"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, September 24, 2008

Wanaume Huchochea Mwendo!

Wanawake hupunguza mwendo wakati wanaume huchochea na kuongeza mwendo.
Wanawake hupenda kuguswa mwili mzima (mwili wake wote ni single sex organ) linapokuja suala la kusisimuana kimapenzi.
Ni mara chache sana wanaume hufahamu mwanamke anahitaji nini linapokuja suala la mapenzi na hata kama anafahamu basi akiingia chumbani baada ya muda kidogo anasahau na kuendelea kufanya kile anataka yeye.

Mwanamke anahitaji mwanaume mwenye mikono slow wakati wa kusisimuliwa na kuandaliwa kuwa tayari kwa tendo la ndoa, hata hivyo mwanaume akishakuwa amesisimka husahau na kuendelea kuwa na mikono mwepesi kukimbilia sehemu muhimu ambazo mwanamke husisimka zaidi akidhani wote wanahitaji mwendokasi sawa.
Ni jukumu la mwanaume kufahamu mahitaji ya mwanamke wakiwa faragha hii ni kuhakikisha mwanamke anaridhika kupata kile anastahili.

Tendo la ndoa ni uzoefu wa tofauti kwa mwanamke na mwanaume pia, raha anayoipata mwanaume hasa akishasisimka ni hitaji kubwa la kutaka kuingiza na kutoa (release), kama vile nguvu ya kutaka kutoa risasi kwenye bunduki.
Mwanamke yeye akishasisimka na kuwa wet huwa na hitaji kubwa la kupokea, yaani hitaji la kutaka kitu kuingia ndani yake.

Kwa kuwa mwanaume huwa na nguvu hasa ya kutaka kutoa sperms ili kufika kileleni hivyo akishasisimka tu anatamani kuingiza na kutoa, wakati huohuo mwanamke akishasisimka huwa anakuwa na hamu kubwa ya kupokea, kuingiziwa kitu na kujaziwa hadi aridhike, hivyo basi kama mwanaume ana mwendokasi na kumaliza haraka hitaji la mwanamke kutaka kujaziwa raha inaweza isifike mahali panapotakiwa na matokeo yake hujisikia ametumiwa tu na mwanaume kufanikisha raha yake ya kuingiza na kutoa vitu vyake.

Jambo la msingi ni kuhakikisha mwanamke anaandaliwa na kupokea raha ya kutosha hata kabla mwanaume yaja release na kumaliza raha yake.

Mwanaume anahitaji kuwa mtundu kuhakikisha anaanza kwanza na layers ambazo si sensitive moja baada ya nyingine huku akiwa na mikono slow ili kuhakikisha mwanamke anapata raha ya mwili mzima kabla ya kupokea kitu.

Kumbuka!
Mwitikio wa kusisimuliwa kwa mapenzi kwa mwanamke ni mzunguko unaohusisha saikolojia, mazingira na homoni pia anaweza kuathiriwa sana na hisia, mawazo, lugha, utamaduni na sababu za kibaolojia, hivyo kitu cha msingi ni kuhakikisha kabla ya kufika mbali ana hamu na anatamani tendo la ndoa.

2 comments:

Anonymous said...

Tafadhalini sana waungwana kuna kitu kinamsumbua rafiki yangu kwani yoko na mke pia mkwe wake yuko na shanga kiunoni na mkewe hunungunika kuwa jamaa hajui kuzitumia kaja kwangu nimuelekeze lakini masikini hata mimi sina nijualo. msaidieni jamani kama mnajua kuzitumia?
Msafiri

Anonymous said...

Mimi nadhani kama huku mke wake kwao shanga ni muhimu cha kufanya ni kumbwambia au kukaa na mume wake na kumfundisha (wanaume huwa hawapendi kufundishwa ingawa si wote) au anakae nae ameuelekeze ni jinsi gani anapenda huyo mumewe azitumie kwenye faragha yao.
Mapenzi ni kuelimisha na kufundishana kile unataka mwenzio akufanyie haina haja kuanza kulalamika nje wakati suala ni rahisi tu na lingeishia huko huko chumbani. Wakae pamoja kama wapenzi na amwelekeze mwenzake A- Z na kwamba hizo shanga jkwake ndo mapenzi hasa badala ya urembo tu wa kiunoni.
Mwanaume naye asidhani kufundishwa kitu na mwanamke basi ataonekana hajui mambo, ni muhimu kumtanguliza mke na kukubali ushauri wake then ampe kile anataka.
Mawasiliano ni muhimu sana kwao pamoja na kuwa wazi kila mmoja nini anataka.
Au ina maana huyo mwanamke ana shanga na hajui zinatumika hadi asimfundishe mumewe, Kumbuka shanga ni utamaduni wa baadhi ya watu wengine zina maana na wengine hazina maana kabisa.
Hakuna kisichowezekana wakiwa wazi na moyo wa kushauriwa.

Upendo daima