"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, September 22, 2008

Wewe Ungesemaje?

Nimeulizwa swali na mtoto wangu Emmanuel (Miaka 5); nimjibu bila kusitasita pia wazi kabisa kwa ukweli mtupu.
Ameniuliza:
Je, nani nampenda zaidi kati yake (Emmanuel) na mama yake (mke wangu)?
Ili kumjibu swali lake ilibidi nifikirie sana na kuwaza hadi miaka 80 ijayo na zaidi, pia miaka mingi hata kabla yeye mwenyewe hajazaliwa.

Nimemwambia wazi kabisa kwamba nampenda kwa sababu ni mtoto wangu, ila linapokuja suala la nani nampenda zaidi nimemwambia nampenda zaidi mama yake ambaye ni mke wangu na sababu kubwa ya msingi ya kumpenda zaidi mke wangu kuliko yeye ni kwamba;
Yeye kwanza alinikuta mimi tayari naisha na mama yake yaani alinikuta mimi naisha na mpenzi wangu ambaye ni mama yake na ataniacha na mama yake ambaye ni mke wangu akiwa mkubwa.

Ataenda kwa mke wake na huko nikitaka kuja au kumtembelea acha kuishi na yeye; nitatakiwa kumuomba ruhusa ili anikubali.

Ndiyo maana nampenda zaidi mama yake kwani yeye ni mpitaji tu siku akiwa mkubwa hata nimwambie abaki hatakubali au mke wake hatakubali hivyo nampenda zaidi mke wangu ambaye naweza hata kufia kifuani mwake.
Hii haina maana kwamba simpendi, nampenda sana na kumpa mahitaji yake na haki zake, ila likija suala la mke wangu yeye ni namba moja.

Je, mwenzangu ungeulizwa kati ya mke na mtoto au mume na mtoto yupi unampenda zaidi ungesemaje?
Na ungetoa sababu zipi?

9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mmh watoto mara nyingine wana maswali ambayo sisi watu wazima huwa hatuwazi mara nyingi. Nadhani jibu lako ulilomjibu ni sahihi kabisa hata mimi ningejibu hivyox2 pia mimi ningejibu nawapenda wote sawa sawa nadhani inategemea nani anajibu mama au baba. kumbuka uchungu wa mtoto aujua mama.mawazo yangu

Thinker said...

Swali ni Gumu japo mie binafsi naona ni vigumu to compare to things different. Wangekuwa wote ni watoto au wote no wake mtu basi swali lilikuwa sahihi na lingekuwa gumu kulijibu. lakini mtoto anapedwa kwa upendo wote kama mtoto na mke anapedwa kwa upendo wote kama mke. Pia upendo hauchagui na hauna upendeleo . Mimi ningejibu wote nawapenda . japo vigezo vinavyo elezea upendo juu ya kila mmoja wao ni tofauti!!

Lazarus Mbilinyi said...

Asante sana kwa maoni yenu,
Ukweli ni kwamba mtoto anapendwa kwa upendo wote kama mtoto na mke/mume anapendwa kwa upendo wote kama mke au mume.
Pia ukweli ni kwamba watoto wanawakuta na watawaacha wenyewe mke na mume mnaishi wenyewe hivyo ni vizuri kila mmoja mtoto na wanandoa kulifahamu hili.

Pia naamini ukimwambia mtoto unampenda mama yake au baba yake kuliko yeye nahisi kuna aina ya feelings anazipata kwamba baba au mama hanipendi hivyo kuathirika tangu mdogo kwamba sipendwi, ni vizuri kumwambia nakupenda sana sawa na mama au baba.
Hapa nilitaka kupata maoni kutoka kwa wenzangu ila nilimwambia nampenda sawa na mama yake ingawa moyoni mwangu najua ipo siku atanichana na mke wangu na yeye ataenda kwa mke wake na kuwa na watoto wao.
God bless u

George said...

kwa jinsi mtoto alivyokuuliza,watakiwa kumpenda mtoto zaidi kidogo ya mama,kwa sababu nina imani kuwa mtoto ni damu yako,ebu fikiri kama angekuuliza kati ya wewe(razalus) na mama(mkeo} unampenda nani zaidi?,pia kumbuka mke hutarikiwa,nawe kujikuta waoa mke mwingine.mtoto hatarikiwi.mtoto ni sehemu yako ya mwili.gmchibuga@gmail.com

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka George ujumbe wako umefika.

Upo sahihi kwamba mtoto ni damu yangu, naamini hata mama yake pia ana damu yake.
Ila kumbuka msingi wa ndoa ni kwamba mimi na mama yake ni kitu kimoja na kwamba bila mama yake asingekuwepo, angepatikana mtoto mwingine ila si yeye.
Kama unaamini katika talaka ni sahihi, na pia mke anaweza kufa na mtoto akabaki.
Bottom line inabaki kwamba mtoto lazima apendwe mia kwa mia na mama lazima apendwe mia kwa mia hakuna wa kidogo wala zaidi kwani kila mmoja anapata upendo unaostahili yaani upendo wa mtoto na upendo wa mke au mume.
Haiwezekani ukawa unampenda mmoja zaidi ya mwingine wakati mwingine ni mtoto na mwingine ni mama au baba.
Mtoto anapewa upendo wa kuwa mtoto na mama au baba anapewa upendo wa kuwa baba au mama na hakuna kuingiliana.

Ila ni kweli hapa panachanganya kidogo, anyway ndo kunoa ubongo.

Ubarikiwe

Mary Damian said...

Huyu mtoto na swali lake.. Mimi ningejibu nawapenda wote. Lakini akiuliza nichague nani zaidi nitajibu babako oooh au yeye (mtoto), Jamani sijui, nimjibuje, nitasema nawapenda wote.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Mary,

Ukweli ni kwamba mama/baba ana upendo wake na mtoto anaupendo wake na huwezi kuuunganisha pamoja, upo sahihi kila mmoja unampenda ingawa katika ukweli bado kuna watu wanawapenda watoto kuliko mmoja ya wanandoa.

Ubarikiwe

jingo said...

swali i gumu kwani huyu mtoto wako amekuuliza lile swali gumu liliopata kutungiwa nyimbo na wasanii kwamba katikati ya bahari wewe utamuokoa nani?
kwamba mama(mke wako) na yeye(mtoto wako)wanataka kuzama baharini nawe unauwezo wa kumuokoa mtu mmoja tu,je utamuokoa nani?
naona umekuwa wazi kuwa utamuokoa mama(mke wako)ni swali gumu sana!
linahitaji busara sina tatizo na ulivyolijibu na maelezo uliyompatia mtoto yanajitosheleza na kuridhisha!

Lazarus Mbilinyi said...

Jingo,
Asante kwa majibu mazuri na comments nzuri, ukweli kila mmoja ana upendo wake, mke au mume ana nafasi yake na upendo wake na mtoto naye vilevile na ni vizuri mtoto akajua kwamba baba na mama wanapendana na ni mke na mume na pia akajua kwamba baba na mama wanampenda kama mtoto wao.

Asante sana