"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, September 13, 2008

Miaka 80 ya Ndoa

Frank na Anita Milford wakati wa Aniversary ya miaka 80 ya Ndoa yao Huko Uingereza wanandoa wazee Frank miaka 100 na Anita miaka 99 hivi karibuni waliadhimisha sherehe yao ya kumbukumbu ya Ndoa Kutimiza miaka 80


Walikutana mwaka 1926 na kuoana tarehe 26 Mei 1928, wamebarikiwa kuwa na watoto wawili, wajukuu watano na vitukuu saba
(Kweli familia za kizungu hawazaliani)


Wao wanakiri kwamba na kushauri kwamba ili ndoa idumu kuna umuhimu wa wanandoa kumaliza tofauti zao kabla ya kwenda kulala kitandani na pia kutumia muda mwingi pamoja.

Pia Malkia wa Uingereza amewatumia zawadi ya kadi ya kuwapongeza wanandoa hawa kutimiza "Oak Annivesary" ya ndoa yao kitu ambacho kutokana na kumbukumbu za kitabu cha Guinness wanandoa waliovunja rekodi nchini Uingereza walifikisha miaka 81.

Nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa mafanikio makubwa kama hayo, naamini ni mfano tosha kwa sisi ambao safari bado bichi kabisa na ndefu maana miaka 80 pamoja si haba milima na mabonde bado ipo mbele.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mmh miaka 80 mbali sana na miaka hii ya leo sijui.lakini lazima itakuwa kazi sana kuwa na miaka yote hii. Swali je lile swala la ndoa wanaweza kweli kulimudu au ndo basi. maana naona wamekula chumvi nyingi kweli.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta, ni kweli ni kazi sana kufikisha miaka 80 ya ndoa pia sema kwa mfano kwetu Tanzania (Africa) watu wanakufa mapema ndo maana huwezi kukuta wazee wenye miaka zaidi ya 100, Hata hivyo naamini kwetu Afrika kuna wengi sana ambao ndoa zao hudumu hadi kifo wakiwa wazee.
Kuhusu hawa wazee kujirusha na tendo la Ndoa (unyumba) naamini kwao si lazima kuwa na penetrative sex kwani hata kutembea kwenyewe wanatumia mikongojo je, shughuli yenyewe wataiweza, si unaambiwa tendo moja la sex hadi kileleni unachoma calories 250 na unakuwa umekimbia Km 8 so tusitegemee kabisa hawa wazee kushinda mbio ya marathon ya sex.
Nahisi wao wakitaka kujirusha ni kushikana shikana na kubusiana na kukumbatiana na kama wanaweza kunyonyana miili yao basi raha na maisha yanaendelea.
Pia naamini hamu ya tendo lenyewe inaweza kuwa imeisha maana homoni zinazohuisika na sex zimepungua sana hivyo hawana libido na wao hawaoni umuhimu kujirusha.
Mawazo yangu tu lakini!
Asante

Anonymous said...

Hahaahahah, Dunia ya leo na vijana wa leoo Sijuiii!!!! Tuombe Mungu atujaalie uzima nasi tufike huko,na tujitunze pia vizuri kwani ndo msingi wa yote Siku njema wapendwa,
Msafiri