"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, September 10, 2008

Nimeachwa na Nimeumizwa, nifanyeje?

Binadamu yeyote ameumbwa na asili ya uwezo wa kuponya maumivu au kuumizwa hisia zake.
Kama imetokea umeachwa na mpenzi wako ambaye ulitegemea mnaweza kuwa na maisha ya pamoja baadae usiogope.
Kwanza mshukuru Mungu kwa kuwa amekuacha sasa kuliko kukuacha baada ya kufunga ndoa.
Kitendo cha kuachwa na mchumba au mtu ambaye mlikubaliana kuwa wachumba na hatimaye ndoa kweli huumiza sana.

Wala usiogope maumivu ya kuumizwa na mapenzi, ogopa moyo ambao hauwezi kupenda tena.
Mara nyingi tunapoumizwa katika mapenzi au mahusiano tunapata maumivu makali sana na wengine hushindwa hata kwenda kazini, wengine hushindwa kupata hata usingizi kwa siku kadhaa, wengine huamua kuchukua uamuzi wa hata kupigana na kushitakiana kwa kupotezeana muda hata hivyo ni kwa sababu ya maumivu.
Wengine huweka nadhiri kwamba hawatapenda tena nk.
Kitu cha msingi kwanza ni kukubali (admit) kwamba upo kwenye maumivu na kwamba umeumia.
Hata ufanyeje huwezi kukimbia maumivu kwenye mapenzi, utaendelea kupambana hizi hisia upende usipende.
Ukiumizwa umeumizwa haijalishi utaamua kuwa kama mtoto kuumia na kuachia au kuwa ngangari kwa kubaki na maumivu ndani.

Kitu cha pili baada ya kubali umeumizwa ni kuachilia ile hali kwa kufanyia kazi kama unaweza kulia machozi lia sana kwani kulia machozi huleta relief na kujisia mwepesi then endelea kufurahia na kuona ni jambo la kawaida na pia wewe si mtu wa kwanza kuachwa na kuumizwa kwenye mapenzi.

Haina haja kuanza kukataa kwamba hukupenda au hukuwa katika upendo wa ndani na huyo aliyekuumiza.
Ulimpenda kwa sababu kulikuwa na sababu ya msingi na kitendo cha mahusiano kuharibika hii haina maana kwamba ulipenda vibaya au ulifanya jambo baya.
Kupenda mtu ni process ambayo ilikupasa wewe kuwa mtu anayependa, na hivyohivyo hata kama umeumizwa jambo la msingi ni kuendelea kujipenda mwenyewe na kujiamini kwamba wewe hukufanya kosa lolote na kwamba bado una nafasi kubwa zaidi ya kupata mtu wa kupendana na wewe upya.
Unatakiwa kuvaa positive focus kujipenda au kujikubali mwenyewe na baada ya hapo onesha upendo kwa wengine.
Kumbuka huwezi kupenda mtu then usipate maumivu hakuna kitu kama hicho, unavyopenda zaidi ndivyo mambo yakienda vibaya utapata maumivu makali zaidi.

Maumivu ni sehemu ya urithi wa mapenzi.

Huwezi kumbadilisha mtu mwingine, lakini unaweza kubadilisha jinsi unavyojihusisha na watu wengine.
Huwa Inachukua watu wawili kujenga na kuendeleza mzunguko wa mgogoro, lakini inamchukua mtu mmoja tu kumaliza mgogoro, kwa kufanya mabadiliko ndani yako unaweza kumaliza mgogoro, kuponya maumivu ya kuumizwa na wakati mwingine kurejesha upendo wa kweli kwa yule unayempenda.
Hofu, mashaka, na kukasirishwa huweza kubadilishwa na upendo na ushirikiano na hatimaye unapata suluhisho la tatizo na hatimaye peace of mind.

Una kila kitu kinachoweza kukuwezesha kuponya maumivu ya kuachwa na mpenzi, jiamini.

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ndiyo, lakini kama si mshichana ambaye ameachwa na sio mvulana ambaye ameachwa. Isipokuwa ni familia imeamua ninyi msiwe pamoja je ni sawasawa. Kwani mimi nina rafiki ambaye ana mchumba wake ambaye walipendana sana na bado wanapendana na huyo kija mpaka leo kwa maumivu ambayo ameyapata hajaoa bado anaamini siku moja watakuwa pamoja lakini msichana ameolewa. Lakini naye bado anampenda na kumwaza kila siku. Je hili ni sawa na kuachwa kwani nalo ninavyowaona linawauma sana je niwasaidiaje?

Anonymous said...

Kaka ubarikiwe sana, Cha msingi inabidi tuwe tunasamehe na kusahau kama hutasahau itakuwa hujasamehe.Tujiamini na kumuomba mungu kwa kila jambo. Siku njema wapendwa
Msafiri

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,
Hapo kuna mambpo mawili, kwanza kuumia kwa sababu wazazi hawamtaki mchumba wako hili kwa kweli halikubaliki kwani binti au kijana ana uhuru na haki ya kuoa au kuolewa na mtu anayemtaka yeye kuwakubali wazazi ni hiari yako hata hivyo maumivu ni maumivu tu inabidi uwasamehe na kusahau kama umekubaliana nao kwamba chaguo lako halikuwa sahihi na wakati huohuo bado unampenda mchumba wako. Kwa nini ukubali wazazi wakati wewe ndo umempenda kijana? kama kwa maumivu hajaoa hadi leo kweli hiyo kali, unampompenda mtu lolote linaweza kutokea je akifa? naamini anatakiwa kujikubali kwamba kwanza hakupena kwa makosa na pia unaweza kuanza maisha upya na kumpenda mwingine.
Kitu cha msingi ni kujikubali kwamba ameumia na asamehe na kuendelea na maisha yake kwani huwezi kupenda then usiumizwe.
Huyo anatakiwa kutiwa moyo kisaikolojia ameathirika sana kiasi kwamba anaona mapenzi hayana maana.

Yasinta Ngonyani said...

asante nitamsalimia rafiki yangu nadhani itamsaidia

Lazarus Mbilinyi said...

Sawa kabisa dadangu,
Kama nilivyotangulia kusema ni kwamba binadamu Mungu ametuumba tukiwa na uwezo wa ku -heal maumivu (hurt) yoyote.
Kosa kubwa rafiki yetu amefanya ameamini hawezi kupenda tena na kupata mtu ambaye atampa upendo tena kama mpenzi wake wa kwanza.
Hata hivyo anatakiwa akubali kwamba ameumua na hakufanya kosa kupenda na now it is over aanze ukurasa mpya kuenjoy maisha yake na kutafuta mtu ambaye anaweza kupendana naye. Ni ngumu ila hakuna lisilowezekana.

LM