivyo pia kuna kupanda na kushuka cha muhimu tutende yale yampasayo mwanadamu kutenda mbele za mungu. Mbarikiwe nyote leo hii na siku zote pia.
Msafiri

Bwaya said...

Ndoa bila kuhesabu gharama ni hasara tupu.

Migogoro. Kuvunjika kwa ndoa. Watoto wa mitaani. Ni matokeo ya kutokuwapo na hesabu za gharama halisi kabla ya kuingia katika ndoa.

Asante kwa maelezo murua.