"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, September 13, 2008

Wanawake tu!

Hapo ni wanawake tu, mwanaume huruhusiwi

Ni jambo la kawaida kutenganisha wanawake na wanaume wakiwa jela Prisons, mabweni, au kutumia vyoo, baadhi ya michezo na hata shule.
Hata hivyo kuna baadhi ya nchi utumiaji wa mabasi ya abiria (public transport) suala la kutenganisha wanaume na wanawake halikwepeki.
Abiria hutenganishwa aidha kwa kila jinsia kutumia mabasi yake ( wanaume mabasi yao na wanawake mabasi yao) au basi moja linalotenganisha wanaume mbele na wanawake nyumba.

Kuna nchi kama Japan, Misri, India, Taiwan, Brazil, Mexico, Belarus na ufilipino nk wameamua kutenganisha huduma ya mabasi kwa kuwa na mabasi ya wanawake (women only buses) na mabasi kwa ajili ya wanaume hii ni kutokana na vitendo vya kidhalilishaji ambavyo wanawake wamekuwa wanapata kutoka kwa wanaume wahuni na ili kunusuri hiyo hali sasa kila jinsia na mabasi yake.
Huu usafiri huweza kuwa muda wote au muda fulani katika siku na inaweza kuwa kwenye train (subway) au mabasiPicha juu Basi la wanawake mengine huendeshwa na wanaume na mengine huendeshwa na wanawake wenyewe.

Pia zipo baadhi ya dini hutenganisha waamuni wanawake na wanaume wakiwa kwenye ibada kiasi kwamba ibada inapoendelea hakuna kuonana wanawake na wanaume.
Na zipo dini zingine zimetenganisha milango ya kuingilia ndani ya nyumba zao za ibada.

Sijajua sababu hasa ni ipi, au wasitamaniane? yaani hadi kwenye nyumba za ibada?

Picha juu ni Wanafunzi wa shule (DSM) wakiwa wameduwaa baada ya Konda kuwaambia wakiingia tu angewafanyia kitu mbaya
(Globalpublishertz)


Wakati nchi kama Tanzania hata suala la mabasi ya wanafunzi limeshindikana Serikali ikiwa imeshona masikio kwa super glue na kushindwa kutatua hili tatizo.

je, hili la wanawake na kuwa na mabasi yao hasa kutokana na wanawake kudhalilishwa linaweza kufanyika?

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ama kweli sasa dunia imeharibika, tumwembe mungu atulinde wanawake. Inavyonekana mwisho wanawake hawatatoka hata nje. Tutakuwa kama wafungwa tena afadhali hata ya wafungwa huwa wanapewa ruhusu mara chache. Kazi kweli

Lazarus Mbilinyi said...

Naamini pia baadhi ya sehemu wanaume wanawadhalilisha wanawake kwa nsababu sheria ni butu hazina makali sana ndo maana wanawafanya vibaya.
Hata hivyo kwa nchi kama Tanzania ambapo wanafunzi tu wanshindwa kuwa na mabasi yao je wanawake?
Kazi bado ipo

Anonymous said...

Habari kaka, Uzalilishaji upo tu kila mara kwani hapo mwezi wa kwanza tu mwaka huu hapo Arusha kijana mmoja alipigwa na wananchi baada ya kumchafua mama mmoja kwenye makalio yake na shahawa baada ya kutokwa na udenda kwani walikuwa wamesimama na walikuwa wamebanana sana.
Msafiri