"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, September 20, 2008

Kitinda Mimba

Eti vitinda mimba wengi hudeka sana? Wataaalamu wa masuala ya haiba na saikolojia ya watu wana mengi ya kusema kuhusu nafasi unayozaliwa katika familia (birth order) na athari zake.
Ukweli ni kwamba watoto kuwa tofauti kitabia hutokana nafasi yako katika kuzaliwa (wa kwanza, katikati au mwisho) ktk familia, aina ya wazazi, idadi ya watoto na wakati mwingine mazingira na malezi.
Kwa mfano ukizaliwa peke yako automatically utakuwa na tabia aidha za kifungua mimba au kitinda mimba.

Kitinda mimba wengi huwa ni watu ambao wanajichanganya sana kwani tangu watoto huwa wanakuwa na hali ya kujihusisha na wengine na si watoto wa kuchungwa sana kama kifungua mimba hivyo huwa na ujasiri wa kufanya jambo lolote hata kama lina risk kubwa.

Pia kitinda mimba huwa na tabia tofauti kwani wazazi huwa hawaelekezi nguvu nyingi kama kifungua mimba (hawako strictly sana) na pia kitinda mimba yeye siku zote hubaki mtoto tu kwani hana mwingine chini yake na kila analosema na kufanya kwa wazazi huhurumiwa kwa kuwa yeye ndo mtoto.

Hawa vitinda mimba mara nyingi hupewa kila wanachohitaji hadi wanakuwa spoiled na matokeo yake huwa wanadeka sana.
Pia hawa huwa hawaogopi maisha kila kitu hukiona rahisi tu hawana shida sana ya kuwaza kwamba maisha ni vita badala yake huona maisha kama zawadi tu ni kuishi.

Je, unahisi kuoa au kuolewa na kitinda mimba huweza kuathiri ndoa kwa kiasi fulani?

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli hata mie nimesikia ya kwamba vitinda mimba huwa vinadekezwa sana. Lakini naweza kusema hii yote inategemea na malezi pia tamaduni.Ni kweli wengine hudekezwa kiasi kwamba wanakuwa wajinga kabisa na wengine kinyume. Huu ni uzoefu wangu.

Fita Lutonja said...

Mimi ni kitinda mimba kwa baba na mama yangu lakini mbona sinatabia kama hiyo, ila kuendekezwakwelinilikuwa ninaendekezwa sana ila kisaikolojia sikijivunia na hilo niliona kama kawaida tu na pindi wanapozidi sana kunisifu nilikuwa najisikia vibaya sana kwani nilikuwa naona kama ndugu zangu ninawatenga ila pamoja na hayo oo hoo!!!!!!!!!!!!!! kumbe sina muda nitakuandikia badae

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka Lutonja,
Ni kweli wazazi hasa wakiwa na watoto zaidi ya watatu mtoto wa mwisho wanamlea tofauti ila kila mtoto huzaliwa na akili na uwezo wake so wakati mwingine hata wazazi unawashangaa wka nini wanakupendelea na kukulemaza.
Mimi ni mtoto wa tatu kwa wazazi wangu lakini Baba alikuwa ananipenda kuliko watoto wake wote na kuna wakati nilikuwa najisikia vibaya kwani kitu wenzangu wameomba amekataa, mimi nikiomba anatoa au kunipa bila tatizo.
Kila mtoto yupo tofauti!