"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, September 11, 2008

Mwanamke ni Kusikilizwa!

Mashitaka mengi tunayopata wanaume kutoka kwa wake zetu ni kwamba;
Huwa hatuwasilikizi na pia hatuwajali”

Kumsikiliza mwanamke anapoongea ni pamoja na kuachana na kile ulikuwa unafanya, concentrate kwenye kile anaongea, kusikiliza hisia zake zinaongelea kitu gani na si kile mdomo unaongea tu.

Wanaume tunahitaji kufahamu kwamba wanawake mara nyingi huongelea matatizo yao kwa maana ya kuwa karibu na sisi na kupata ahueni kutokana na matatizo yanayaowapata, si lazima mwanaume kuanza kutoa solution ya matatizo anakwambia.

Kama tulivyosema huko nyuma kwamba mwanamke akipata matatizo hutafuta mtu maalumu wa kuongea naye, kumshirikisha hisia zake na kile kitendo cha kuongea humpa ahueni (relief) hivyo basi mwanaume kazi kubwa ni kumsikiliza na zaidi sana kuhakikisha anafahamu kwamba unamsikiliza.

MFANO
Mariamu anarudi nyumbani akiwa hoi na kazi pamoja na kusumbuliwa na bosi wake.
Anaporudi home anajisikia ni vizuri kuongea na mumewe.
Fikiria Mariam ana wanaume wawili mmoja wa kweli (James) na wa pili ni kwa ajili ya kutufanye tuelewe mfano (Kelvin).
Unadhani ni mume yupi kati ya James na Kelvin atakuwa amempa ahueni kwa matatizo yake na pia atakuwa alikuwa anamsikiliza?

Mariam: Kazi yangu ni ngumu sana hadi nakosa muda wa kupumzika!
James: Kwa nini usiache hiyo kazi na tafuta kazi nyingine ambayo utakuwa na muda.
Kelvin: Ooh! Pole sana inaonekana leo ulikuwa na siku ngumu sana mke wangu!

Mariamu: Yaani siamini nimeshindwa kumpigia simu Shangazi leo!
James: Usihofu atakuelewa, si anajua upo busy.
Kelvin: Ooh Pole sana mke wangu, unajua kupenda wewe ndo maana nakupenda!

Mariamu: Unajua shangazi ana mapito magumu sana so ananihitaji kuongea naye:
James: Una wasiwasi mno na wewe, kwa nini unajisumbua wakati upo busy na kazi yako.
Kelvin: Pole sana najua leo umechoka, sogea basi nikukumbatie nimekumis sana leo.
(Mariam na Kelvin wanakumbatiana na Mariam ana relax)

NB: Mariam anakasirika na anamwambia James siku zote hunisikilizi na hunijali.
Pia anamwambia Kelvin:
"Kila siku napenda sana kuongea na wewe, unanifanya kuwa mtu wa furaha, asante sana kwa kunisikiliza, najisikia raha."

Ukweli ni kwamba James alikuwa anasikiliza, lakini kwa lugha ya mwanamke alikuwa hasikilizi kwa kuwa alikuwa anajitahidi kutoa solution kwa yale alikuwa mkewe Mariam anamwambia.
Kwa upande mwingine, Kelvin alikuwa anasikiliza kwa sababu alikuwa anaongea lugha ambayo mwanamke anaielewa na anaitaka na alikuwa anampa kile mwanamke anahitaji.

Je, wewe ni James au Kelvin?

10 comments:

Anonymous said...

Nimependa hii,Upo sawa kabisa na pia napenda kuwakumbusha wenzangu kuwa kama wewe unarudi nyumbani mapema ni vizuri uwe unamsaidia mama kazi pale nyumbani kabla yeye hajarudi,Pia siku zile ambazo wewe huendi kazini pia saidia mama kazi.Usijali kuitwa mume bwege kwani unatenda mema.
Msafiri.

Yasinta Ngonyani said...

Nimekumbuka mbali sana: Hii huwa inatokea mara nyingi sana. Na mara nyingi wanawake wengi wanasema waume zao ni kama James. Na mara nyini inakuwa hivyo kama alivyofanya Mariam kutafuta akina Kelvin ili kuona naye ni mtu kati ya watu. Asante kwa mfano mzuri

Fikirikwanza said...

Lakini tukubaliane kuwa huu mfano alio toa mwanamke alikuwa anauliza maswali na anasema mambo ya msingi na james alikuwa na makosa . Lakini sometimes hawasilikizwi kwa sababu wanaongea wanayo yajua wao na kitu kimoja ambacho watu wengi hawakijui ni kuwa siku ya kwanza unapo ingea na some one basi hiyo huwa ndoo picha yako kwake kila siku.Of'se wanaume wanapenda kuwasiliza wanawake na wanapenda sana . Lakini hivi wanaume hawapendi kusilikilizwa?

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Asante kwa kuwakilisha maoni ya wanawake wengi kwamba sisi wanaume tunahitaji kuwasilikiza haijalishi unaongea kitu gani.

Nakubaliana na wewe Fikiri kwanza kwamba James kweli alikuwa anajibu sawa na wanaume wengi pia unaposema "wanaongea wanayojua wao na wengi hu-filter ujumbe na kuona kila siku anaongea tu" hapo ndipo mgogoro huanza, wanawake wana lugha zao na wanaume wana lugha zao jambo la msingi ni kufahamu tofauti iliyopo then unafanya kile kinapaswa kufanya ili mwenzi wako na yeye ajisikie kweli mwenzangu ananijali, hata hivyo ndoa ni kujifunza na kukua kila siku, na kazi kubwa ni kusameheana na kutorudia makosa tunafanya na zaidi sana kuhakikisha mwenzako anaridhika na mwenendo mzima wa maisha ya mahusiano.
Love is a decision to serve someone ndiyo maana inahitaji kuweka efforts kila siku kuhakikisha unapalilia ndoa inakuwa na afya njema.
Mbarikiwe kwa michango yenu.

Fikirikwanza said...

Lakini mzee ajue wengi wao wanaume ndoo wanafanya kazi na sometimes qwanarudi wamechoka ,na anafika home anaulizwa mambo ambayo ni pposite kabisa na yaliyomo kichwani mwake. badala ya kuuliza habari za kazini nna kumweka sawa yeye kwanza ndoo yupo na maswali yake anayo yajua. Huoni kama kunauwezekano wa mtu kujibu vibaya kuliko Mr james. Tunamba somo kwa ajili ya hawa warembo ,jinsi wanavyo takiwa kufanya ili waweze kusikilizwa ?.tatizo si wanaume mie naona tatizo wanaaka kufanyiwa vitu bila wa kujaribu kuvifabnya. Mwanauùe ni mwepesi kujifunza kuka kwa mwanamke kuliko mwanamke kujifunza kutoka kwa mwanaume. wasisahau kupiga magoti hadi ardhini wakati wanawasalimie waume zao wakiwa wanatoka kazini??????

Anonymous said...

Fikirikwanza Ni kweli wanaume wengi ndo wanafanya kazi na huwa wanarudi home hoi na wakati mwingine wamejeruhiwa na mabosi wao.
Mwanaume akirudi anataka muda wa kwake, kujitenga na kupata ahueni kwa kuchoka, mwanamke naye anataka kuongea asikilizwa na mumewe ambaye amechoka ajisikia anasikilizwa na kupendwa. Hapo ndo kasheshe huanza, mwanamke anatakiwa kujua mwamba mwanaume akiwa amechoka anahitaji muda wake (kwenda pangoni) kupumzika na kupata ahueni hahitaji kusemeshwa wala kushauriwa maana unamsumbua. Ni vizuri warembo kujua kwamba wanaume wapo tofauti na wao na kwamba si kila wakati unatakiwa kumuongelesha.
Kuhusu wanawake kupiga magoti nahisi huo utamaduni sasa unatoweka kama endangered spicies kwenye animal or plant kingdom.

Lazarus

Yasinta Ngonyani said...

Sasa hapa tunazungumzia Afrika au. Kwani hata hivyo eti mwanaume ndiye anayefanya kazi na anarudi nyumbani kachoka. Je kama mwanamke yupo nyumbani anafanya nini anakaa na kumsubiri mumewe tu au. Hii sio haki kabisa huu ni upendeleo kwani mwanamke kama haendi kazini basi ana kazi ya kutunza nyumb, kulea watoto kupika nk. Ni sawa kabisa na kazi ya siku nzima ofisini tena inaweza kuwa ngumu zaidi. Basi kama hivyo wanaweza kubadili mwanamke abaki nyumbani ana kufanya kazi za nyumbani na mwanamke aende kazini kufanya kazi za "ofisini" Lazima kuwa na usawa.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,
Hata Afrika siku hizi wote wanawake na wanaume tunafanya kazi ofisini. Hivyo suala na mmoja kuwa nyumbani limepitwa na wakati pia hata mwanamke au mwanaume anayekuwa nyumbani naamini huwa anachoka na kazi za nyumbani pia. Point muhimu ni kila mmoja kutambua nini mwenzake anahitaji wakati amechoka, kama ni mwanamke ni kusikilizwa na mumewe na kama ni mwanaume basi ni kupewa muda na mkewe wakati yupo pangoni.
Asante sana kwa maoni yako

Fikirikwanza said...

Sijasema wanawake wakae home wala wanaume wakae ofisini ,nilalo sema ni jinsi ambavyo hivi viumbe vinaweza kusikilizana. Tatizo wanawake wanataka kupendwa hata bila kugharimia.Kuna cost nzuri tuu zisizo zidi uwezo wa mwanamke yoyote ili awaeze kupewe upendo wa kweli na kusikilizwa na huyo mwuza mkaa wake. Lakini wengi wetu tunataka bingo hadi ndani ya ndoa.
Mimi nafikiri lazima wanawake wakubali kulipa gharama ili wapate hivyo wanavyo vihitaji!!!.

Fikirikwanza said...

Hallo nyie naonabado hajanielewa , sijazungumzia mwanamke kukaa nyumbaniau mwanaume na hilo ni juu yao kama wanaona ni bora kupigishana zamu ni juu yao. Ugomvi wangu ni juu ya swala eti wanawake hawasikilizwi. Tatizo wanawake wanataka kusilkilizwa na kupendwa bila kugharimia. Hizi pilipili zina bei yake bwana na ukizitaka hazizidi uwezo wa mwanamke yeyote chini ya jua. Tatizo wanawake wao kila kitu wasipo tendewa wanaona wanaonewa wakati ni jukumu lao kuhakikisha kuwa wanapedwa na wanasikiliswa. Kama mwuza mka wako hakusikilizi tafuta chanzo,rekebisha na ongeza chumvi ya upendo ikiwezekana weka na pilipili kiasi (usizidishe utakuwa ugonvi)!!.
Thank you,stay blessed.