"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, September 7, 2008

Tukikimbilia pangoni tuache!

Wengine mnaiga, wanaume ndo wanajua siri ya kukimbilia mapangoni wakipatwa na shida au matatizo ya msongo wa mawazo na wakitoka huko wanakuwa bomba sana. Moja ya tofauti kubwa kati ya wanaume na wanawake ni jinsi ya kukabiliana na msongo wa mawazo.
Mwanaume akiwa na msongo wa mawazo hujitenga, huwa mwenyewe na huwa mkimya na hataki kuguswa wala kuongeleshwa na mtu yeyote, wakati mwanamke hujisikia kuogopa na kuathirika kihisia.
Mwanaume hujisikia ahueni atakaposhughulikia tatizo lake yeye mwenyewe bila kuhitaji msaada wakati mwanamke hujisikia ahueni pale atakapokuwa anazungumza au kuongea kuhusu Matatizo yake na mtu mwingine anaweza kuwa mume wake au mtu yeyote anayemwamini.
Mwanaume akipata msongo wa mawazo iwe kukasirishwa kazini, au Matatizo yoyote hujitenga na kwenda kwenye pango (cave) lake katika akili zake ili kuendelea kupambana na kupata solution ya tatizo lake peke yake.
Huwa anakuwa anajihusisha zaidi na kushughulikia tatizo lake na kuwa kama vile amepoteza uwezo wa kutoa ushirikiano kwa mke au mpenzi wake kwa zaidi ya asilimia 95.
Hujitenga, huwa mbali kimawazo, huwa kama amejisahau kwamba ana mke ambaye anahitaji kumsikiliza.
Anakuwa yupo kimwili na si kiakili kwani asilimia 95 zinakuwa kwenye kushughulika na tatizo lake.
Akiwa katika hali ya msongo wa mawazo inakuwa ngumu sana kumpa mwanamke attention kubwa na hisia ambazo mwanamke anastahili.
Na ikiwa atapata solution kwa tatizo lake basi haraka sana atatoka kwenye pango lake ambapo alikuwa amejificha na kurudisha ushirikiano kwa mke au partner wake kama kawaida.
Na kama hatapata majibu ya Matatizo yake basi anaweza kukwama huko kwenye cave lake kwa muda mrefu zaidi.
Wakati mwingine ili wasikae muda mrefu kwenye pango utaona wanaume wanapenda sana kusoma magazeti, kuangalia news kwenye TV, kufanya mazoezi nk.

Kwa mfano!
Mzee Mlyabange na mkewe Tuladzuma wote wamerudi nyumbani hoi wakiwa na msongo wa mawazo baada ya mabosi wao kuwakasirisha huko kazini.
Baada ya kufika nyumbani Mzee Mlyabange anaamua kupoteza mawazo yake kwa kujisomea gazeti la Kilimo cha kisasa na hataki kabisa kusumbuliwa na mtu kwani bado anatafakari jinsi ya kupata solution baada ya bosi kumkasirisha kazini.
Wakati huohuo mkewe naye (Tuladzuma) baada ya kurudi home huku amechoka na kelele za bosi anataka kuongea na mumewe Mlyabange ili kupata ahueni ya visa vya bosi.
Hii ina maana kwamba Mzee Mlyabange baada ya kutatizwa na bosi ameamua kukimbilia kwenye cave lake hataki kuongeleshwa na mtu na wakati huohuo na mke wake naye (Tuladzuma) anataka kusikilizwa na mumewe kwani bosi naye kamjeruhi.
Bila shaka kila mmoja akiamua kufanya kile anataka hata kama wanapenda sana bado kutakuwa na zogo na kukwazana ajabu.
Mzee Mlyabange atadhani mkewe Tuladzuma anachonga sana na hataki kumpa muda, na Mke naye atamuona mzee hamjali na hataki kumsikiliza.

Hili ni tatizo la mahusiano mengi na ili kutatua tatizo hili haitategemea ni kiasi gani Mr. Mlyabange anampenda kiasi gani mkewe Tuladzuma bali ni kuhusiana na uelewa wao wa tofauti zilizopo kati ya mwanaume na mwanamke na jinsi ya kumpa mwenzake kile anastahili.
Mwanaume akipatwa na msongo wa mawazo au tatizo, kama wewe ni mwanamke kwanza utajua tu hasa jinsi anavyojiweka kivyake na hata ukimuuliza je, unatatizo lolote?
Bila shaka jibu utakalopata mwanaume atakwambia hakuna shida nipo safi tu na pia atakwambia shida yake haikuhusu wala usijali
(hata kama ni usiku wa manane usingizi hana bado atakwambia hakuna shida yoyote hapo hua jamaa yupo pangoni usimsumbue)
Ujue hapo yupo kwenye pango (cave) anahitaji muda wake mwenyewe ili ashughulikie tatizo lake.
Kuendelea kumsemesha ni sawa na kuendelea kumfuata kwenye cave lake na matokeo unaweza kuliwa au kuumizwa na nyoka anayelinda cave lake (hasira, matusi, kupigwa, kutokujibiwa chochote au kuvurugana kabisa)
Kitu cha msingi kama ni mwanamke ukishaona dalili za kuwa jamaa ameenda pangoni wewe ni kuachana naye, fanya vitu vingine kujipa raha zako mwenyewe ndipo utashangaa jamaa katumia muda kidogo kukaa huko mapangoni.

Kumchungulia mwanaume pangoni au kumfuata pangoni na hata kuendelea kumsemesha akiwa pangoni hakumfanyi awahi kutoka pangoni, bali kunaweza kusababisha akwame huko na kubaki huko kwa muda mrefu zaidi. Dawa ni kumpa muda wa kutosha na kuachana naye kabisa hadi amalize muda wake na atarudi mwenyewe.

1 comment:

Anonymous said...

Mimi sina mengi zaidi ya kusema Nashukuru kwa elimu hii unayotoa kwa watu ili kuhakikisha ndoa zetu zinakuwa zenye afya.
Na mungu Awabariki sana
MSAFIRI