"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, September 26, 2008

Wanautwika haraka!

Wanawake siku zote (si wote) wakinywa pombe kidogo tu hulewa na kuonekana wameutwika ile mbaya kuliko wanaume.
Wengine huenda mbali zaidi hata kujikojolea na kujisahau kabisa mahali walipo hubaki hapo hadi kilevi kitoke na wengine hata wakiutwika hukaa muda mrefu sana ili fahamu ziwarudie na fahamu zikirudi wengine huwa tayari mambo kadhaa mabaya wameshafanya au wamefanyiwa.
Why?
Timu ya wanasayansi ikiongozwa na Profesa Charles Lieber kutoka Mount Sinai School of Medicine New York Marekani, wamegundua kwamba wanawake wanakosa au wana upungufu mkubwa wa Enzyme ijulikanayo kwa jina la Gastric alcohol dehydrogenase (ADH), hii Enzyme huvunjavunja kilevi (alcohol) kabla ya kuingia kwenye damu.
Hii ina maana kwamba mwanamke akinjwa pombe kilevi huenda moja kwa moja kwenye damu bila kuchunjwa wala kuvunjwavunjwa kwanza kupunguza nguvu na sumu ambazo zinaweza kuwa kwenye pombe.

Pia wanatoa tahadhari kwamba wanawake wanaweza kuathirika zaidi na magonjwa yanayohusiana na ulevi haraka kuliko wanaume kama vile Cirrhosis ya Ini na Dementia

Pia wapo wanaume hutumia kilevi kama chambo kuwapata wanawake kwani wanafahamu kiwango sawa mwanamke hulewa zaidi.

Kumbuka ulevi ni mbaya kwa wanawake na wanaume husababisha familia mambo kwenda ndivyo sivyo.

Hutahukumiwa kwa kuwa ulikuwa mlevi bali kwa sababu ulikataa yule anayeweza kuondoa kiu ya kilevi yaani Kristo.
Dada kautwika hadi anajihisi yupo kwenye Queen bed yake home.
Pombe si chai au soda

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

wanawake wengi wanafikiri wanaweza kushindana na wanaume kumbe hawajua kama miili yao na pia kilo zimeachana sana. Angalia sasa mambo hayo hapo iko kazi kweli kweli.

Anonymous said...

Ni kweli dada Yasinta, wengi hudhani pombe ni chai, hata hivyo vituko tunavyoviona ni balaa, ngumi hupigwa, ngeu watu hupata, wengine hulala kwenye mitalu, wengine husabisha ajali za magari na wengine hugongwa na magari kwani wakiwa barabarani wanataka barabara nzima kuwa zao, wengine wakienda chooni ndo jumla piga mbonji hukohuko. Kazi kwelikweli.
By Mtwivila

ashura said...

Thats right mr mbilinyi. Also don't forget that changing hormonal levels at certain times during the menstrual cycle increases the level of alcohol in a female's body. A woman drinking the same amount of alcohol every day will have twice or more the level of alcohol in her blood during the middle of the menstrual cycle around the time of ovulation as she will at other times in her cycle. SHYROSE- MEMPHIS