"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, September 19, 2008

Kifungua Mimba

Kwa kuwa u kifungua mimba nahisi unaweza kuwa kiongozi mzuri au rais! Emmanuel Lazarus Mbilinyi
Kuna imani nyingi za kweli na za uwongo kuhusiana na mtoto wa kwanza kuzaliwa yaani kufungua mimba.
Pia ni kweli kwamba kwa wazazi, mtoto wa kwanza kuzaliwa awe kike au wa kiume huwa kuna kuwa na uzoefu wa tofauti sana na huleta challenge kubwa mno kwa wazazi.

Watafiti wengi na Wanasaikolojia wengi wana imani kwamba mtoto wa kwanza kuzaliwa huwa na sifa tofauti na watoto wanaofuatia na hata mtoto wa mwisho kuzaliwa yaani kitinda mimba na pia kumekuwa na migongano mingi sana kukubaliana kwamba kifungua mimba huwa tofauti na watoto wengine, wengi wanakataa kabisa na wengine wanakubali.

Zifa zifuatazo huendana sana na mtoto wa kwanza kuzaliwa kama vile kuwa na Akili (intelligence), hii hutokana na kuwa na exposure kubwa na watu wazima tangu akiwa mdogo kitu ambacho humpa uzoefu wa tofauti.

Pia vifungua mimba wanajulikana vizuri sana kuwa na uwezo wa kuongoza au kuwa viongozi labda hii ni kutokana na kupewa jukumu la kuongoza wenzake wanaofuatia tangu akiwa mtoto.
Utafiti unaonesha kwamba marais wengi wa marekani walikuwa ni vifungua mimba katika familia zao.

Pia vifungua mimba wengi ni watu ambao wapo organized ni watu ambao wakipewa project ni moja ya watu ving'ang'anizi huhakikisha wanamaliza.

Utafiti pia unaonesha kwamba vifungua mimba wengi hujiamini sana, hii ni kutokana na wazazi kuwapa support kubwa tangu siku ya kwanza wanapozaliwa.

Kama wewe ni mzazi je, ulijisikiaje ulipopata kifungua mimba wako?

Na kama wewe si kifungua mimba kama mimi je, unaamini haya ni ya kweli?

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mimi siamini kuwa kifungua mimba huwa na akili sana. Na pia sioni tofauti kupata kifungua mimba wa kiume au kike mtoto ni mtoto tu Au nisikataa kabisa kwani kifungua mimba wangu ni wa kike na kitinda mimba wangu ni wakiume. Na mimi mwenyewe si kifungua wala kitinda mimba.Ila hii nimesikia wengi wanapenda hasa Afrika mtoto wa kwanza awe wa kiume. Pia mke akizaa mtoto wa kwanza wa kiume atapendwa na familia nzima na hataachika kiurahisi. Nilivyosikia mimi

Lazarus Mbilinyi said...

Ni Kweli kabisa dada Yasinta mtoto ni mtoto awe wa kike au wa kiume. Pia kuwa kufungua mimba hakuna lolote kwamba eti utakuwa na akili, kujiamini, utendaji mzuri, kuwa kiongozi. Mtoto yeyote katika familia anaweza kuwa watofauti so kuwa kifungua mimba kusikufanye ujione bora, hakuna kitu kama hicho.
Huko India (wahindi) ndo balaa mama ukizaaa mtoto wa kike kifungua mimba ni kasheshe na inafika mahali wanawaua kabisa kisa kifungua mimba ni binti sijui akili zao zipo wapi.
Pia kuna makabila Tanzania (sikumbuki) wanapenda sana kifungua mimba awe wa kiume au lazima katika familia wapate mtoto wa kiume na mwanamke anaweza kuzaa watoto hadi wawe kama team ya netball kama mtoto wa kiume hapatikani, huo ni ulimbukeni kabisa na kupitwa na wakati kwani mtoto ni mtoto
Maoni yangu tu

Anonymous said...

Kaka upo sawa kabisa kwani u sawa asilimia 100 na haupo sawa asilimia 100 pia napenda kusema kuwa kwa wakati huu wa sasa watoto wote ni sawa hata kwa utendaji wao,Nafikiri inatupasa watu wa dunia ya tatu tubadilike na tuache uchildnalism. Msafiri