"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, September 18, 2008

Mama na Mwana!

Vitu vingi ambavyo mtoto wa kiume hujifunza kwanza, hufundishwa na mama yake na hii humfanya mama kuwa mtu wa tofauti kwa mtoto wa kiume. Kwa mtoto wa kiume mama ni mfano wa kuigwa kwa kuwa ndiye anayempa picha kamili kufahamu wanawake wanakuwaje.
Sauti ya kwanza kuisikia na tabasamu la kwanza kulipata hutoka kwa mama yake, na watoto wengi huanza kutamka nena Mama mapema kuliko Baba.

Ni mara nyingi sana kuona watoto wa kiume wakiiga baba zao na kutaka kuwa kama baba zao hata hivyo mama huathiri sana maisha ya mtoto wa kiume katika mahusiano na wasichana (uchumba hadi ndoa).
Kuna msemo kwamba mtoto wa kike huelekeza antenna yake kwa baba na mtoto wa kiume huelekeza antenna yake kwa mama hata hivyo mama huweza kumfundisha vizuri mtoto wa kiume kuwa caring and loving.

Upendo wa mama kwa mtoto wa kiume unavyozidi kuwa strong huwa wanajenga bond ambayo huwezesha mama na mtoto wake wa kiume kushikamana kiasi kwamba ikitokea mtoto wa kiume akapata mchumba au mke mama hujisikia kupungukiwa kitu na hatimaye mama huanza kuingilia ndoa au mahusiano ya mtoto wake.
Hii hutokana na gap la nafasi (upweke) ambayo mtoto wake aliijaza na sasa kahamishia kwa yule anampenda mchumba au mke.
Wakati mwingine hii huenda mbali zaidi kwani wapo watoto wa kiume ambao hata maamuzi yao ndani ya ndoa zao na mahusiano kila kitu huamriwa na mama zao.
Pia hufika mahali kijana wa kiume huweza hata kudai huduma kama zile alikuwa anapata kwa mama yake kama vile vyakula na baadhi ya tabia.

Ukweli unabaki kwamba mtazamo wa ulimwengu kwa mtoto wa kiume huathiriwa zaidi na malezi ya mama.

“Mwanangu, shika maagizo ya baba yako, Wala usiache sheria ya mama yako”
Mithali 6:20

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kwanza napenda kusema asante kwa mafundisho mazuri. Ni kweli kabisa akina mama huwa huingilia kati ndoa za watoto wao wa kiume: Tena imewahi tokea mama anakwenda nyumbani kwa mtoto wake wa kiume na kuanza kuweka utaratibu wakati kijana ameoa, yaani kama kutandika kitanda, kufua ngua na kama ulivyosema chakula yaani hata kumpikia chakula. mmm kazi kweli

Fikirikwanza said...

Hii ni kweli lakini sometimes ni opposite badala ya kuwapenda wao huwafanya ni watu wakujifunzia kuwanyanyasa na kuwapiga. Ndoo maana watoto wengi wa kiume sometimes huwaona baba zao ndoo rafiki wakubwa kuliko mama zao. Japo hujisingizia kuwa wao ndo wanajua kuwaonya watoto wao lakini mara nyingine wanazidisha! vipigo si solution.