"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, September 8, 2008

Wanaume na kushauriwa!

Hata mwanaume anapoendesha gari tu, mwanamke inabidi kuwa makini unatoa ushauri baada ya kuombwa na yeye au unatoa tu kwa sababu unampenda?
Je, utajibiwa au mzee anaamua kula jiwe na kuumiza hisia zako? Ilitokea siku moja Mzee Mlyabange na Mkewe Tuladzuma walikuwa wanaendesha gari lao kuelekea kwenye sherehe za harusi posta mpya jijini DSM.
Mzee Mlyabange ndiye alikuwa anaendesha gari.
Wakati wanadhani wamefika eneo la sherehe ilidhihirika kwamba ni dhahiri walikuwa wamepotea njia.
Mara moja Mkewe Tuladzuma akamshauri mumewe waombe msaada kwa watu wawaelekeze jengo sahihi na sehemu sahihi ya sherehe, maajabu mumewe alijibakia kimya bila kuongea wala kujibu chochote.
Mzee Mlyabange aliendelea kuendesha huku anatafuta jengo hadi alifanikiwa kufika na kupata jengo sahihi la sherehe.

Kihisia mkewe Tuladzuma aliumia sana hasa kwa kitendo cha mumewe kubaki kimya na kuonesha kutomsikiliza na kumjali pale alikuwa anamshauri watafute msaada kuulizia njia na jengo sahihi.

Kwa upande wa mke wake (Tuladzuma) kitendo cha kutoa ushauri kwa mumewe ni kuonesha anampenda ndiyo maana alimshauri watafute msaada kwa watu wengine.
Na Mzee Mlyabange kwa upande wake alikuwa amekwazika sana na kitendo cha mkewe kumshauri kwani mzee alihisi kama vile mke wake hamuamini na hatamfikisha kwenye sherehe. Kwake haukuwa ushauri bali Dharau na kuelezea kwamba mwanaume hawezi.

Tofauti kubwa iliyopo kati ya wanawake na wanaume ni kwamba wanaume huwa hawapendi kupewa ushauri au kushauri mtu hadi wao wenyewe waombe.
Pia wanaume wana asili ya kujitatulia Matatizo yao wenyewe (kama kwenda pangoni) isipokuwa aombe mwenyewe.
Mkewe Tuladzuma hakujua kwamba kitendo cha mumewe kupotea njia hakikumaanisha apewe ushauri bali atiwe moyo na support kwamba atapata njia na kuonesha kumpenda zaidi.

Ukweli ni kwamba mwanamke katika ndoa au mahusiano anapoamua kutoa ushauri ambao hajaombwa (unsolicited) au kujaribu kusaidia kiushauri mwanaume bila kuombwa huwa hajui ni kiasi gani huwa inachukiza sana mwanaume na matokeo yake unaweza kuona mwanaume anakujibu kwa mkato au mwanaume anakula jiwe na kukuacha umeumia hisia zako.

Unapomshauri mwanaume kwa jambo dogo kama kuendesha gari na kupotea njia mwanaume hujiona kama vile umemdharau kwa jambo dogo sana je jambo kubwa utamuamini?

Tangu kale wanaume ni mafundi, ni wataalamu, ni heros, ni mashujaa, ni experts, ni watatuzi wa Matatizo sasa unapompa ushauri bila kuombwa ni kama unamfanya yeye hana lolote.

Naamini jambo la msingi ni wewe mwanamke kusoma saikolojia za mume wako na jinsi ambavyo huwa anaitikia ushauri wako, kwani kuna wakati unatakiwa kumtia moyo na kuonesha upendo kuliko kushauri au kulalamika tu kwamba hajaweza kufanya hiki na kile.

Pia kumbuka mwanaume kujiamini kwingi hutokana na mafanikio anayopata kutokana na ufanisi, uwezo na taaluma yake na kitendo cha kumshusha humuumiza sana.
Pia wanaume huwa hawapendi kuongelea kuhusu Matatizo yao hadi yeye mwenyewe akueleze na pia hupenda kutatua Matatizo kivyao kwani huamini kwamba likitokea tatizo lazima yeye ndiye atoe solution.

6 comments:

Power Up Love said...

I invite you to visit www.PowerUpLove.com a community of real people sharing real strories about how Love has really impacted and changed their lives. Please share your story, struggles, prayers requests, or testimonies.

Lazarus Mbilinyi said...

Thanks so much,
visited and is so glorious site full of blessings.
I have added in my blog/website list.

Thanks so much for the good work!

Yasinta Ngonyani said...

Nimeamini wanaume wengi hawapendi ushauri.Na pia hujifanya wanaweza kila jambo na pia wao ndio wanapenda kutoa ushauri kwa wengine bila kufikiri kwa nini yeye hapendi kushauriwa. labada ni kweli wanawake inabidi tuwasomee sana waume zetu kisaikolojia.

Lazarus Mbilinyi said...

Ni kweli dada Yasinta ni muhimu sana kwana kumfahamu mume wako yupo tofauti na wewe kivipi ndo uwe unapenda kumshauri kila kitu kwani usipofahamu unaweza kusema hataki kushauriwa na huwa hasikilizi kumbe hana tatizo lolote ni jinsi tu wewe unavyowasiliana naye bila kuzingatia wanaume wanatofautiana na wanawake kivipi.
Asante sana

Anonymous said...

Hali yako na familia kaka, Hope mlikuwa na wikendi njema na iliyobarikiwa na bwana, Nasi pia mungu yu panamoja nasi, Sina cha kusema ila tunashukuru kwa haya. Mbarikiwe sana.
Msafiri

Fikirikwanza said...

badala ya kwenda itandula anajikuta yupo kwa mzee hibwa. si unajua pale ng'anga story zinavyo kulea. childish things makes people feel happy.