"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, September 9, 2008

Mwanaume hakwepi, atakuona tu!

Tabasamu hufungua dirisha la Upendo na kujiamini.
(Picha kwa hisani ya Yusta M.) Mungu alituumba wanadamu kwa namna ambayo mwanaume huvutiwa na mwanamke kama sumaku hata hivyo kuna wakati mtu hujikuta nguvu ya jinsi tofauti kuvutwa na yeye inakuwa hakuna.
Hali huwa mbaya zaidi kwa akina dada hasa wale ambao muda wa kuolewa umefika na hakuna dalili ya mwanaume yeyote kuvutiwa naye.

Wanaume hutafuta mwanamke ambaye anavutia, mrembo, anafurahisha kuwa naye pamoja.
Mwanamke ambaye mwanaume hujisikia proud kuwa naye, anayeongea kirahisi bila kulalamika, ambaye anajiamini, anayejifahamu yeye ni nani bila kuyumbishwa na upepo wa aina yoyote.
Lakini kuna mambo matatu muhimu sana kwa mwanamke na yakiwa sehemu ya maisha yake basi mwanaume atafanya kila analoweza kuhakikisha anakuwa ndani katika maisha yake na kumpa chochote anahitaji.

Lengo ni mwanamke kujizoesha yafuatayo kuwa sehemu ya maisha yake na hatimaye mwanaume kuvutiwa naye.

Mwanamke mwenye tabasamu
Hii ni silaha yenye nguvu na ya uhakika kwa mwanamke.
Mwanamke mwenye tabasamu anarahisisha kwa mwanaume kumuona ni mwenye kujiamini na mchangamfu.
Wanawake wengi huwa na woga jinsi ya kuonekana mbele ya mwanaume na matokeo yake hubania tabasamu, kitu ambacho hupunguza attraction kwa mwanaume.
Pia tabasamu ni alama ya kukubaliwa, wanaume mara nyingi huhitaji message inayompa usalama kwamba mwanamke anaye kutana naye kuna usalama hata kabla hajajitambulisha.

Mwanamke anayeongea na kusikiliza bila kuwa ndo muongeaji (dominate)
Wanaume nao hupenda kusikilizwa, mwanaume huhitaji mwanamke ambaye anachonga sana na yeye kuishia kuwa msilikizaji tu.
Wanaume wengi ni kweli huwa wanategemea mwanamke kuwa mwongeaji pia hawako tayari kuwa wasikilizaji tu.
Mwanamke anayeongea na kusikiliza bila kung’ang’ania kuongea mwenyewe tu wanaume huwafurahia sana na hapo uwezekano wa kuolewa naye huongezeka.

Mwanamke anayevaa kimwanamke
Tunafahamu kwamba wanaume huvutiwa na vile wanaona (visual). Wanawake pia hujisahau kwamba wanaume huvutiwa na wakati mwingine kuchanganyikiwa kabisa na vile mwanamke unaonekana kwa nje kuanzia mavazi.
Kama unataka kuonwa na wanaume Hakikisha unajua na kupanga vizuri utoke vipi kwa pamba zako.
Kwa kadri mwanamke anavyovaa nguo soft (feminine) ndipo wanaume huwezi kumuona, hapa nina maana kuvaa kama mwanamke.

9 comments:

Anonymous said...

Kaka Hapo sawa kabisaaaaaa Ila napenda kusema kuwa Kila shetani na Mbuyu wake na kama wewe unasema wa nini kuna watu wanasema Nitampata lini? Kitendawili jamaniiii
Msafiri

Yasinta Ngonyani said...

mimi nilikuwa nadhani mwanamke si sura/uzuri mwanamke ni tabia. Unajua pia nimesikia wimbo wa Remmy Ongala anasema ukitaka kuoa oa mke mbaya kwani ukioa mke mzuri kila siku utakuwa ugomvi ndani ya nyumba kila mtu atasema mi mzuri na mwingi atasema hata mi mzuri. Kwa hiyo afadhali kuoa/kuolewa na mke/mume mbaya au wote muwe wazuri. kuzuia ugomvi.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,
Ni kweli mwanamke ni tabia si sura na pia kwa uelewa wangu nahisi hakuna mwanamke mbaya sura kwani wewe unaweza kuona sura ya mwanamke fulani ni mbaya lakini mwanaume mwenzako ndo anaona hakuna mwanamke mzuri kama huyo.
Pia hata wenye sura mbaya(kama wapo) ni vizuri kuwa na tabasamu, kuwa makini na kuongea na kusikiliza na pia kuvaa inavyostahili ili aonekana ni mwanamke anayevutia.
Ni kweli tabia ni pamoja na mwonekano.
Mambo ya mapenzi wakati mwingine huchanganya sana ila kwa yote MKE MWEMA HUTOKA KWA BWANA"

Ubarikiwe

Yasinta Ngonyani said...

unaposema inabidi avae mavazi yanayostahili una maana gani. Halafu umesema mwanaume yeye haoni mwanamke ana sura mbaya je na mwanamke hivyohivyo au.

Anonymous said...

Asante kaka mbilinyi kwa ujumbe mzuri.mungu akutie nguvu.

Anonymous said...

usengwile sana kaka Mungu akutie nguvu.

Lazarus Mbilinyi said...

Nami nawashukuru kwa kupita hapa na kupata chochote unaona kinafaa kuimarisha mahusiano yako na yule umpendaye.
Kama una swali, ushauri, hoja na mchango wowote basi usisite nitumie ili tujifunze na kukua na hatimaye maisha kuwa bora.

mbarikiwa mno

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta Asante kwa swali zuri.

Kuhusu mavazi naamini wewe ndo unaweza kuwa una hisia zaidi huwa unajisikia vizuri au unajisikia ni mwanamke unapovaa mavazi yapi?
Hapa nazungumzia mavazi ambayo ni ya kimwanamke zaidi kuliko yale ambayo wanaume na wanawake wote tunavaa (si muhimu sana) ila wanaume huvutiwa na mwanamke ambaye anaonesha u-feminine.
Kuhusu sura naamini ni kweli wanaume na wanawake wote sawa tu ndiyo maana utakuta kila mwanamke anampenda mwanaume fulani hata kama wanawake wengine wanasema mwanaume hana sura pia kila mwanamke ana ladha yake anataka mwanaume awe.

Fikirikwanza said...

Hallo ,nyie naona mnazivamia pilipili ambazo hamjajua kuzila vizuri. Japo ni kweli lakini kuna vitu ambavyo watu wamejaribu lakini wanaume hawakuridhika kamwe. lipsick zimepanda soko lakini bado hii kitu relation bado complex kama nini.