"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, September 15, 2008

Maksi ni zilezile!

Zawadi ni zawadi, muhimu ni Caring anayopata kutoka kwa mwanaume Wanaume wengi (si wote) hudhani kwamba kumpa mwanamke zawadi kubwa, au kumnunulia kitu cha thamani kubwa kama gari au nyumba au kumfanyia jambo kubwa kunampa alama kubwa (maksi) na ni kuonesha mapenzi makubwa na kwamba kwa kufanya hivyo basi mwanamke hastahili kutokuwa na furaha.

Ukweli ni kwamba kila zawadi au jambo unalofanya kwa mwanamke lina nafasi sawa au maksi moja tu kati ya mia, hivyo basi ukimnunulia gari unapata maksi moja, ukimjengea nyumba unapata maksi moja, ukimnunulia pipi unapata maksi moja, ukimbusu unapata maksi moja, ukimsaidia kufua nguo unapata maksi moja, ukimpeleka vacation nje ya nchi unapata maksi moja, ukimkumbatia unapata maksi moja, ukimpa neno la kumtia moyo unapata maksi moja nk.
Ukiongea naye kwa kumsikiliza unapata maksi moja, ukimununulia chocolate unapata maksi moja, ukimnunulia kiatu cha kisasa unapata maksi moja pia.
Kwa mwanamke zawadi zote zina thamani sawa, iwe kubwa au ndogo, kumfanyia vitu vidogo vina thamani sawa na kumfanyia mambo makubwa, hii ina maana kwamba kumpa zawadi kubwa au zawadi ndogo humpa furaha sawa.

Mfano
James ni Daktari kwenye hospitali moja kubwa jijini DSM Tanzania na kazi yake ina pesa nyingi sana kiasi kwamba familia yake imeweza kujenga nyumba, kusomesha watoto, kununua gari na kulipa bills kwa ajili ya mahitaji muhimu ya familia yao.
Daktari James anaamini Mkewe Mariamu anastahili kuwa na furaha kwa sababu fedha anazopata zinawezesha wao kuwa na maisha bora na pia haoni umuhimu wa yeye kusaidia mkewe kazi ndogondogo na kuwepo nyumbani kwa ajili ya kukaa na familia, hivyo wakati mwingie huchelewa nyumbani kuendelea kufanya kazi ili apate pesa nyingi mke afurahi zaidi.

Mkewe Mariamu ni mama wa nyumbani, yeye hufanya kazi za pale nyumbani na zaidi huhakikisha kila kitu pale nyumbani kipo in order.
Mkewe Mariamu analalamika kwamba mumewe kwanza anachelewa nyumbani, pili hasaidii kazi ndogo ndogo za pale nyumbani, hana muda na mumewe anajisikia upweke na anajisikia mumewe hamjali.

Daktari James naye haoni sababu kwa mkewe kulalamika na Kutokuwa na furaha kwani yeye anapata pesa nyingi kuipa support familia na ameshajenga nyumba na kuinunulia familai gari.
Anaamini kuwa na pesa nyingi ni zawadi tosha kwa mke na mke anastahili kuwa na furaha.
Pia James anaamini kuwa anapofanya kazi kubwa ya udaktari na kupata pesa nyingi hastahili kufanya kazi ndogo ndogo pale nyumbani kumsaidia mkewe.

Anaamini pay cheque yake ina point nyingi (maksi 80) kuliko pengine kumsaidia mkewe kutandika kitanda (maksi 1) hajui kwa mwanamke kuwa na pay cheque kubwa kuna maksi moja na kumsaidia kutandika kitanda kuna maksi moja tu.

Unapotaka kumuelewa mwanamke huhitaji kuwa logical bali emotional, mwanamke yupo after romance, jinsi unavyompenda, unavyomsaidia vitu vidogo, unavyomsikiliza, unavyombembeleza, unavyompa muda wa kuwa pamoja na kufurahia, unavyombusu, unavyomkumbatia, unavyomtia moyo, unavyocheza naye nk, kwake ni muhimu kuliko kununua gari au nyumba na kuamini kwamba hapo mwanamke atakuwa na furaha na hana sababu ya Kutokuwa na furaha.
Unaruhusiwa kumfanyia mambo makubwa sana lakini kumbuka anza kwa kumfanyia mambo madogomadogo kwanza.

Kwa kuwa umefanya mambo makubwa haina maana kwamba hutakiwi kufanya mambo madogo na kwamba mambo makubwa au zawadi kubwakubwa ukimpa hana sababu ya Kutokuwa na furaha na kuona unamjali.

6 comments:

Fikirikwanza said...

Hallo naona pilipili za leo hata ukiziweka nyingi hazikolee kabisa. Mimi nilifikiri utazungumzia kupeana zawadi lakini hili swala la zawadi kwa wanawake naona linaweza lisiwe sahihi sana. Wote tunapenda zawadi na wote tunapenda kufanyiwa mambo madogo ambayo pengine tunajua tungeyafanya wenyewe. Kunamambo ambayo wanawake ukiwafanyia ni kweli wanakupa maksi moja pengine zero. lakini kuna mambo ambayo wao wanayujua kuwa ukiwafanyia ni maksi 100%. Na hili ndilo limefanya wanaume wayapuuze mambo madogo kwani hata wao ukiwafanyia mambo makubwa watakupongeza tofauti na ukiwafanyia madogo. Najua kuvua kiatu na koti ni wajibu wa kila mwuza mkaa lakini imagine huyu mwuza mkaa anafika home anakaribishwa vizuri na mrembo wake kwa heshima,busu la furaha,kufumba na kufumbua koti halioni ,soksi,viatu vimesha vuliwa ,lugha nyororo nk. Unafikiri huyu mwuza mkaa kesho atasahau kutandika kitanda chake au kutafuta chochote kile ili walau mrembo wake aone uwepo wake?. Nafikiri hivi vitu ni sychrone au bidirection kwamba tukitaka kufanyiwa tufanye kwanza kwa wao tunao taka watufanyie?.

Anonymous said...

Kaka upo sawa, Napenda kusema kuwa kujali ni kuguswa na kitu.Kama mke hajakugusa moyoni utaona kuwa ni kawaida tu kila siku. Lakini kama yu ubavuni mwako tujamtenda hata siku moja kwani moyo wako utauma. Mbarikiwe na Siku hii njema, Msafiri

Lazarus Mbilinyi said...

Fikirikwanza,
Asante sana kwa maelezo mazuri na yanayoonesha uzoefu wako. Kama ungekuwa umekaa kwenye ndoa angalau miaka miwili tu najua maelezo yako yangebadilika kidogo kwani hakuna kitu kigumu kama kumjua mwanamke anataka nini kwenye ndoa na usipojifunza kwa juhudi tofaut zilizopo kati ya mwanamke na mwanaume unaweza kufanya mambo mwakubwa (yenye maksi 100) na bado mwanamke akakakwambia humsikilizi na humjali na ni mpweke pale tu ukifanya hayo mambo makubwa bila kuwa na mawasiliano mazuri, bila kuwa na muda wa pamoja (quality time) na yeye bila kumtimizia primary emotions zake. Kwa mwanamke kutimiza mahitaji ya hisia zake (emotions tank) ni muhimu kuliko mizawadi mikubwa hata kama atakushukuru kwa kukupigia magoti.
Vitu vidogovidogo kwa wanawake ni muhimu sana na kabla hujampa kitu kikubwa onyesha upendo kwanza then ni kweli itakuwa mia kwa mia.
Huwa haina maana sana kwa mwanamke umjengea nyumba na ashinded peke yake kwenye hiyo nyumba na wewe hupatikani eti umempa nyumba nzuri hivyo hana haja ya kutokuwa na furaha.
Bottom line ni kwamba mwanamke anakutaka wewe zaidi kuliko vitu tunavyowapa na zawadi zina raha yake hasa zikiwa na upendo, na sisi wanaume kuwa romantic.
Ukule ulaviwona!

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli zawadi si mwanamume au niseme penzi si pesa, penzi ni wewe kuamua kumpenda mwenzako na penzi ni moyo wa mtu. kama alivyosema Fikirikwanza ukitaka kufanyiwa basi mfanyie kwanza mwenzako ili iwe sawa. Kwani inakatisha tamaa kama mmoja tu anamfanyia mwenzake.

Anonymous said...

Fikirikwanza safi sana , naona upo sawa kabisa,Wanaume sometimes wanatulemeza sana ,hadi tunajisahau kabisa .Ni kweli wanaume mara nyingine wanakosea lakini kama wanawake tunao wajibu pia wa kuhakikisha tunasababisha mambo kwenda sawa ,tusiwe watu wa kulala lala ,kulalamika tuu,eti hatupendwi,hatuletewi zawadi ,ni wakati wetu wanawake kujua wajibu wetu na ninaamini tukifanya ipasavyo tutafanyiwa zaidi. Wanaume ukiwapenda sawasawa hawana ujanja ,watakupa kila unacho hitaji na watakupenda tuu.

Fikirikwanza said...

Mr Mbilinyi naona hujeelewa , sijasema kuwa tusijali wanawake na wale sijasema tusiwe na upendo ninacho sema ni jinsi mnavyo ona kuwa haya mambo ni one direction . Naunga mkono na Mr msafiri kwama kama wanawake hawata jibidishe naamini utakuwa vigumu hawa viumbe kutendewa haya mnayo yasema. Ni kweli lakini mke anye kugusa moyoni ni rahisi sana kujitolea kwa ajili yake. Lakini kama tukisisitiza eti wasikilizwe wakati wao hawana mpango wa kusililiza wala kupedwa naamini inaweza kuwa vigumu. Jamii yenu inahitaji ukombozi na huu ukombozi unatakiwa kuwa well balanced . Hivi vitu havitokani tuu na mafundisho aliyo pewa mtu bali vivile vinatokana na mguso anao upata mtu kutoka kwa mwingine.