"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, September 6, 2008

Si upendo tu bali kuelewa tofauti

Hata kama mwanaume na mwanamke wanapendana sana bila kujua tofauti zilizopo kati ya mwanaume na mwanamke bado migongano haiwezi kukwepeka. Wakati mwingine migongano inayotokea katika ndoa au mahusiano si kwa sababu wahusika wamepoteza upendo wa kweli baina yao bali ni kutofahamu tofauti iliyopo kati ya mwanaume na mwanamke.
Yaani wengi (si wote) hugombana, huzira, huumia, hukasirikiana, kukwazana na wakati mwingine kuzipiga si kwa sababu hatupendani bali hatufahamu tofauti kubwa zilizopo kati ya mwanamke na mwanaume.

Kwa nini mwanaume akipatwa na tatizo au shida au msongo wa mawazo huwa mkimya na kutotaka kuongea na mtu hata mpenzi wake?


Kwa nini njia nzuri kwake kujisikia relief (ahueni) ni kutoongea na wakati mwingine huamua kusoma gazeti au kuangalia TV au kutulia kimya peke yake?


Na je, kwa nini hata mke (au mpenzi wake) au mtu yeyote akiaanza kumuongelesha bado jibu analopata ni kwamba hata tatizo na anasema niache mwenyewe, wakati huohuo unajua kabisa huyu ana kitu kinamuumiza kwenye akili yake?

Je, unapomuongelesha unakuwa unamsaidia au ndo unazidi kumsumbua na kufanya awe mkali zaidi?

Kabla ya kupata majibu ya maswali hayo hebu tuanza kwa kuangalia tofauti za kawaida zilizopo kati ya wanawake na wanaume.

Wanawake hupenda kuongelea kuhusu watu, wakati wanaume hupenda kuongelea kuhusu vitu. Ndiyo maana umbeya mwingi hupatikana kwa wanawake kuliko wanaume (si wote).
Wanawake ni waongeaji wazuri faragha, wakati wanaume ni waongeaji wazuri mbele za watu. Ndiyo maana mara nyingi kwenye halaiki wanaume ndo videdea wa kuchonga.
Wanawake wanalia machozi mara tano zaidi ya wanaume, ndiyo maana ukiona mwanaume (si wote) anatoa chozi ujue leo yamemfika.

Wanawake ni wepesi kuomba msaada hasa wakipotea njia, wakati wanaume ni wagumu sana kuomba msaada wakipotea njia.
Wanawake huathiriwa sana na kuguswa na harufu, wakati wanaume huathiriwa sana na kile wanaona kwa macho.
Wanawake tangu mtoto mdogo huwa na uwezo wa kuongea huku anakuangalia machoni au usoni wakati wanaume huchelewa sana kuwa na hii sifa.
Wanawake huathiriwa sana na watu wengine, wakati wanaume hujiangalia yeye mwenyewe kwanza.
Wanaume (si wote) ni waongo kuliko wanawake.

Tutaendelea na kuangalia tofauti zilizopo!

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli kabisa halafu wanawake wana huruma sana. Siku nyingine unaposafiri uwe una aga

Lazarus Mbilinyi said...

Ni kweli ni muhimu sana kuaga unaposafiri kwani kuna wengine sala zao kwa Mungu ndo zinatufanya tuendelea kuishi na kuepushwa na ajali mbalimbali.
Ila wakati mwingine yaani mtu lazima kusafiri bila kupanga na unakosa muda wa kuwaaga watu beautiful kama wewe dada Yasinta.

Asante sana kwa maombi yako.

Fikirikwanza said...

Ukipata mke anaye nuna hivi ni safi sana ,anakupa muda wa kufanya mambo mengine kwani baadaye atafurahi kwa jinsi alivyo nuna vizuri. Cha msingi unatakiwa uwe na kamera karibu. Kumbukumbu!